Hivi dini ni imani au ni jina?

Hivi dini ni imani au ni jina?

Hivi unabatizwa na kukubali kuwa Askari wa Yesu Kristo na baadae unamkana!
Hakuna muislamu anayemkana Masih Issa (Yesu Kristo), kinachokanwa ni uungu wake au kuwa mtoto wa Mungu, lakini waislamu wote wanaamini Masih Issa bin Maryam ni mtume wa Mwenyezi Mungu aliyezaliwa bila ya baba, aliyefufua na kuwaponya vipofu wenye ukoma na balanga kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na aliyepaishwa kwa Mwenyezi Mungu na atarudi duniani tena kwa mara ya pili ili akamilishe kile alichokiacha.
 
Hauwezi ukawa muislam alafu ukaitwa Paulo.
Au ukawa mkristo ukaitwa Hassan.
Yaani hainogi.unaweza siku ukapata matatizo watu wakashindaa kukusaidia.
Au unaweza ukaenda sehemu ukafa.
Watu wanakuja una jina la kikristo kumbe muislam.
Mwisho wa siku utazikwa kikristo wakati ni muislam
Raha gani...Dini Ni imani na imani Ni matendo..nikiitwa Ndumilakuwili..kunashida gani...Kama nimuislimu na nafuata Dini..

Wangapi wanahayo majina na wamebaki kuwa waisilamu majina..
 
Hauwezi ukawa muislam alafu ukaitwa Paulo.
Au ukawa mkristo ukaitwa Hassan.
Yaani hainogi.unaweza siku ukapata matatizo watu wakashindaa kukusaidia.
Au unaweza ukaenda sehemu ukafa.
Watu wanakuja una jina la kikristo kumbe muislam.
Mwisho wa siku utazikwa kikristo wakati ni muislam
Aisee...Wewe hujui kutu...HAKUNA KITU KAMA HICHO. Jina Sio utambulisho wa Dini...Ni jinsi unavyoishi na matendo yako.
Wangapi wanaitwa Paulo hawaendi kanisani Wala misikitini waanabudu wanavyovijua..

Jina Sio Dini ..Wewe mwenyewe unaweza kuwa na jina la kiislamu lakini hamna unachofuata kwenye Dini yako...zaidi ya kucomment vitu usivyo vijua.

Wale maswahaba walivyosilimu nani aliwabadilisha majina?..
Haya Mambo ya kumbadilisha majina..nikuwafanywa waisilamu kuwa waisilamu majina na Sio vitendo
 
Dada yangu, ni vizuri kwa mtu aliyesilimu kuchagua jina la Kiislam kwa ajili ya utambulisho wake lakini pia tumeambiwa tuchague majina mazuri.

Pia kuna wakati mtu atalazimika kubadili jina mfano mtu anayetumia jina katika majina ambayo ni maalum kwa Allah tu. Mfano mtu kuitwa Al-Khaaliq (Muumba) au Ar Razzaq (Mwenye Kuruzuku). Hii haifai.

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbadilisha mtu aliyesilimu aliyekuwa akiitwa Abul-Hakam (baba wa Hukumu) akimwambia kuwa Allaah Pekee Ndiye Mwenye sifa hiyo ya Al-Hakam, na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza kama ana watoto na majina yao, yule mtu akataja wanawe watatu, Shurayh, Muslim na 'Abdullaah. Basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Kuanzia leo wewe ni Abuu Shurayh.” [Abu Daawuwd].

Ni vyema kuwaita watoto au kuwaita watu (mfano aliyesilimu) kwa majina ya Allah kwa kufuatanisha na neno 'Abd (Mja). Mfano kumuita mtu 'Abdur-Razzaaq (Mja wa Mwenye Kuruzuku) au 'Abdu-Allah (Mja wa Allah).

Inafaa kwa mtu kutumia majina ambayo ni sifa za Allah lakini pia ya WanaAdamu kama vile Maalik (Mfalme).

