Hivi CHADEMA bado wapo?

Hivi CHADEMA bado wapo?

Mmeanza kuisahau Chadema kwa kuianzishia thread....kwi! kwi! kwi!
Mbona unajichkesha unatatizo gani au unasoma shule za bweni make wanafunzi wa bweni ndiyo hasa wanayo haya matatizo ya kujichekeshachekesha.
 
Mwenyekiti na katibu wako hoi kabisa hawajui wafanye nini.

[h=3]Mbowe atoboa CCM ilivyohodhi wabunge 201 Bunge la Katiba[/h]
















Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimehodhi Bunge Maalum la Katiba kwa kuingiza makada wake 160 kati ya wajumbe 201 wa kuteuliwa na Rais.

Kadhalika, kambi hiyo imesema wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hawatarejea ndani ya Bunge la Katiba na wataendelea na harakati za kudai Katiba mpya nje ya Bunge.

Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe, akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2014/15, alisema Ukawa wataendelea na harakati zao za kudai Katiba mpya yenye kujibu haja, matakwa na matumaini ya Watanzania walio wengi nje ya Bunge Maalum kwa kuwa limetekwa nyara na CCM.

Alisema utafiti uliofanywa na kambi hiyo umebaini kuwa kati ya wajumbe 201, wajumbe 160 ni wanachama na viongozi wa CCM waliochomekwa kwenye Bunge hilo kwa kutumia kivuli cha waganga wa kienyeji, taasisi za kidini, asasi za kiraia, taasisi za kitaalamu, watu wenye malengo yanayofanana na hivyo kuweka msingi mbaya katika Bunge hilo.

"CCM iliendelea kufanya hila za kuchakachua kanuni za Bunge Maalum ili kupitisha hoja zao kirahisi na ziliposhindwa walitumia mabavu ya wazi kwa kulazimisha Mwenyekiti wake Taifa, Kikwete kutumia kivuli cha Urais kusisitiza msimamo wa CCM na kutisha wajumbe wa Bunge hilo kwamba wakipitisha muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume basi Jeshi la Wananchi litapindua serikali," alisema.

Mbowe alisema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni itaendeleza harakati nje ya Bunge Maalum zitakazowezesha kubadilishwa kwa muundo wa Muungano kwa kuivua Tanganyika koti la Muungano, kuipitia Zanzibar mamlaka kamili ndani ya Muungano na kujenga mahusiano ya hadhi na haki sawa baina ya Tanganyika na Zanzibar.

"Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kuweka wazi msimamo wake na wanachama wa Ukawa kwamba haitakuwa busara kuendelea na mjadala wa Bunge Maalum wenye lengo la kupitisha mapendekezo ya kundi la viongozi wa CCM, hatutashiriki Bunge lililojaa kauli za kibaguzi, kashfa, vijembe na matusi dhidi ya wajumbe wa Ukawa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba," alisema Mbowe.

Alisema Ukawa wamekataa kuwa sehemu ya Bunge Maalum lililojaa vitisho, kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana na kushinikizana na kwamba hawatarejea hadi dhima halisi ya Bunge hilo itakapopatiwa ufumbuzi.

Mbowe alisema kwa sasa Rasimu ya Katiba mpya imewekwa kando na wajumbe wa kundi la walio wengi kujivika jukumu lililokuwa la Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakidai kupokea maoni mbadala ya wananchi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa kiasi kikubwa wa haki ya wananchi ambao kwa ujumla wao walitoa maoni yao kwa Tume ya Katiba


MAPATO NA MATUMIZI
Mbowe alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, hadi kuahirishwa kwa Bunge hilo kiasi cha Sh. blioni 27 zilitumika na kwamba kwa ujumla mchakato mzima kwa kipindi cha miaka miwili umetumia kiasi cha Sh. bilioni 102 na kwamba kiasi hicho ni kikubwa katika nchi ambayo maendeleo na huduma za jamii zenye umuhimu mkubwa kwa ustawi wa wananchi zimekwama kwa kukosa fedha.

Alisema fedha kwa ajili ya Bunge Maalum zilitakiwa kuidhinishwa na ama sheria ya matumizi ya serikali iliyotungwa mahususi na Bunge au sheria iliyotungwa kwa mujibu wa ibara ya 140 ya Katiba inayohusu mfuko wa matumizi ya dharura unaoanzishwa kwa ajili ya mambo ya haraka.

Aidha, Mbowe alihoji na kuitaka serikali kutoa majibu ya bajeti ya matumizi ya Bunge Maalum ni kiasi gani na kwa ajili ya matumizi gani, kiasi kilichotumika hadi sasa na kwa matumizi gani, nani aliyejadili na kupitisha bajeti hiyo, sheria gani iliyotungwa na Bunge lipi iliyoidhinisha matumizi ya fedha hizo na kwa waraka gani Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliidhinisha matumizi hayo.

