Memorial Post: Julai 20, 2012 Mitandaoya Kijamii iliibuka na Historia ya jina la Mwigulu Nchemba.
Akiwa anasoma shule ya msingi Makunda kata ya Kyengege tarafa ya Kinampanda wilaya ya Iramba mkoa wa Singida, Mh Lameck Mkumbo Madelu alifeli mtihani wa taifa darasa la saba, baada ya kufeli huko akawa anatafuta njia ya kurudia.
Kwa bahati nzuri kulikuwa na darasa la kata la kata ya Kyengege lililokuwa linajumuisha shule za Makunda, Mgundu na Kyengege yenyewe. Kutokana na kuwepo darasa hilo la kata ikawa kuna nafasi kwani mwanafunzi Mwigulu Nchemba (msukuma) alikuwa ameacha shule akiwa darasa la sita kwani mwinuko wa kielimu kwa wasukuma ulikuwa chini sana wakati huo. Ndipo Mwl Malumbi alipoweza kumuuzia jina la Mwigulu Nchemba bwana Lameck Mkumbo Madelu.
Baada ya kurudia masomo bwana Lameck alifaulu kwa kutumia jina la Mwigulu Nchemba lakini baadae akiwa Secondari aliliongeza likawa Mwigulu Lameck Nchemba
Source: Admission books
1. Makunda Primary School
2. Darasa la kata Kyengege
3. Ilboru secondary
4. Wakazi wa Makunda