History in the making: NASA’s Juno spacecraft arrives at Jupiter!

Faida za Juno Mission ni pamoja na uchunguzi wa mfumo mzima wa jua (zikiwemo sayari) jinsi hapo awali zilivyoundwa na kupata taarifa kwa jinsi mfumo ulivyo sasa na utakapokua hapo baadae. Sababu ya kufanya uchunguzi kwa sayari ya Jupiter ni kwa kua ni sayari kubwa kuliko zote hvyo inaaminika itakua na taarifa nyingi za "Mfumo wa Jua" kuliko sayari nyingine.
Hivi wewe unayefikiria mahitaji yako ya hapa niliko na ya sasa hivi, jiulize hili: Isaac Newton na wenzake walikuwa na mawazo sampuli hiyo walipovumbua mifumo mbali mbali ya kisayansi/kiufundi?
Ukisoma pole pole hapa, utakuta wengi wana hizo mihemko ya kudunisha hii habari muhimu kwa binadamu wote(haijawahi fanyika), huku wakifoka na kutokwa.

Science marches on. Upende usipende.
 
Na sisi tunajivunia kua na mabasi ya mwendo kasi, haya ni mafanikio pia

haaa kweli kabisa mkuu, mafanikio yanatofautiana, mwingine akinunu baiskeli ameona kafanikiwa, mwingine akijenga nyumba anaona kafanikiwa, wao wamepeleka chombo sayar ya mbali, sisi tunajivunia kuwa mabasi ya mwendo kasi
 
Tukisema wenzetu walipewa akili watu watabisha wakati hapa kwetu mambo madogo kama uchaguzi tu watu wanakwiba kura je kuvumbua vitu si hadithi
 
mkuu hapa hakuna Mafanikio yeyote kwa Dunia Bali ni Uharibifu kwa Dunia.

Hawa wana sayansi ndiyo chanzo cha uaribifu, kila kukicha wana Mchokonoa Mungu.

Wewe unajua ni Athari gani zinaweza kutokea pindi makosa yanapotokea kwa wao kurusha vyombo hivyo kwenye sayari?

Embu tujiulize mabadiliko ya tabia nchi na ali ya hewa yanatokana na nini?

Magonjwa mbali mbali kwa wanadam, ambayo haya kuwepo yanatokana na nini?

Wanadamu watajiangamiza wenyewe kwa kujifanya wanajua maarifa kuliko Mungu.

Asikiaye na Afahamu.

Unawaponda wanasayansi huku unabofya keyboard as if imetengenezwa kwa ramli!
 
Ile Setilaiti ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupiter imefika kwenye sayari hiyo na kuanza kuizunguka.Wanasayansi wanakadiria setilaiti hiyo ilifika majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za Afrika Mashariki.Setilaiti hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi ilivyoumbwa.Mawasiliano kutoka kwa chombo hicho cha juu yalipokelewa katika maabara ya Nasa eneo la Pasadena, California kwa shangwe."Vituo vyote vya Juno, tunapokea sauti ya kufanikiwa kwa chombo Delta B," kituo cha udhibiti wa Juno kilitangaza. "Roger Juno, karibu Jupiter."Image copyrightGETTYImage captionChombo cha Juno kikipaaWanasayansi wanatarajiwa kutumia chombo hicho kufahamu Zaidi muundo wa sayari ya Jupiter ambayo hujulikana kwa Kiswahili kama Zohali.Wanafikiri muundo wake kikemia unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi sayari hiyo iliundwa miaka bilioni nne unusu iliyopita.Hakuna chombo cha anga za juu kilichowahi kufika karibu sana na sayari hiyo kama kilivyofanya chombo cha Juno.Miali nururishi kutoka kwa sayari hiyo huwa na uwezo wa kuharibu vyombo vya kielektroniki visivyokingwa vyema.Chombo vya Juno kimezingirwa na kinga ya madini ya Titanium.Kwa sasa Juno itakuwa ikichukua siku 53 kuizunguka sayari hiyo.Baadaye Oktoba, itaongeza kasi na kuikaribia zaidi sayari hiyo na kuanza kutumia siku 14 kumaliza mzunguko.Image copyrightGETTYLengo kuu litakuwa kubaini iwapo kuna oksijeni katika sayari hiyo. Hii sana itakuwa imefungamanishwa na maji, iwapo yapo."Kiwango cha maji katika sayari ya Jupiter kitatueleza mengi kuhusu ni wapo sayari hiyo ilikuwa ilipoundwa mapema katika mfumo wa jua,” anasema mmoja wa wanasayansi wanaohusika katika mradi huo Candy Hansen."Tunafikiri kwamba Jupiter iliundwa ikiwa pahala tofauti na ilipo sasa."Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidiSayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.
Source:bbc
 
Jupiter size (1000 x earth) ,wow this is just crazy,ok flight time from NY to Australia by commercial airliner is like 24 hrs so this means at 1000 x bigger than our planet a trip within Jupiter cities can take 3 yrs ? hii Jupiter is no joke na tuna mengi ya kujifunza lazima kuna siri nyingi sana kwenye hizi planets
 
Kuna mafanikio gani wao kurusha hicho chombo kwenda huko Jupiter? Kwenda wakigundua kunafaa watu kuishi ndio wataenda huko?? Kama safari ya kwenda huko ni miaka mitano, it means ukitaka kuishi huko kwenda na kurudi duniani kuona ndugu zako itawachukua miaka 10 pekee kwaajili ya safari.. Hakuna chochote cha maana bora hizo sayansi zao wanazotudanganya nazo watengeneze dawa ya kutibu Ukimwi na Zika..

Wamarekani ni waongo sana.. Na si ajabu hata huko Jupiter hawajaenda ni kutafuta misifa tu..
Lazima useme hvyo maana huamini kama inawezekana af wenzako wanafanya hvyo ili kuinua upana wa akili zao kama wewe unavyofanya juhudi za kujua njia mpya za ufisadi
 
Lazima useme hvyo maana huamini kama inawezekana af wenzako wanafanya hvyo ili kuinua upana wa akili zao kama wewe unavyofanya juhudi za kujua njia mpya za ufisadi

...alafu haimjii akilini kuwa kama watafanikiwa kuichunguza jupiter na ku-comfirm bila doubt kabisa kwamba ni habitable, basi na akili za ku-invent chombo chenye chenye spidi zaidi itakuwepo tayari
 
Back
Top Bottom