Aidha, alisema majibu ya maswali hayo ni muhimu ili kuepusha Taifa na balaa la ufisadi na wizi mkubwa wa fedha za umma kama ilivyotokea mwaka 2005 kwa mabilioni ya fedha yaliibwa kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (Epa) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya kugharimia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

KAULI ZA CCM KUHUSU SUK
Mbowe alisema CCM nje ya Bunge hilo wameendelea na kauli za uchochezi na kibaguzi zinazoweza kuvunja amani na kwamba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Zanzibar Jumapili iliyopita, baadhi yaviongozi wake walisema wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar iliyoundwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Alisema madhumuni ya mchakato huo ni kuvunja SUK ambayo iliamuriwa iwepo na kura ya maoni ya Wanzanzibari wote na imesaidia kuleta amani na utulivu Zanzibar.

KAULI ZA KIBAGUZI
Alisema kauli ya Makamu wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, katika mkutano wa CCM, alisema Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu, ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkogwe si raia wa Zanzibar ni kauli ya kibaguzi, kichochezi na yenye kupandikiza chuki dhidi ya watu wenye asili ya Kihindi.

"Ni kauli inayopaswa kulaaniwa na kila mpenda amani popote alipo," alisisitiza. Alisema viongozi wa serikali wanawajibika kukemea kauli hizo, lakini hawafanyi hivyo na badala yake kuonekana ama kuzitoa, kuzikoleza au kuzishabikia bila kutathmini nafasi na wajibu wao wa kuliunganisha Taifa.

UCHAGUZI MKUU/MITAA

Alisema iwapo Tanzania itakwenda katika uchaguzi mkuu bila Katiba mpya Taifa litaingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba ambao utakuwa rahisi kuzaa machafuko haswa kipindi cha uchaguzi.

Alisema Katiba inatumika sasa ina mapungufu mengi na haiwezi kuwa jawabu la uchaguzi ulio huru na wa haki katika mazingira ya sasa yanayojengwa na uzoefu wa chaguzi zilizopita chini ya mfumo wa vyama vingi na kwamba upo uwezekano wa chaguzi za serikali za mitaa kufanyika bila Katiba mpya kama ambavyo serikali imeshasema na kuanza maandalizi ya uchaguzi huo Oktoba mwaka huu.

Aidha, alisema Kambi hiyo inaishauri serikali kuweka utaratibu wa mpito kushughulikia masuala yote ya uchaguzi na kwamba Taifa haliwezi kuingia kwenye uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa kwa utaratibu uliopo sasa na uchaguzi mkuu mwakani.
 
Mwenyekiti na katibu wako hoi kabisa hawajui wafanye nini.

_MG_1089.JPG


photo+%281%29.JPG
 
Ndugu zanguni,

Kama ilivyotabiriwa, Chadema ndio inayeyuka kama barafu juani . Wengi tuliyajua haya lakini makamanda viroba wakabisha kwa matusi marefu marefu, lakini sasa nadhani nao wameanza kuamini kuwa chadema ni kama ngoma wa mdundiko tu, haieleweki inakwendfa wapi na sasa mwisho wa ngoma umefika wanajibanza kwa ukawa.

JITAMBUENI MBULUMUNDUS
IMG_9927.JPG

Hawapo wewe ndio upo kawatangazeeee.
 
CDM ndo mpago wa Mungu,hakuna kingine cha kuleta mabadiliko kwa watu bali cdm pia mawanzo yako ni mgando kweli,unaamini utabili wa mtu anauraia wa sehemu mbili mstuni na uraiani kama huna hoja lala
 
Kwani kuna muda maalum uliopangwa nchini wa vyama vya siasa kuona umuhimu wa kuungana!? Ni miaka mingapi!? TANU na Afro Shiraz Party ilivichukua miaka mingapi tangu vianzishwe mpaka vilipoona umuhimu wa kuungana mwaka 1977!? Wapi nilipoandika kwamba vyama hivyo vimeamua kuwa kitu kimoja!? Tofautisha kati ya kuunganisha nguvu na kuwa kitu kimoja, mbele ya safari kama vyama hivyo kupitia viongozi wake na wanachama wataona umuhimu wa kuvunja vyama vyao na kuunda chama kimoja basi hakuna ubaya wowote wa kufanya hivyo.

Mkuu BAK, CHADEMA ndio wamegundua leo kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu?
Lini vyama hivi vitatu vimepatana na kuwa kitu kimoja???
 
Chris Lukosi ana historia ya kufukuzwa kila anapokwenda toka zamani. Huyu kijana alikuwa askari polisi ndani ya jeshi letu la polisi Tanzania. Alifukuzwa ndani ya jeshi hilo kwa utovu wa nidhamu na wizi wa mali ya umma. Alikutwa anaiba mafuta (diesel) kwenye gari la dolia (kigofu cha polisi) kule Sumbawanga.