Haifai pia mtu kujiita au kuitwa 'Abdur-Rasul (Mja wa Mtume) au 'Abdun-Nabbiy (Mja wa Nabii) au 'Abdul-Hussain (Mja wa Hussain), kwa sababu uja ni wa Allah pekee na si wa kiumbe chochote. Majina yenye Shirki hayafai. Hata Swahaba Abu Hurayrah alikuwa akiitwa 'Abdush-Shams (Mja wa Jua) lakini aliposilimu Mtume alimbadilisha jina akamuita 'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rehma)

Mtu Mwenye jina lenye maana mbaya pia halifai. Na Uislam unamruhusu mtu kubadilisha jina lolote lenye maana mbaya hata kama alipewa na wazazi wake.

Mengi katika niliyoandika nimeyatoa Alhidaaya.com.

Soma pia yafuatayo kwa faida zaidi;

Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto

Jamii

Fiqh Ya Majina Ya Watoto

www.alhidaaya.com

Ni Sunnah kutunza jina zuri, na katika majina mazuri ni:

'Abdullaah (Mja wa Allaah Subhanahu wa Ta'aala)

na

'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rahmah);

na majina ya ki kweli hasa ni:

Al- Haarith (Anayezaa)

na

Humaam (Hodari);

na majina mabaya zaidi ni:

Harb (Vita)

na

Murrah (Chungu)

Hadiyth ifuatayo imethibitisha:

((Majina yanayopendezewa kwa Allaah (Subhaana wa Ta'aala) ni 'Abdullaah na Abdur-Rahmaan.)) [imeripotiwa na Muslim.

Kwa Abu Daawuud kuna nyongeza((Na majina ya ki kweli hasa ni Al-Haarith na Humaam, na mabaya zaidi ni Harb na Murrah)).

Na majina mabaya, na yale ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao, ni makuruhu (Yasiyopendeza), kama vile:

Nujayh (fanikiwa),

Barakah (baraka),

Kulayb (kijimbwa),

Harb (vita),

Murrah (chungu),

Shihaab (kimondo),

Himaar (punda),

Aflah (fanikiwa sana),

Yasaar (wepesi),

Rabaah (faida), na

Naafi` (kunufaika)

na majina kama:

Sittun-nisaa (mwanamke wa wanawake wote) ni yanayogombezewa sana.

Na Mfalme wa Wafalme limekatazwa, kama ilivyokuwa:

'Shahenshaah',

na

Aqdhwaal-Qudhwaat (hakimu wa mahakimu).

Na inapendelewa kubadilisha majina mabaya na ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao.

Na inapendelewa kwa mtoto wa kiume, mwanafunzi au mfanyakazi kutomwita kwa jina lake, na kwamba watu wazuri (wanaume na wanawake) wawe wana kun-yah, hata ikiwa hawana watoto wa kiume, na kun-yah huhusiana na mtoto wa kiume wa mwanzo.

Na imekatazwa kuwa na Kun-yah ya 'Abul-Qaasim kwa mtu ambaye jina lake ni Muhammad na vile vile kwa watu wengine, katika kipindi cha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vile vile baadae ya hapo.

Tanbihi:

Kuna khitilafu baina ya madhehebu juu katika nukta hii- wengine wameshika kwamba katazo lake (kutumia kun-yah ya Abul-Qaasim) liliwekwa katika kipindi cha uhai wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tu na si baada ya kufariki.

Na aliyeruka mipaka (faasiq) au mzushi asipewe kun-yah mpaka kukiwepo hofu ya fitnah, au ikiwa kwa sababu ya utambulishi, (kama vile Abu Lahab).

Na inapendelewa kwamba mtu asitumie kun-yah yake pekee (yaani bila ya kutimiza jina lake pia), isipokuwa akiwa anajulikana kwa kun-yah yake na sio kwa jina lolote isipokuwa hilo.

Na pia imekatazwa (Haraam) kumtania mtu kwa jina ambalo halipendi. Kama ikiwa anajulikana kwa jina jengine (ambalo halimchukizi) na hata kama jina hilo lina dhamiria kitu ambacho kinamhusu yeye ambacho ni cha kweli.

