Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Mdharuba unatuangusha kaka,,daah!!
 
Dah...huu utumwa sasa...maana simulizi mtu inakunogea weeeee kila wakati unachungulia km imeendelea.
 
RIWAYA: HISTORIA BATILI [Fake History]
Na..
Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255718274130
+255654727266

EPISODE O23
2⃣3⃣
★★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA......
“Kunikera kwangu ni kutofuata ninachokushauri, nimekusamehe moja kwa moja kwa kumuua kipenzi cha mdogo wangu nimpendaye.. Lakini siku zijazo sitakusamehe kwa lolote, hivyo naomba twende sawa kutokea sasa” Mzee J4 alionekana kubadilika ghafla, Khatib alikua kwenye wakati mgumu sana ambao hakuwahi kutegemea.

SASA ENDELEA...
Pamoja na wakati mgumu alioupata hapa, Khatib alijitutumua na kuanza 'kumkata kucha na meno' Mzee J4.
“Mzee wangu nakuahidi sitoenda kinyume kabisa, niko pamoja nawe, nakusikiliza, nakuheshimu, niko tayari kufanya lolote kwa ajili yako, niko tayari kukutumikia, na nakuahidi kuwa siwezi tena kufanya jambo kama hili” .
“Sawa, kuwa makini sana kijana, wewe bado kijana mdogo, dunia inakuhitajia kwa mambo mengi mno ndugu yangu” Mzee J4 alionekana kuongea na Khatib kwa kutumia busara ya hali ya juu sana, alitaka asieleweke vibaya mbele ya Khatib, ingawa alikua na lake moyoni. Anachokifanya Mzee J4 ni kuhakikisha anajenga uaminifu wa hali ya juu kwa Khatib, ili baadae apate mtelezo, mambo yake yapate kwenda kama anavyotaka. Pia alitegemea ulinzi kutoka kwa Khatib, kwani alijua kwa kuwa karibu naye na kumuonyesha jinsi gani anajua habari zake, ingesaidia sana kumuweka Khatib katika himaya yake na baadae kumuamrisha kufanya chochote akitakacho. Kwa ujumla Mzee J4 hakukubaliana hata kidogo na kitendo cha Khatib kumuua Sauda, ilimuuma, ingawa alikua akijua mpango ule wa siri wa Khatib kutaka kumuua mkewe, na alikua na uwezo wa kuzuia, lakini aliamua kuacha lile jambo litokee, maana aliona upo muda ambao atakuja kuidhihirishia dunia kuwa watu wengine ni tofauti na wanavyoonekana kwenye macho ya watu. Mtu anayeonekana mwema, anatoa misaada kwenye jamii, anapendwa sana na pengine watu wakampendekeza agombee hata nafasi za udiwani na ubunge katika sehemu zao, kumbe anaweza kuwa ni muuaji na anayejali zaidi maslahi yake kuliko kitu kingine chochote. Inahitaji watu wenye jicho la tatu kama kina Mzee J4 kuwatambua watu kama hawa katika jamii.