Huko aliko Uingereza alikuja juu kama moto wa kifuu katika kuanzisha na kueneza Chadema wakati yeye mwenyewe hakuwa na kadi ya uanachama. Chadema walimstukia na kuanza kumchunguza kulikoni?, kabla Chadema hawajapata jibu Mh Freeman Mbowe alitua Uingereza na Chris Lukosi akatumwa na lile kundi la mauaji ili amuwekee Mh Mbowe sumu. Chadema ni mpango wa Mungu hivyo waliweza kupata habari hizo mapema sana na Chris Lukosi hakuweza kumkaribia ama kukutana na Mh Mbowe. Chadema wakaona isiwe taabu kwanza jitu lenyewe halina hata kadi ya uanachama na wakaamua kumfukuza kama mbwa mwizi.

Kibaya zaidi aliwatukana sana CCM tena matusi ya nguoni. Aliwatukana viongozi wakubwa ndani na nje ya CCM ambao mpaka sasa wanamsubiri aingie 18 zao wamfyeke makende. Huyu kiumbe pamoja na kuwatusi Chadema kila leo, CCM hawawezi kumpatia uanachama hata kwa dawa.

Cha ajabu zaidi kiumbe huyu ana uraia wa Uingereza, kwanini anajisumbua na siasa za Tanzania?.
 
Frankly speak, Kiukweli kama ilivyokuwa kwa Tanganyika kufa natural death, hivyo hivyo kwa chama changu CHADEMA, tatizo ni uongozi wa juu kujiamlia mambo bila mpangilio, kujaza watu kwenye mikutano ya UKAWA isiwe sababu ya kujifariji kwani huu ni muungano usio stable kabisa(Show off), mnaosema ni muungano wa kwenye katiba mpya tu na nyie mmepotoka na kupotoshwa kwani tayari watu washaanza kujipanga kwa uchaguzi wa 2015.

Athari zake zitawafika hasa vijana wachanga kisiasa kwa kukosa fursa za uongozi sababu by nature UKAWA ITALAZIMU KUTUMIA WANASIASA WAZOEFU NA WAKONGWE KUTOKA CDM, CUF na NCCR hivyo hakutakuwa na dhana ya vijana kama nguvu ya mabadiliko.

ndio mpango mzima.
 
Frankly speak, Kiukweli kama ilivyokuwa kwa Tanganyika kufa natural death, hivyo hivyo kwa chama changu CHADEMA, tatizo ni uongozi wa juu kujiamlia mambo bila mpangilio, kujaza watu kwenye mikutano ya UKAWA isiwe sababu ya kujifariji kwani huu ni muungano usio stable kabisa(Show off), mnaosema ni muungano wa kwenye katiba mpya tu na nyie mmepotoka na kupotoshwa kwani tayari watu washaanza kujipanga kwa uchaguzi wa 2015.

Athari zake zitawafika hasa vijana wachanga kisiasa kwa kukosa fursa za uongozi sababu by nature UKAWA ITALAZIMU KUTUMIA WANASIASA WAZOEFU NA WAKONGWE KUTOKA CDM, CUF na NCCR hivyo hakutakuwa na dhana ya vijana kama nguvu ya mabadiliko.

ndio mpango mzima.
 
Mzee anagopa kuwagiwa radhi ya bintiye!!

attachment.php
 
Ndani ya CCM ni raha tupu - kweli kijana anafaidi

10416622_623296971111734_1237464970913797645_n.jpg
 
Kwani kuna muda maalum uliopangwa nchini wa vyama vya siasa kuona umuhimu wa kuungana!? Ni miaka mingapi!? TANU na Afro Shiraz Party ilivichukua miaka mingapi tangu vianzishwe mpaka vilipoona umuhimu wa kuungana mwaka 1977!? Wapi nilipoandika kwamba vyama hivyo vimeamua kuwa kitu kimoja!? Tofautisha kati ya kuunganisha nguvu na kuwa kitu kimoja, mbele ya safari kama vyama hivyo kupitia viongozi wake na wanachama wataona umuhimu wa kuvunja vyama vyao na kuunda chama kimoja basi hakuna ubaya wowote wa kufanya hivyo.

Wale usipoteze muda wako kuwapa maelezo,wakumbushie tu,Chama Tawala Malawi,baada ya kukosa Ikulu wengine wamejinyonga na Mwenyenchi akafuta matokeo,mwisho wake ameambulia AIBU.Hawa ni wakuaacha tu.
 
pole kama bado unafikiria kuna chama kiitwacho chadema. siku hizi hiyo ni saccos, na makao yake makuu yapo kule tengeru na ofisi ndogo pale ufipa-kinondoni.

Ndugu zanguni,

Kama ilivyotabiriwa, Chadema ndio inayeyuka kama barafu juani . Wengi tuliyajua haya lakini makamanda viroba wakabisha kwa matusi marefu marefu, lakini sasa nadhani nao wameanza kuamini kuwa chadema ni kama ngoma wa mdundiko tu, haieleweki inakwendfa wapi na sasa mwisho wa ngoma umefika wanajibanza kwa ukawa.

JITAMBUENI MBULUMUNDUS
IMG_9927.JPG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom