Hivi desturi ya Kujenga nyumba nje nzuri ndani ovyo tumeitoa wapi Tanzania

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Watanzania wengi tunamatatizo ya Ushamba hasa katika ujenzi wa nyumba, kiukweli sisi ambao tumekulia sana nchi za nje tunaona mambo ni tofauti sana.

Katika ujenzi wa nyumba hapa nchini, nyumba nyingi ni nzuri sana kwa nje na zimejengwa kwa gharama kubwa nje kuliko ndani, utadhani huko nje ya nyumba ndo tunakaa muda mwingi, hii yote wanafanya kwa kurusha roho wapita njia na majirani huku wengine ndani kukiwa ni pahovyo mno, wengine wanapaka rangi nje ndani hajapaka.

Uzuri wa nyumba unapaswa kuwa ndani ya nyumba ambapo ndo utakuwa unatumia muda wako mwingi wa maisha. Tujaribu kupiga kwa Wenzetu wa Dunia ya Tatu, mambo ya Ushamba tuyaache na tuangalie basics.

Sasa tubadilike
 
Hiyo ni taswira ya mtu mnafiki. Au hamjitambui?

Pia picha yenu ya kutokuweka akiba majumbani, inasomeka kwa namna ambavyo Mvua zinanyeshaga, mafuriko yanaleta madhara hadi mnanachangia wahanga wa mafuriko na miezi michache baadae, umeme hakuna, mgao eti maji yamefanya nini nini sijui. Magufuli akaona mbali akaja na ujenzi wa bwawa lakini leo anatukanwa na watu wanaodhani wataishi duniani milele ama kana kwamba mbinguni anamiliki shetani!

Kukosa mipango ama kuwa na mipango ya maneno maneno tu, utekelezaji na ufuatiliaji sifuri. Kazi za kuzima moto! Huku nako kunadhihirika katika mambo mengi likwemo la mamlaka za ardhi, kushindwa kupima miji kwa mujibu wa master plans, badala yake wanakwenda kupima watu wakishajiamulia kujenga watakavyo. Halfu baadaye wanasema "ujenzi holela",. Au watu wanajenga pasipostahili, wanasaidiwa kupelekwa na miundombinu kama masoko, barabara, umeme, maji na kodi tunachukua halfu shortly baadaye wanaambiwa bomoeni mmejenga kwenye open space, mara, mabondeni, mara, mhhhhhh!.

Miji imejaa viraka viraka hadi katiba, lakini watu wanasimama bila aibu, mishipa imewatoka wakisema "hii ni sawa".

Sasa tunafikia kukopa fedha ili tulipe madeni, bila hata ya kuagalia tulikopa mwanzo kwa ajli ya nini na hicho tulichokopea kimekidhi malengo yaliyoandikwa? (maana kuna yaliyoandikwa na yaliyokusudiwa ambao hayya ya pili lni ya mioyoni tu, wala hayyasemagwi). Hivi wachumi wetu kumbe wanakazi gani? Bank kuu yetu ni ya kutunza kibubu tu?,.

Mkuu hiyo ndiyo picha unayoiulizia, undani wake ni huu na hii mifano michache katika mingi niliyoifunika.
 
Back
Top Bottom