Mwenyekiti wa Halmashauri Longido matatani, atakiwa kujiuzulu

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido, SIMON OITESOI ameingia kwenye mgogoro wa kiuongozi na kutakiwa kujiudhulu kufuatia kushindwa kusimamia mamlaka yake ipasavyo katika baraza la madiwani na kuruhusu upotevu wa mamilioni ya pesa za halmashauri hiyo kunakofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

Katika kikao kilichoketi cha baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo,mwenyekiti huyo alionekana kuwa busy na simu wakati kikao kikiendelea jambo linalotazamwa kama ni utovu wa nidhamu kwa mkuu wa wilaya hiyo MARCO NG'UMBI aliyekuwa akitoa maelekezo ya serikali.

Baadhi ya madiwani walidai kuwa ulegevu wa mwenyekiti huyo umelikosesha MENO baraza hilo kiasi cha kushindwa kuhoji matumizi mabaya ya fedha yanayosababishwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo.

Katika baraza hilo mkuu wa wilaya alilieleza baraza hilo la madiwani jinsi baraza hilo limeshindwa kusimamia mapato ya halmashauri huku fedha nyingi zikipotea bila kuwepo usimamizi .

Alisema makusanyo ya halmashauri hadi desemba mwaka jana yalifikia zaidi ya bilioni 1.036 lakini hadi sasa ni sh,milioni 90 pekee zimeenda kwenye maendeleo na hiyo ni chini ya asilimia 7 tu ambayo ni kinyume na utaratibu unaozitaka halmashauri kutoa asilimia 40 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

"Mlitakiwa angalau mmetoa sh,milioni 414 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Longido ,ukimya wako mpaka sasa unamaanisha nini kama wewe sio sehemu ya haya madudu yanayiendelea hapa"


Ndani ya kikao hicho mkuu hiyo wa wilaya hakupepesa macho pale alipoeleza wazi kuwa halmashauri hiyo imejaa upigaji.

Alisema kuwa fedha zinazotokana na mapato ya halmashauri zinapigwa kabla hazijaingia kwenye mfumo unaotakiwa kwa kutumia mashine za POS(fedha Mbichi).

4. Ajira nje ya utaratibu rasmi wa ajira. Kuna baadhi ya wakusanya ushuru ambao walichomekwa baada ya kamati ya ajira kumaliza kupendekeza majina ya walioshinda usaili lakini baada ya hapo ulitumia nafasi yako kushinikiza kuongezwa baadhi.

5. Hivi majuzi zilivuja taarifa kuwa wewe ni sehemu ya mkandarasi anayejenga hospitali ya wilaya aitwaye serico engineering co.Ltd. Lori lako lenye namba za usajili t 254 djr lenye rangi ya blue aina ya mitsubish, limepewa kazi ya kuchota na kuuza mchanga, kokoto, mawe na vifusi na kuuza katika hospitali ya wilaya. Hadi kufikia october mwaka jana, ulichota tripu 193 na hadi disemba ulishachota tripu 400.

Tatizo sio gari lako kuchota mchanga ama material nyingine, tatizo ni kwamba kwa sababu wewe ni kifutu cha longido usichogusika haulipi ushuru ambapo kwa tripu hizo 400 ni shilingi milioni 6 ambazo zinatakiwa kuingia halmashauri yako ambayo inakuhudumia kwa karibu kila kitu na wewe unaisimamia. Hapo bado zile ambazo zinatakiwa kwenda wizara ya madini maana material yote hiyo ni madini. Utaratibu wa maadili ya uongozi hauruhusu diwani yeyote kujiingiza katika tender yoyote kwa sababu italeta mgongano wa kimaslahi.