Kun-yah (Lakabu au Jina la kupachika)

Ushahidi uliombwa wa kuchukuliwa kun-yah kuwa ni Sunnah. Kuna vidokezo mbali mbali juu ya hili katika Hadiyth.

Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kun-yah, na hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba kuwa na kun-yah ilikuwa kwa yeye pekee, na hii ndio inayoamua ni Sunnah (kumfuata mtu katika kitu ambacho hakikua kwa ajili yake pekee (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Zaidi, kuna Hadiyth iliyoripotiwa na At-Tirmidhiy katika "Ash-Shamaail"

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita mvulana mdogo kwa kun-yah, kuonyesha kwamba si muhimu kuwa na mtoto kabla ya kutumia kun-yah.

Mazungumzo zaidi ya Hadiyth hizi yanapatikana katika Fat-h al-Baariy (maelezo ya Swahiyh Al-Bukhaariy).
 
Kuna watu wanatafuta kufanana na waarabu. Ndio hao wanafanya assimilation, tena ukikaa vibaya nadhani wanaweza hata kujichubua na kuweka nywele relaxer ili wafananie na waarabu kabisa.
Ungewataja Hao watu wanaofanana na waarabu ingekuwa vizuri na si kuleta umbeya kama Juma luk@le
 
Napataga kigugumizi sana nikisikia mtu kabadili dini kisha anabadilisha na jina,eti jina la kiislam au la kikristo.

Kwani ukibaki na jina lako na kuendelea na ibada za kumuabudu Mungu kwani haikubaliki? Nimebahatika kwenda Japan,China na Russia. Nimekuta kuna waislaam wengi na wakristo, ila sijakuta mtu anaitwa Muhammad au William.

Kumjua mtu dini yake hadi umuulize lakini sio kwa jina. Sasa tunaomini hivyo tunakwama wapi?
Huo ni uamuzi wa mtu mkuu.

Mtu unaweza kuitwa machepe na ukawa muislamu.

Unaweza kuitwa saidi na ukawa mkristo.

Hata waarabu wa zamani kabla ya kuwa waislamu walikuwa na majina yao na baada ya kusilimu wengi walibaki na majina yao yale yale kuomesha kuwa jina sio shida katika uislamu.shida ni matendo na imani yako
 
Dada yangu, ni vizuri kwa mtu aliyesilimu kuchagua jina la Kiislam kwa ajili ya utambulisho wake lakini pia tumeambiwa tuchague majina mazuri.

Pia kuna wakati mtu atalazimika kubadili jina mfano mtu anayetumia jina katika majina ambayo ni maalum kwa Allah tu. Mfano mtu kuitwa Al-Khaaliq (Muumba) au Ar Razzaq (Mwenye Kuruzuku). Hii haifai.

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbadilisha mtu aliyesilimu aliyekuwa akiitwa Abul-Hakam (baba wa Hukumu) akimwambia kuwa Allaah Pekee Ndiye Mwenye sifa hiyo ya Al-Hakam, na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza kama ana watoto na majina yao, yule mtu akataja wanawe watatu, Shurayh, Muslim na 'Abdullaah. Basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Kuanzia leo wewe ni Abuu Shurayh.” [Abu Daawuwd].

Ni vyema kuwaita watoto au kuwaita watu (mfano aliyesilimu) kwa majina ya Allah kwa kufuatanisha na neno 'Abd (Mja). Mfano kumuita mtu 'Abdur-Razzaaq (Mja wa Mwenye Kuruzuku) au 'Abdu-Allah (Mja wa Allah).

Inafaa kwa mtu kutumia majina ambayo ni sifa za Allah lakini pia ya WanaAdamu kama vile Maalik (Mfalme).