*******************************
Baada ya kufukuzwa nchini Afrika Kusini, ambapo aliishi miaka ishirini na moja akitafuta maisha, Mzee J4 alirudi nyumbani na kuendelea kuishi na rafiki yake wa kijini. Jini huyu aina ya Subihani aliyemtambua kwa jina la SAYYEED, alikuwa akimtumia kwa kazi tofauti safari hii ukilinganisha na kazi alizokua akizifanya miaka kumi iliyopita. Kazi yake ya sasa ilikua ni ya kumkusanyia taarifa kuhusu watu wote wanaomzunguka na yeyote ambaye atahitaji kujua habari zake. Mzee J4 aliamua kufanya hili ili aendelee kujiweka salama baada ya maisha yake kuvurugika mara tu alipofukuzwa nchini Afrika Kusini ambapo kwa kipindi cha miaka kumi ya mwishoni alikua akiishi kama Mchungaji. Kwa kipindi hicho alikuwa akiaminiwa sana kama Mchungaji ambaye watu wengi walipitia kwake kwa maombi na kufanikiwa. Kazi kubwa ya Sayyeed kipindi hiki ilikua ni kuhakikisha watu wanashawishika kumfuata mchungaji yule wa uongo huku akitumia uwezo wake wa kijini kuwaponya na kutenda miujiza kwa kila ajaye hapo kupata huduma. Baada ya miaka miwili tu Mzee J4 alikua mchungaji maarufu kuliko mchungaji yeyote nchini Afrika Kusini. Alitengeneza pesa nyingi sana.. Akawa anamiliki kanisa kubwa mno. Kwa kipindi hiki alifahamika kama Mchungaji Daniel Mwanachia, akiachilia mbali dini yake na kulifuta kabisa jina lake la kiislam Jumanne Selemani. Alifanya hivi baada ya kupokea ushauri huu kutoka kwa rafiki yake huyu wa kijini ambaye alikabidhiwa na rafiki yake kipenzi aliyempokea Afrika Kusini kabla ya kufariki. Urafiki wa jini aliokua nao kwa rafiki yake Mzee J4, aliuhamishia kwa Mzee J4 mwenyewe na kuonekana kushamiri zaidi kwani Mzee J4 alikua akimuheshimu sana jini huyu. Wakafanikiwa kuanzisha huduma zao za kichungaji huku nguvu za kijini zikiwa zinatumika katika kila hatua mpaka wakafikia mafanikio hayo makubwa.
Mzee J4 alianza kupata ushindani na kupigwa vita sana na wachungaji wazawa wa Afrika Kusini na kujikuta anaanza kupoteza uhakika wa maisha yake ya mbele huku Sayyeed akimsaidia sana kumkwepesha na mitego mbalimbali ya kifo. Mpaka pale ambapo hali ilikua mbaya zaidi na Sayyeed akamshauri Mzee J4 aondoke Afrika Kusini kwani aliona hakukuwa na mwisho mzuri, hivyo basi kabla mambo hayajavurugika aondoke mapema pale nchini ili aweze kuambulia walau mtaji tu wa kwenda kuanzia huko Tanzania. Mchungaji Daniel Mwanachia (Mzee J4) alikataa ushauri huu wa Jini Sayyeed na akahisi labda jini huyo ameshawishiwa na moja ya maadui zake ili amuondoe yeye. Ndivyo ilivyo!! Binadamu ni wagumu kukubali ushauri hata wa marafiki zetu tunaowaamini pale tu tunapoona ushauri utatuweka mbali na maslahi yetu. Na haya yalimkuta Mzee J4, kwani Sayyeed hakuendelea kumsisitiza bali aliendelea kumlinda na kuhakikisha Mzee J4 yupo salama mpaka hapo atakaposhuhudia mwenyewe yaliyokua mbele yake.
Ingawa alishahudumu kwa miaka kumi na alishakuwa na wafuasi wengi nchini kote, Mchungaji Daniel Mwanachia alifukuzwa nchini Afrika Kusini ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali zote alizokuwa nazo. Akarudi nyumbani na silaha moja tu-SAYYEED.
************************
“Utashangaa sana kwanini najua kila kitu kuhusu wewe, ila usiwe na wasiwasi, haya ni mambo ya kawaida tu.. Waswahili wenyewe wanaita uwezo wa jicho la tatu” Mzee J4 aliamua kumtoa wasiwasi Khatib baada ya kumuona jinsi alivyokuwa mnyonge mpaka kufikia kutamka maneno yale ya udhaifu na kunyenyekea kwake pamoja na pesa nyingi alizokuwa nazo.
“Sawa Mzee nakuelewa, nahisi pia hiyo elimu yako inaweza kuwa na mchango katika haya maisha yangu ya kila siku” Khatib alijitutumua akiamini siku moja pesa yake inaweza kumueka chini Mzee J4 na kuwa mtumishi wake anayemlipa!! Hakujua kuwa alikua anaota mchana tena kiwandani.