Leo wewe ndiye mtia saini mikataba yote ya wakandarasi lakini bahati mbaya sana wewe ndiye unaungana nao kula sahani inayokuhudumia na kukataa kwa makusudi kulipa kodi zinazotakiwa inyanyue halmashauri yako, tafsiri yake serico walipata tender hii baada ya kukaa na wewe kwenye vile vikao vyako vya chamber za dhambi ya hujuma juu ya watu wa longido, na halmashauri yetu pendwa. Maana yake unaihujumu kwa makusudi halmashauri yako unayoiongoza na inayokuhudumia na kuihujumu serikali yako ya ccm. Huu ni uhujumu uchumi wa wazi kabisa na hapa unastahili kushtakiwa na kufungwa kabisa.

Mwenyekiti wa CCM yuko kimya, katibu na mwenezi wameungana na wewe kwenye udhaifu huu. Nimeanza kuelewa kwa nini unapigana kuwaingiza viongozi wa ccm wanaokuunga mkono ili wakufichie madhaifu akiwemo mwenyekiti wa ccm ambaye hathubutu kutoa tamko kwa wilaya yake inayochezewa. Udhaifu, ulaji na uhujumu uchumi

6. Halmashauri yako ya upigaji ambayo inaongozwa na mkurugenzi mpigaji asiye na maamuzi na ambaye umemshika pua naye akashikika, mmeanzisha project ya kufyatua matofali ambayo jana dc amesema itengenezewe utaratibu mpya wa uendeshaji, imenunua gari ambalo linafanyiwa service na watu kutoka dar na ambao mnawagharamia nauli, malazi na perdiems na hela ya kufanyia gari service (maajabu ya musa). Mkurugenzi wako huyu aliwahi kununua mashine kama hiyo huko alikotoka monduli na haifanyi kazi. Kabla hamjanunua mashine hiyo, kwa nini hukujiridhisha kwanza kabla ya kununua? Au kwa sababu kulikuwa na asilimia kidogo kwa ajili yako? Tuambie wanalongido, nani alishauri mashine hiyo inunuliwe na kamati ipi ya uendeshaji ya halmashauri (cmt) au kamati ipi ya fedha baraza gani la madiwani lilipitisha bajeti ya manunuzi? Huoni hii ni sehemu ya dharau kwa baraza lako la madiwani ambalo nilishasema hapo awali kwamba ni kibogoyo? Udhaifu

7. Halmashauri yako ni kituo cha “vibarua”. Kwanza nasikitika unawaita watanzania wenzetu vibarua wakati wengine wana miaka 16 kwa maana ya tangu halmashauri kuanzishwa hadi leo na bado una sauti ya kuwaita vibarua. Kila mwezi zaidi ya shilingi milioni 9 na laki mbili na nusu hutumika kulipa hao unaowaita vibarua. Wafanya usafi ndani ya halmashauri wapo 10 ambapo jana mlielekezwa na dc mpunguze hadi wanne. Cha ajabu katika hili, pamoja na matumizi makubwa na ya “hovyo” kama dc alivyosema, bado watu hawa wanaidai halmashauri. Mfano; 2020 wanadai miezi 6, na tangu mwaka jana october hawajalipwa mpaka dakika hizi wakati kila mwezi mnafanya transactions za kuwalipa. Nini kinaendelea katika hili? Hizo pesa mnazotoa benki mnazipeleka wapi? Kuna taarifa zinaendelea chini ya maji na nitathibitisha wakati wowote kuanzia sasa ya kwamba cashier wa halmashauri, dt, mkuu wa idara ya utumishi wa halmashauri, mkurugenzi, wewe mwenyekiti wa halmashauri, cc wa baraza la madiwani ndio wapigaji wakubwa na ndio mnaosain kwa niaba ya wengi na mnakula pesa ambazo zimekuwa zikiombwa pale watu wanaposain kuwa wamekuja kwenye kikao halafu mnawaambia bado pesa hazijatoka na zikitoka tutawataarifu. Taarifa zinasema “hamjawahi” kuwapa taarifa za pesa zao kutoka na mmekuwa mkibwia hizo pesa with your fellow crooks. Katika hili, namuomba dc afuatilie na aombe forensic audit kwa halmashauri yetu hasa kwa hawa manyamera wenzako mnaoutia umaskini halmashauri yetu na kukaribisha hati chafu mlizozoea kila mwaka. Unafikiri hawa “vibarua” watoto wao wanakula mawe wakati wapo halmashauri full time maana mmewataka hivyo? Na hata wale ambao mmekuwa mkiwawekea mafao yao ya kustaafu mmesitisha kwa miaka kadhaa na hizo mkabwia kama kawaida yenu. Katika hili hutabaki salama. Utalaaniwa uingiapo na utokapo halmashauri, utalaaniwa nyumbani kwako na hata nje ya nyumba yako, utalaaniwa wakati wa joto na wakati wa baridi. Watalaaniwa wote waliokula pesa za watu hawa ambao hawana sauti na ukakataa kuwa sauti yao. Mifugo yako na wanao wakose amani mpaka watoto wa hawa vibarua wapate pesa zao walizovuja jasho. Ukose amani daima mpaka hizi pesa ulipe haraka iwezekanavyo.