Haifai pia mtu kujiita au kuitwa 'Abdur-Rasul (Mja wa Mtume) au 'Abdun-Nabbiy (Mja wa Nabii) au 'Abdul-Hussain (Mja wa Hussain), kwa sababu uja ni wa Allah pekee na si wa kiumbe chochote. Majina yenye Shirki hayafai. Hata Swahaba Abu Hurayrah alikuwa akiitwa 'Abdush-Shams (Mja wa Jua) lakini aliposilimu Mtume alimbadilisha jina akamuita 'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rehma)

Mtu Mwenye jina lenye maana mbaya pia halifai. Na Uislam unamruhusu mtu kubadilisha jina lolote lenye maana mbaya hata kama alipewa na wazazi wake.

Mengi katika niliyoandika nimeyatoa Alhidaaya.com.

Soma pia yafuatayo kwa faida zaidi;

Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto

Jamii

Fiqh Ya Majina Ya Watoto

www.alhidaaya.com

Ni Sunnah kutunza jina zuri, na katika majina mazuri ni:

'Abdullaah (Mja wa Allaah Subhanahu wa Ta'aala)

na

'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rahmah);

na majina ya ki kweli hasa ni:

Al- Haarith (Anayezaa)

na

Humaam (Hodari);

na majina mabaya zaidi ni:

Harb (Vita)

na

Murrah (Chungu)

Hadiyth ifuatayo imethibitisha:

((Majina yanayopendezewa kwa Allaah (Subhaana wa Ta'aala) ni 'Abdullaah na Abdur-Rahmaan.)) [imeripotiwa na Muslim.

Kwa Abu Daawuud kuna nyongeza((Na majina ya ki kweli hasa ni Al-Haarith na Humaam, na mabaya zaidi ni Harb na Murrah)).

Na majina mabaya, na yale ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao, ni makuruhu (Yasiyopendeza), kama vile:

Nujayh (fanikiwa),

Barakah (baraka),

Kulayb (kijimbwa),

Harb (vita),

Murrah (chungu),

Shihaab (kimondo),

Himaar (punda),

Aflah (fanikiwa sana),

Yasaar (wepesi),

Rabaah (faida), na

Naafi` (kunufaika)

na majina kama:

Sittun-nisaa (mwanamke wa wanawake wote) ni yanayogombezewa sana.

Na Mfalme wa Wafalme limekatazwa, kama ilivyokuwa:

'Shahenshaah',

na

Aqdhwaal-Qudhwaat (hakimu wa mahakimu).

Na inapendelewa kubadilisha majina mabaya na ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao.

Na inapendelewa kwa mtoto wa kiume, mwanafunzi au mfanyakazi kutomwita kwa jina lake, na kwamba watu wazuri (wanaume na wanawake) wawe wana kun-yah, hata ikiwa hawana watoto wa kiume, na kun-yah huhusiana na mtoto wa kiume wa mwanzo.

Na imekatazwa kuwa na Kun-yah ya 'Abul-Qaasim kwa mtu ambaye jina lake ni Muhammad na vile vile kwa watu wengine, katika kipindi cha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vile vile baadae ya hapo.

Tanbihi:

Kuna khitilafu baina ya madhehebu juu katika nukta hii- wengine wameshika kwamba katazo lake (kutumia kun-yah ya Abul-Qaasim) liliwekwa katika kipindi cha uhai wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tu na si baada ya kufariki.

Na aliyeruka mipaka (faasiq) au mzushi asipewe kun-yah mpaka kukiwepo hofu ya fitnah, au ikiwa kwa sababu ya utambulishi, (kama vile Abu Lahab).

Na inapendelewa kwamba mtu asitumie kun-yah yake pekee (yaani bila ya kutimiza jina lake pia), isipokuwa akiwa anajulikana kwa kun-yah yake na sio kwa jina lolote isipokuwa hilo.

Na pia imekatazwa (Haraam) kumtania mtu kwa jina ambalo halipendi. Kama ikiwa anajulikana kwa jina jengine (ambalo halimchukizi) na hata kama jina hilo lina dhamiria kitu ambacho kinamhusu yeye ambacho ni cha kweli.

Kun-yah (Lakabu au Jina la kupachika)

Ushahidi uliombwa wa kuchukuliwa kun-yah kuwa ni Sunnah. Kuna vidokezo mbali mbali juu ya hili katika Hadiyth.

Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kun-yah, na hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba kuwa na kun-yah ilikuwa kwa yeye pekee, na hii ndio inayoamua ni Sunnah (kumfuata mtu katika kitu ambacho hakikua kwa ajili yake pekee (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Zaidi, kuna Hadiyth iliyoripotiwa na At-Tirmidhiy katika "Ash-Shamaail"

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita mvulana mdogo kwa kun-yah, kuonyesha kwamba si muhimu kuwa na mtoto kabla ya kutumia kun-yah.

Mazungumzo zaidi ya Hadiyth hizi yanapatikana katika Fat-h al-Baariy (maelezo ya Swahiyh Al-Bukhaariy).
Sawa tunatakiwa.kuwa na majina mazuri..Sasa nikuulize jina Ben Ni baya?..

Mtu kubadili dini Natakiwa nianze kuap.kwa wanasheria kubadili vyeti vyangu vyote na documents ?

Mnasema Dini Ni nyepesi..huoni.huu.mchakato.mzima.wa kuaapa na nk... Inafanya Mambo yawe magumu..

Kabadili jina Inafaida gani katika dini ya Uislamu?...Je nikibadili jina ndo napendwa na Allah...Au Ni matendo yangu na bidii yangu ya kujifunza Dini na kufanyia kazi Elimu yangu?

Mnafanya mamabo magumu..wakati dini Ni nyepesi.

mtu.kuwa mchamungu haina uhusiano na Jina lake...Ndo maana.mimi watoto Wangu nawapa.majina ya.kikabila...sioni sababu ya kuwaita hayo.majina ya Kiarabu eti ndo watakuwa wachamungu.
 
Issa na Yesu Kristo ni watu wawili tofauti kabisa.
Hakuna muislamu anayemkana Masih Issa (Yesu Kristo), kinachokanwa ni uungu wake au kuwa mtoto wa Mungu, lakini waislamu wote wanaamini Masih Issa bin Maryam ni mtume wa Mwenyezi Mungu aliyezaliwa bila ya baba, aliyefufua na kuwaponya vipofu wenye ukoma na balanga kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na aliyepaishwa kwa Mwenyezi Mungu na atarudi duniani tena kwa mara ya pili ili akamilishe kile alichokiacha.
 
Hata Mungu alibadili majina ya watu alipowakusudia jambo fulani... mfano Abrahamu aliitwa Ibrahimu, Sarai aliitwa Sara na Yakobo aliitwa Israeli.

Japo Mungu alikuwa hamaanishi 'dini' katika tafsiri yetu, lakini ilimpasa kubadili majina... hii ni kwa mujibu wa Biblia.
Hizo ni hadithi tu,😁😂El ni mungu wa kipagani
 
Sawa tunatakiwa.kuwa na majina mazuri..Sasa nikuulize jina Ben Ni baya?..

Mtu kubadili dini Natakiwa nianze kuap.kwa wanasheria kubadili vyeti vyangu vyote na documents ?

Mnasema Dini Ni nyepesi..huoni.huu.mchakato.mzima.wa kuaapa na nk... Inafanya Mambo yawe magumu..

Kabadili jina Inafaida gani katika dini ya Uislamu?...Je nikibadili jina ndo napendwa na Allah...Au Ni matendo yangu na bidii yangu ya kujifunza Dini na kufanyia kazi Elimu yangu?

Mnafanya mamabo magumu..wakati dini Ni nyepesi.

mtu.kuwa mchamungu haina uhusiano na Jina lake...Ndo maana.mimi watoto Wangu nawapa.majina ya.kikabila...sioni sababu ya kuwaita hayo.majina ya Kiarabu eti ndo watakuwa wachamungu.
Dada yangu, umesoma vizuri nilichokiweka?
 
Sio lazima kwa aliyesilimu kubadili jina lake anaweza kubaki na jina lake la kabla ya kusilimu, ila inapendeza zaidi akachagua katika majina mazuri ya Kiislam.

Vile vile kuna kuna majina mtu hatakiwi kujiita au kuitwa katika Uislam. Mifano nimetoa katika comment yangu hapo juu. Sasa kama mtu amesilimu na kabla ya kusilimu alikuwa akiitwa jina ambalo katika Uislam halifai analazimika kubadilisha. Na hata kama ni Muislam aliyepewa jina ambalo halifai na wazazi au walezi wake mfano lina shirki ndani yake, analazimika kujibadilisha akijua hilo.

Nikakupa na mifano mfano mmoja ni wa Swahaba Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'Anhu), kabla ya kusilimu alikuwa akiitwa 'Abdush-Shams (Mja wa Jua). Aliposilimu, Mtume ( Swalla Allahu 'Alayhi Wa Sallam) akambadilisha akamuita 'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rahma).

Nadhani hapo utakuwa umenielewa kidogo dada yangu.

Allah akubariki na azidi kukuongoza katika Haqq wewe na sisi sote.
 
Dada yangu, umesoma vizuri nilichokiweka?
Nimekisomaaa...Na kwa muhtasari tunataiwa tuwe na majina mazuri..na majina ambayo hayana sifa za Umungu..hicho ndo nilicho elewa.

Lakini SI LAZIMA KUBADILI JINA Kama halina sifa hizo mbili.
 
Elimu yangu katika dini bado ni ndogo mno dada yangu. Ngoja nijaribu kuwaita baadhi ya watu ambao nawadhania kuwa ni wenye elimu kidogo ya dini wakufafanulie zaidi InshaAllah. Cc Jurjani Abuu Dharr Kazakh destroyer
 
Napataga kigugumizi sana nikisikia mtu kabadili dini kisha anabadilisha na jina,eti jina la kiislam au la kikristo.

Kwani ukibaki na jina lako na kuendelea na ibada za kumuabudu Mungu kwani haikubaliki? Nimebahatika kwenda Japan,China na Russia. Nimekuta kuna waislaam wengi na wakristo, ila sijakuta mtu anaitwa Muhammad au William.

Kumjua mtu dini yake hadi umuulize lakini sio kwa jina. Sasa tunaomini hivyo tunakwama wapi?
Asalam alaykum warahmatullah wabarakatuh

Neno ,DINI, ni neno la kiarabu lenye maana ya njia,
Lkn sio njia ya kwenda kwa akina mshana Hapana ni njia ya kumuelekea mwenyezi mungu,

Neno uislam maana yake ni

,UNYENYEKEVU,

lkn unyenyekevu huo ni mbele ya mungu(Allah)

Kwa maana hiyo huwezi kuwa mnyenyekevu kwa muumba ikiwa ww hauna dini, na kama hauna dini hauna imani , na kama hauna imani chochote utafanya, ndio maana kuna waislam licha ya kubadili dini na kuwa wakristo bado hawali ngurue kwa sababu kuna imani Fulani inawakataza bado ipo ndan ya nafsi yao , kwa hiyo dini ni msingi wa kila kitu , ukibadili dini badili na jina huo ndio uhalisia, kristo maana yake ni mpakwa mafuta ,sasa , hakuna kitu chenye nguvu ktk watu wenye imani thabiti kama dini
 
Dini ni Imani, lakini pia inaweza kuwa a central part ya utambulisho wa mtu.
Utambulisho unahusisha: Jina, mavazi, utamaduni n.k.

Umetoa mfano wa Wachina, Wajapani na Warusi kwamba huwezi kukuta mtu anaitwa Muhammad au William japo baadhi yao wana dini zao za Kiislam na Kikiristo.

Yawezekana ikawa kweli, lakini ukizama sana utakuta hayo majina yao yana vielementi vya Uislam au Ukristo na wenyewe wanajua huyu ni wa imani yangu na yule siyo wa imani yangu.
Kwa kuongezea wachina wanaokuja kufanya kazi africa ujiita majina kama john nk na ukiwauliza wanakwambia jina lake la kichina ni sawa na john au wiliam
 
Elimu yangu katika dini bado ni ndogo mno dada yangu. Ngoja nijaribu kuwaita baadhi ya watu ambao nawadhania kuwa ni wenye elimu kidogo ya dini wakufafanulie zaidi InshaAllah. Cc Jurjani Abuu Dharr Kazakh destroyer
Nimeitikia wito kaka.