“Mimi nataka uwe binaadamu bora na mfano wa kuigwa katika ulimwengu huu” Mzee J4 'alikazia 'point'.
Wakajadili na mambo mengine ya kidunia kwa muda mchache kabla ya Mr Khatib kuwasha gari yake na kuanza safari.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Ila mi nakupenda sana Walter, nakuahidi sitakusaliti, wewe ni wa kwanza na wa mwisho kwangu” Sarah, alikuwa ameegesha kichwa chake kifuani mwa Walter Mbwambo akiongea maneno haya baada ya kupata 'break fupi' katika kazi ile ya usiku inayochosha mwili pamoja na akili.
Sarah alikutana na Walter chuoni, wote wakiwa wanasoma Bachelor of Commerce. Walter alikua akitokea katika familia ya kimasikini ya Mzee Mbwambo pale mkoani Kilimanjaro. Kutokana na juhudi zake katika masomo na kipaji alichopewa na Mungu, Walter alifanikiwa kupata 'Schorlaship' ya kwenda kusoma Degree yake ya kwanza nchini humo baada ya kushika nafasi ya tatu kitaifa katika mtihani wake wa kidato cha sita. Kutokana na maisha ya kawaida sana aliyokuwa anaishi Walter, uchangamfu wake, na hata jinsi alivyo makini kufanya kile kilichomleta pale chuoni, Sarah alijikuta yeye ndiye anayemwambia Walter kuwa amevutiwa naye, kinyume na tamaduni zetu za kiafrika tukiamini kuwa mwanamke kumtamkia mwanaume kuwa anampenda ni kama kujitusi. Walter hakupinga wazo hili ingawa pia hakukubali kirahisi. Wakakubaliana kuwa wawe wapenzi lakini 'Elimu kwanza'. Hivyo walishirikiana sana kwenye masomo huku wakiwa na malengo ya kuwa mke na mume hapo baadae licha ya tofauti ya dini iliyokuwa kati yao.
Walter alikua amepangiwa 'Apartment' ikiwa ni moja ya 'benefits' za schorlaship aliyopata. Hivyo basi, Sarah alikua akitumia nafasi hii ya Walter kuwa peke yake na kuja 'kukita ago' hapa kwa siku kadhaa huku ratiba yao ya chuo ikiendelea kama kawaida.
“Nipo kwa ajili yako, na ondoa shaka MyLove” Walter alimtoa wasiwasi Sarah ambaye alionekana kuhofia sana juu ya Walter wake haswa akiangalia jinsi wasichana wengi haswa wale waliokuwa wakitokea Afrika Mashariki walivyokuwa wakivutiwa naye mtoto yule wa kipare ambaye alimudu kuongea kiswahili fasaha sana ambacho kiliwapa watu wengi wakati mgumu kugundua kuwa alikuwa mpare wa Mwanga pale mkoani Kilimanjaro.
“Kuna swali muhimu sana ambalo sijawahi kukuuliza MyLove, ingawa usishangae ninavyokuuliza sasa wakati tumeshakata miaka miwili na nusu hapa chuoni” Walter alimueka 'attention' Sarah kwa kutaka kumuuliza kitu kuhusu yeye.
“Go on swerie.. Just ask” Sarah alijibu kwa kujiamini.
“Hivi Sponsor wako wa masomo hapa chuoni ni nani?” Walter aliuliza.
“Daah, Walter ina maana mpaka leo hujui nani ananidhamini? But sikulaumu, it can be, coz.. Sio part ya masomo yetu wala mapenzi yetu..kwahyo nadra kuliongelea hilo..anyway, mimi nadhaminiwa na shem wangu mwaya” Sarah alijibu kwa manjonjo ya kiswa-english kama wafanyavyo 'wasomi wetu'
“Shem wako unamaanisha mke wa kakaako au mume wa dadaako?” Walter alitaka ufafanuzi bila hata kujua kuwa hapa amechapia.