8. Mwaka jana alikuja mkuu wa mkoa wa arusha john mongela. Akafanya ziara ambayo alitembelea maeneo kadhaa ndani ya wilaya ya longido. Ajabu na kusikitisha ni katika sehemu mbili. Moja, ni katika hospitali ya wilaya ya longido ambapo pesa zilikuja zaidi ya milioni 791 za kujenga majengo manne. Ajabu sio pesa kuja, ajabu ni pesa kuja tangu mwezi wa tatu halafu siku mkuu wa mkoa anakuja mwezi disemba ndio lori la mbao linafika eneo la hospitali. Cha ajabu mwenyekiti umekaa kimya as if hujui kinachoendelea ukafumba macho na masikio, kwa nini tusiseme umelambishwa kitu kama kawaida yako kulambalamba, nimekumbuka; kumbe ndio ulikopewa tender ya kuleta mchanga na vitu vingine ndio maana ulishonwa mdomo pamoja na rc kuuliza maswali lukuki mpaka akakataa kuendelea na ziara mpaka documents zikaletwa hapo hopitalini na bado huongei. Pili, ni pesa za ujenzi ya wodi huko kituo cha afya ketumbeine. Pesa hizi pia zilikuja mwezi wa tatu na rc alipofika ndio msingi unachimbwa. Maskini watu wa tarafa yetu hii hawana kituo cha afya kingine zaidi ya ketumbeine. Lakini ulivyojazwa roho ya ulaji, ukaendelea kukaa kimya huku wananchi wa ketumbeine wakiendelea kuteseka kwa kukosa sehemu ya kulaza wagonjwa na hela zao mmefanya magodoro huko halmashauri. Rais analeta hela longido halafu nyie mnakuja kukojolea halmashauri. Kituko cha mwaka ni kwamba; dt alipoulizwa na mkuu wa mkoa ya kwamba kiasi gani cha pesa kipo, akasema yeye amekuta milioni 219 kumaanisha wahuni mmeshapiga milioni 81 kwenye mambo yenu. Nani aliyewalaani longido? Simon nani aliyekuloga? Au unataka kuifanya longido kama unavyotufanya sisi lumbwa kwa kuonekana mungu mtu? Hakuna ugonjwa usio na dawa, hata ukimwi una kipoozeo chake. Dawa yako imefika na madudu yako yote nitayaanika na mengine nitawatumia wahusika moja kwa moja.

