History in the making: NASA’s Juno spacecraft arrives at Jupiter!

History in the making: NASA’s Juno spacecraft arrives at Jupiter!

Haiwezi kurudi duniani, satellite zote zikifa zinapotelea huku na kuchafua space. Ila kwa hii, baada ya miezi 18 itaacha orbit na kuingia kwenye uso wa Jupiter huku ikipiga picha za mwisho za Jupiter surface. Mwisho itakufa huko kwa radiations za Jupiter na story yake itaishia hapo.
Lengo kubwa la NASA kupeleka Juno ni kujua chanzo cha sayari na ulimwengu(the origin of planet). How???
Jupiter ndo sayari kubwa katika solar system. Tukilinganisha na dunia, ukubwa wa Jupiter ni sawa na dunia 1000 combined. Ukubwa wa Jupiter ni mara 2 ya ukubwa wa sayari nyingine zote kwenye solar system zukiunganishwa kwa pamoja. Kutokana na fact hii NASA wanaamini kuwa sayari nyingine zimetokana na kugawanyika kwa Jupiter, so wakabuni JUNO na kuilauch kwenda Jupiter ili kuexplore Uso wa Jupiter. Hatimae imefika jana kwenye position(orbit) ya jupiter waliyokusudia.let us wait and see
 
mkuu hapa hakuna Mafanikio yeyote kwa Dunia Bali ni Uharibifu kwa Dunia.

Hawa wana sayansi ndiyo chanzo cha uaribifu, kila kukicha wana Mchokonoa Mungu.

Wewe unajua ni Athari gani zinaweza kutokea pindi makosa yanapotokea kwa wao kurusha vyombo hivyo kwenye sayari?

Embu tujiulize mabadiliko ya tabia nchi na ali ya hewa yanatokana na nini?

Magonjwa mbali mbali kwa wanadam, ambayo haya kuwepo yanatokana na nini?

Wanadamu watajiangamiza wenyewe kwa kujifanya wanajua maarifa kuliko Mungu.

Asikiaye na Afahamu.
Nasikia kuna wengine walitaka kujua mungu anakaa wapi mpaka leo hawajarudisha majibu na haijulikani ni wazima au wamekufa
 
Lengo kubwa la NASA kupeleka Juno ni kujua chanzo cha sayari na ulimwengu(the origin of planet). How???
Jupiter ndo sayari kubwa katika solar system. Tukilinganisha na dunia, ukubwa wa Jupiter ni sawa na dunia 1000 combined. Ukubwa wa Jupiter ni mara 2 ya ukubwa wa sayari nyingine zote kwenye solar system zukiunganishwa kwa pamoja. Kutokana na fact hii NASA wanaamini kuwa sayari nyingine zimetokana na kugawanyika kwa Jupiter, so wakabuni JUNO na kuilauch kwenda Jupiter ili kuexplore Uso wa Jupiter. Hatimae imefika jana kwenye position(orbit) ya jupiter waliyokusudia.let us wait and see
Kwani chanzo cha dunia hatukijui si mungu mwenyewe au wanasayansi hawaamini juu ya mungu
 
nani Amesema Mungu Anaishi Kwenye Jupiter?

Ni Sawa kabisa Mungu Anaishi Ndani ya Moyo wa Mwanadamu.

Ila yeye aliye zitengeneza sayari hizo ni Yeye na Yeye siyo mjinga.

Ila kazi ya Mwanadamu siku zote ni Uharibifu, na mchango wangu ni kwamba Je! Wanadamu wanaathirika kiasi Gani kwa kuaribifu utakaojitokeza kwa makosa ya wanasayansi hawa?
Siyo tunachekelea uangamivu bila kuangalia Athari zake.

Nimeshambuliwa kwa matusi ila kabla ya kutukana ni vyema kujikita kwenye Mada husika tusiwe wajinga wa kushangilia kila jambo bila kupima Athari zake.
Hebu Tuambie Athari za JUNO kwa Dunia ... maana Ipo mamillioni ya kilometer kutoka wewe unapotype
 
Kuna mafanikio gani wao kurusha hicho chombo kwenda huko Jupiter? Kwenda wakigundua kunafaa watu kuishi ndio wataenda huko?? Kama safari ya kwenda huko ni miaka mitano, it means ukitaka kuishi huko kwenda na kurudi duniani kuona ndugu zako itawachukua miaka 10 pekee kwaajili ya safari.. Hakuna chochote cha maana bora hizo sayansi zao wanazotudanganya nazo watengeneze dawa ya kutibu Ukimwi na Zika..