Hadithi imekuja, inatuhimiza ya kuwa tuwape watoto wetu majina mazuri, na mtume akataja majina kama vile "Abdillah na Abdulrahman". Jina Abdulrahman ni zuri sana kuliko majina ya kikabila, sababu lina maana.

Kuna majina mazuri na kuna majina mabaya,mtume wa Allah alikuwa anawabadilisha watu majina ambayo yalikuwa mabaya na yenye shirki ndani yake.

Ila kama jina lina maana nzuri halina haja ya kulibadili, na wapo watu wengi walikuwa Wakristo walipo ingia katika Uislamu hawakubadili majina ya wazazi wao. Hapa wapo watu walikuwa wakiingia Uislamu wanabadili mpaka majina ya wazazi wao na hili ni kosa, ila jina la mwanzo unaruhusiwa kubadili. Sababu mzazi wako habadiliki. Mfano kuna brothers kobao unamkuta anaitwa "Bilal Davis" au "Musa Richardson" na mfano wake.

Utaratibu mzuri wa kuwapa watoto majina ukisoma kitabu kiitwacho "Tasmiyaat al Mawluud" ameelekeza umpe mtoto wako majina ya mitume, wake zao, watoto zao, ukikosa huko wape majina ya maswahaba au walio wafata maswahaba yaani kwa ujumla majina ya wajawema. Huu ndiyo utaratibu mzuri, na huwezi kukosa majina mazuri huko.

Mimi watoto wangu siwezi kuwapa majina ya kikabila sababu mengi hayana maana, na majina mazuri yako mengi.
 
Elimu yangu katika dini bado ni ndogo mno dada yangu. Ngoja nijaribu kuwaita baadhi ya watu ambao nawadhania kuwa ni wenye elimu kidogo ya dini wakufafanulie zaidi InshaAllah. Cc Jurjani Abuu Dharr Kazakh destroyer
Nimeitikia wito kaka.

Hadithi imekuja, inatuhimiza ya kuwa tuwape watoto wetu majina mazuri, na mtume akataja majina kama vile "Abdillah na Abdulrahman".

Kuna majina mazuri na kuna majina mabaya,mtume wa Allah alikuwa anawabadilisha watu majina ambayo yalikuwa mabaya na yenye shirki ndani yake.

Ila kama jina lina maana nzuri halina haja ya kulibadili, na wapo watu wengi walikuwa Wakristo walipo ingia katika Uislamu hawakubadili majina ya wazazi wao. Hapa wapo watu walikuwa wakiingia Uislamu wanabadili mpaka majina ya wazazi wao na hili ni kosa, ila jina la mwanzo unaruhusiwa kubadili. Sababu mzazi wako habadiliki. Mfano kuna brothers kobao unamkuta anaitwa "Bilal Davis" au "Musa Richardson" na mfano wake.

Utaratibu mzuri wa kuwapa watoto majina ukisoma kitabu kiitwacho "Tasmiyaat al Mawluud" ameelekeza umpe mtoto wako majina ya mitume, wake zao, watoto zao, ukikosa huko wape majina ya maswahaba au walio wafata maswahaba yaani kwa ujumla majina ya wajawema. Huu ndiyo utaratibu mzuri, na huwezi kukosa majina mazuri huko.

Mimi watoto wangu siwezi kuwapa majina ya kikabila sababu mengi hayana maana, na majina mazuri yako mengi
Issa na Yesu Kristo ni watu wawili tofauti kabisa.
Uwe unaandika mambo ambayo ukiombwa ushahidi unaweza kutupa. Siyo unaandika huu ujinga ambao mpaka unakufa huwezi kuuthibitisha.
 
Back
Top Bottom