9. Ofisi ya mwenyekiti wa halmashauri ndio ofisi yenye gharama kubwa ndani ya halmashauri ya longido. Nini kinachofanya uwe na gharama zaidi hata ya mkurugenzi ambaye anaitwa kila kukicha dodoma kwenye majukumu ya kitaifa? Gharama hizi ni za kweli ama za kubumba? Bado natafakari hili

10. Mahindi ya bei nafuu.Mwenyekiti wa halmashauri ,jicho la wanalongido ndani ya halmashauri bila uoga ,bila aibu ,bila hiana ,bila huruma umekuwa ukinunua mahindi ya msaada longido ,wewe na baadhi ya madiwani na kwenda kuuza kwa bei ya soko (hiked price) kwa watu wako ambao wangetegemea katika kipindi hiki kigumu cha kiangazi kilichofululiza kupata unafuu wa bei kama ambavyo serikali imewahurumia .Umejineemesha sana katika hili lakini laana hii haitakuacha salama.

11. Rushwa zisizomidhilika.Umekuwa ukitumia matatizo ya watu kama faida kwako mfano.Mgogoro wa vijana na wakazi wa kata yako badala uwasaidie ukadai rushwa kwa jina la jeshi la polisi ,hata hivyo nashangaa mpaka sasa umeachwa,baadhi ya wakuu wa idara kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kamati yako ya uongozi, mipango na fedha baadae kupitia mlango wa nyuma umewaomba rushwa ili uishawishi kamati irejelee na kubadilisha maamuzi ya kuwasimamisha katika nafasi zao, kama uongo simama ubishe, umekuwa ukiomba fedha mbichi kutoka kwa wakusanya ushuru, mfano mkusanya ushuru aliyekuwa nakusanyia chanzo cha utalii oldoinyolengai, geti la polisi longido . Na cha ajabu vyombo vyetu vya serikali zimekuacha uko huru hadi sasa.

12. Kubugia fedha za vikao. Wewe na mkuu wa idara ya utumishi,cashier, cc mmekuwa mkila fedha za baadhi ya wajumbe wa vikao na haswa watumishi wakuu wa idara na watumishi wengine wanaohudhuria vikao na kufoji saini zao kana kwamba wamesaini kupokea fedha zao. Cha ajabu bado laana hii haijawapata ila itawapata very soon.

13. Kutofanya malipo halali kwa watumishi wanapotumwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuisaidia halmashauri. Halmashauri yako imekuwa ni saccoss ya watu wachache na kuwatenga, kuwaonea wengine. Watumishi karibu wote isipokuwa mkurugenzi, mweka hazina wa halmashauri, mkuu wa idara ya utumishi, afisa biashara aitwae ray, cashier wa halmashauri, wengine wote wanalalamika kwa ukweli wakitumwa kwa mfano safari yeyote hawalipwi, wakienda kwenye operesheni ya mapato hawalipwi.

14. Kila kitu cha halmashauri yako ni dharura safari dharura, ununuzi wa mafuta kwa ajili ya idara mbalimbali dharura, hata ununuzi wa shajala za ofisi dharura kila kitu dharura kwa sababu fedha huliwa na watu wachache tu.

Naomba niishie hapa ila siyo kwamba madudu yako yamekwisha ,kwa kusema yafuatayo;

i; Mheshimiwa DC apate kujua kuwa mmeanza kumfitini kwa kutengeneza genge la upigaji against mtu wa mungu anayeiokoa longido, hamtafanikiwa katika hili.

ii; Mmeshaanza kusema DC amekuja na nguvu ya soda, utajua hujui. Huyu ni malaika kaja kutusaidia maana wazawa mmekuwa zaidi ya fisi. Mradi ukija mnawahi kusema mtapata nini kutoka kwenye mradi badala ya namna ya kufaidisha longido.

Kwa mara ya kwanza mmempata mwenyekiti kibogoyo kuliko kibogoyo mwenyewe. Mtajua hamjui. Muda wenu waja

*NOTE: WANALONGIDO MUAMKE KULINDA HILMASHAURI YENU. LEO NIMEONA NIANDIKE KWA ERUFI KUBWA ANGALAU IWAVUTIE KUSOMA.
View attachment 2528408
 
Back
Top Bottom