Wamarekani ni waongo sana.. Na si ajabu hata huko Jupiter hawajaenda ni kutafuta misifa tu..
Ila Kama Imechukua Miaka Mitano kuna Namna Watafanya Itachukua Siku Mbili.... Zamani Ulikuwa Unapanda Treni Unafika Dar Baada ya Siku Mbili now Unatumia Ndege Unafika ndani ya saa.. na Kitu
 
Ile Setilaiti ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupiter imefika kwenye sayari hiyo na kuanza kuizunguka.Wanasayansi wanakadiria setilaiti hiyo ilifika majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za Afrika Mashariki.Setilaiti hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi ilivyoumbwa.Mawasiliano kutoka kwa chombo hicho cha juu yalipokelewa katika maabara ya Nasa eneo la Pasadena, California kwa shangwe."Vituo vyote vya Juno, tunapokea sauti ya kufanikiwa kwa chombo Delta B," kituo cha udhibiti wa Juno kilitangaza. "Roger Juno, karibu Jupiter."Image copyrightGETTYImage captionChombo cha Juno kikipaaWanasayansi wanatarajiwa kutumia chombo hicho kufahamu Zaidi muundo wa sayari ya Jupiter ambayo hujulikana kwa Kiswahili kama Zohali.Wanafikiri muundo wake kikemia unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi sayari hiyo iliundwa miaka bilioni nne unusu iliyopita.Hakuna chombo cha anga za juu kilichowahi kufika karibu sana na sayari hiyo kama kilivyofanya chombo cha Juno.Miali nururishi kutoka kwa sayari hiyo huwa na uwezo wa kuharibu vyombo vya kielektroniki visivyokingwa vyema.Chombo vya Juno kimezingirwa na kinga ya madini ya Titanium.Kwa sasa Juno itakuwa ikichukua siku 53 kuizunguka sayari hiyo.Baadaye Oktoba, itaongeza kasi na kuikaribia zaidi sayari hiyo na kuanza kutumia siku 14 kumaliza mzunguko.Image copyrightGETTYLengo kuu litakuwa kubaini iwapo kuna oksijeni katika sayari hiyo. Hii sana itakuwa imefungamanishwa na maji, iwapo yapo."Kiwango cha maji katika sayari ya Jupiter kitatueleza mengi kuhusu ni wapo sayari hiyo ilikuwa ilipoundwa mapema katika mfumo wa jua,” anasema mmoja wa wanasayansi wanaohusika katika mradi huo Candy Hansen."Tunafikiri kwamba Jupiter iliundwa ikiwa pahala tofauti na ilipo sasa."Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidiSayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.
Source:bbc

Kumbe Wanajua Imeumbwa
 
Kwani chanzo cha dunia hatukijui si mungu mwenyewe au wanasayansi hawaamini juu ya mungu
Sayansi huwa inahitaji uthibitisho kwa observations na majaribio na ishu za kisayansi huwa zipo dynamic, sasa kwa kusema chanzo ni mungu inahitaji uthibitisho wa kufanyiwa hizo observations na experiments kwa mtindo huu unaanza vipi kuchanganya ishu za imani na sayansi. Swala si wanasayansi kuamini ama kutokuamini ishu ni sayansi zenyewe zile hatua zake mpaka ikubaliane na statement ama phenomena flani ni kweli. Ndio maana kwenye sayansi Leo tunaambiwa Pluto sio sayari lakini kesho usishangae pia ukaambiwa ni sayari sasa kwenye dini zetu tupo tayari kubadili maandiko pindi observations na experiments zimeenda kinyume na kile ambacho kimeendikwa, na hizo procedure za sayansi zikishindwa kumthibiti mungu?, itakuwaje?. Swala la mungu ni ishu ambazo zinabaki kuwa za kiimani zaidi.
 
Mungu ametupa akili tuzitumie sio kila jambo unaloliona unaliacha na kusema Mungu ndo anayejua kama ingekuwa hivyo hata malaria tungemuachia Mungu.Na Mungu anasema ktk maandiko yake watu wangu wanaagamia kwa kukosa maarifa
 
Noma yani kwa sekunde moja kinatembea kilomita 74...hii ni spidi kubwa hatari

Inahitajika friction na oxygen mlipuko kutokea. Ukishavuka stratosphere hakuna oxygen na hivyo hakuna mlipuko kwa speed hiyo maana ni nje ya stratosphere
 
Inahitajika friction na oxygen mlipuko kutokea. Ukishavuka stratosphere hakuna oxygen na hivyo hakuna mlipuko kwa speed hiyo maana ni nje ya stratosphere
Na je hicho chombo kinaendeshwa na fuel ?..kama ndio ni ipi ?..mafuta au hewa ?,nmesoma hapo kina uzito wa tani 1.6 nimeshindwa kuelewa safari ya miaka 4,hakijazimika tu ? na mafut ahayajaisha tu ?
 
Back
Top Bottom