Hivi 2020 kuna Mtanzania ataichagua CCM?

labda wakibadilisha candidate, jambo ninalojua halitotokea.
 
Kama watanzania waliambiwa elimu BURE hadi chuo kikuu,wakakataa na wakachagua BURE hadi F iv halafu sasa wanalalamika lazima ujiulize kwamba kiakiri sisi watanzania tuko sawa?
 
watu hawawezi kuacha kuichagua ccm kwa sababu ya post yako hii ya kijinga! wataacha kuichagua ccm endapo tu utatokea upinzani wenye nia ya dhati ya kuondoa umaskini wa watanzania, Leo hii upinzani una wagombea ambao walikuwamo ccm miaka zaidi ya 30 na hakuna jipya!
Upinzani wa dhati upi mkuu wenye jeshi la polisi au
 
2005; 80%
2010; 62%
2015; 58%
2020; ??%
??% = what? Jaza mwenyewe. Na hiyo hesabu hapo juu ni pamoja na wizi wa kura, matumizi ya vyombo vya dola, udhibiti wa media na uchafu wote. Lakini graph ilikuwa inachuka kwa kasi sana.
Sasa hiyo ??% toa za ulaji wa rambi rambi, lugha ya matusi kwa wapiga kura, uchumi mbovu, vijana kushindwa kusoma kwa kukosa msaada wa mikopo, njaa na kunyimwa chakula kwa vile ukame haukuletwa na ccm na mazagazaga mengine.
Hakika hiyo ??% yaweza kuwa 35%. Na kama wizi ukidhibitiwa ni 29%. Tume huru ya uchaguzi ikifanikiwa kuwepo hapo ndio funga kazi maana hiyo ??% itakuwa 11.7% sawa na kura za Lipumba kipenzi chenu.
2020. 75%. Hamkumbuki Mkapa alipata 61% 1995 na 71% 2000?? Mmeshasahau??
 
Mkianzisha nyuzi muanze kutafakari kwanza kabla ya kuandika chochote. Kila nukta utakayoipitia ijadili kwa kina uandike. Hiv unadhani ndege zilinunuliwa ili hali hakuna dawa? Ajira zipi zilizozuiwa watu wasiajiriwe, kiongozi yupi aliefanyiwa kisasi? Mnyonge gani aliefanyiwa dhihaka! Tafakari kwanza usikurupuke kuninukuu halafu nitakuambia kimoja baada ya kingine utaelewa
Sasa mtu kama huyu utamuita ana akili timamu!?
Usishangae naye ni degree holder, sasa jiulize standard seven yupoje nchi hii!!!?
 
Kwa huku Kusini CCM 2020 itapita kwa asilimia 98 ..kwa walichowafanyia wakulima wa KOROSHO !
 
FB_IMG_1483627906216.jpg
 
Tumchague nani,Lowasa?hata kama utakuwa umenishikia smg kichwani bora nife na kalamu yangu mkononi kuliko kutiki kwenye kijedwari cha picha ya Lowas!!!!JPM kama angekuwa kwenye nchi ya watu wenye akili timamu wangekuwa wanafanya sherehe kila siku kushangilia kuwa na rais kama huyu,but cha kusikitisha ni kwamba ni rais wa nchi ya watu wenye akili ndogo kama za mleta mada.hivi unajua kwa mfano bei ya shangingi moja ni sh ngapi kiwandani?na bei tuliokuwa tukiuziwa ni sh ngapi?kuna jaribio limefanyika imetoka mil 300 kupitia taasisi a serikali zimeletwa shangingi tatu mpya wakati bei tuliyokuwa tunapigwa ni zaidi ya mil 250 kwa shangingi moja,huko hakukaliki watu wanakimbizana.ww hushangai inakuwaje hostel za udsm zilikuwa zijengwa kwa bilioni zaidi ya 90 lakini taasisi ya serikali ikajenga kwa bilioni 10?hata kama ni kodi na gharama zingine ndio iende mara 9?watanzania tumepigwa sehemu nyingi sana na kinachokera sana siku hizi wale tuliokuwa tunawategemea kukemea ufisadi ndio wamekuwa mawakala wakubwa sana wa kutetea ufisadi na mafisadi!!!!Watanzania tusikubali kamwe kutumika na hawa manyang'au kuwa watetezi wa ufisadi eti kisa pesa walizokuwa wakituibia ndio zilikuwa zinarahisisha mzunguko wa pesa huku mtaani.tumepata rais ambae anasema na watu wanakimbizana kutekeleza,ofisi za umma sasa hivi watu wanawajibika na njia za panya za kujitajirisha binafsi zinafungwa kwa kasi ya ajabu na ndio maana sasa hao wanaojiita wapinzani wanashindwa kuibua ufisadi badala yake ndio kama hivi wanageuka sauti yao ya kuwatetea.rais juzi huko kagera kaagiza ziondolewe kodi za ajabu ili kuboresha bei za mazao kuwanufaisha wakulima,hivi mkulima akilima pamba akapata soko la uhakika na bei nzuri atashindwa kumchagua HjPM by 2020?kumchagua ndio atakuwa hana akili?mkulima wa mtwara ambaye amenufaika na bei ya korosho akajenga nyumba,akaboresha maisha yake kumchagua JPM 2020 atakuwa hana akili?wale ambao watanufaika na kuongezeka kwa viwanda na sekta nyingine kuboreshwa by 2020 kumchagua JPM watakuwa hawana akili?embu acheni kutufanya wote wajinga,tunatambua kuwa mmeshahamia timu mafisadi tangu mumpokee babalao na kuwa sasa hivi nyie ni wasemaji wakuu wa timu hiyo so msituzingue!!!!FANYENI KAZI VIJANA ACHENI KULIALIA TU KAMA WATOTO WADOGO......kila mtu na afanye kazi uone kama maisha ni magumu kama mnavyofikiria,tatizo mmekariri maisha kuwa ni lazima uishi dar na si kwingineko...nendeni vijijini huko kunafursa kibao za kilimo na mambo mengine sio kukomaa mijini tu wakati mambo yamebana na hakuna kipya unachofanya.
 
Mimi itabidi niichague ili izidi kunbania wale jamaa wa buku 7 wa Lumumba, dili imekosa humu mtandaoni hawaonekani kwa kukosa data kwenye simu. Nasikia wana data za kuchat bure FB kulike sketi na make up za wanawake. Au nimekosea jamani
 
hivi lini waalichaguliwa hawa Zaidi ya kupachikwa na kitengo wananchi fungukeni mukitegemea miujiza mutaendeleaa kuwa na madikteta uchwara kila siku
 
Back
Top Bottom