“Hahhahaaa..Walter usinichekeshe, mke wa kakaangu ni wifi na sio shem, shem ni mume wa dada”.
“Wewe si ulinambia una dada mmoja tu na amefariki ni miezi sasa imepita?”
“Yaah, huyo huyo, aliyekuwa mumewe ndiye anayenisomesha mpaka leo hii.. Namshukuru sana yule kaka, ana roho nzuri mnoo”
“Ok, mi nadhani sio roho nzuri tu, pia ana pesa”
“Yaah, pesa anazo, ni tajiri kwakweli, nadhani utakua unamjua tu kwa jina”
“Anaitwa nani kwani?”
“Anaitwa Mr Khatib”
“Mr Khatib? Khatib Mdharuba au mwengine?” Walter aliuliza kwa hamaki na kumfanya Sarah ashtuke.
“Yaah, huyohuyo, ana nini kwani?”
“Daah, Sarah, huyo mtu sitaki hata kumsikia, mama yake ni mshirikina sana, ndiye sababu ya kifo cha mamaangu”.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Usingizi haukupatikana kabisa usiku huu. Regina aliwaza ni jinsi gani atoke pale lakini ilishashindikana. Ni majira ya saa nne na nusu usiku sasa Hisham akiwa yupo sebuleni 'akizuga' kuangalia tv huku akisubiri Regina alale afanye kazi yake. Regina yeye alifahamu fika kuwa hapakuwa na kheri usiku wa leo, kwahiyo akilala tu ndo moja kwa moja.
Hisham yeye hakuwa na wazo kuwa Regina alifahamu kuhusu mpango huu haramu wa kumuua.
Kwa sasa saa ya mkononi aliyokuwa amevaa Hisham ilisomeka saa tano kasoro, ndipo simu yake ilipoita.
“Kaka mimi ndo naingia Moro hivi, nilichelewa kuondoka Tanga, ila kila nilichokusudia nimekamilisha, niliona ni vyema niwahi ili kesho wakati unapeleka hiyo maiti hospitali tuwe pamoja” Sauti ya Khatib katika simu baada ya salamu.
“Ok sawa kaka, nitajitahidi nikamilishe hii kazi usiku wa leo ili kesho mapema kabisa tukatengeneze ushahidi kaka” Hisham alijibu huku akitegemea kuwa jibu hili moja kwa moja halitamfurahisha bosi wake, na ndicho kilichotokea.
“Unataka kunambia kuwa mpaka sasa bado umeendelea kumuacha huyo mjinga hai? Kweli sina jemedari mwaka huu”. Khatib alimshangaa sana Hisham ambaye alionekana kuzembea ilhali ile ilionekana ni kazi ndogo sana kwake.
“Kaka, nakamilisha wala usijali” Hisham alijitutumua kueleza licha ya kuhisi kuwa bosi wake tayari amekasirika.
“Kaka, unashindwaje kutekeleza haraka mtu upo naye humo ndani na mpo wawili tu? Zana zote unazo kaka, yaani umeshindwa hata kumuekea ile dawa ya usingizi kwenye AC? Kweli kaka? Haya kama hiyo ngumu basi leo umenambia umemuonesha upendo ili akuamini, imekuaje ukashindwa kuweka hata hiyo sumu kwenye ua na kumpa? Si lazima angenusa? Sasa upendo wako ni upi?.. Huo ni ujinga Hisham, sasa nakwambia hivii.. Ikifika asubuhi hajakufa huyo muhuni ujue utakufa wewe”. Khatib alisema kwa hasira.
“Sawa kaka nimekupata, wewe nipe huu usiku halafu utaona”. Hisham aliitikia huku mwili ukimtetemeka.
“Poa, ila nakukumbusha tu kuwa ukiua kwa bastola ujue jela itakuhusu, sitakuwa na msaada kwako”. Mr Khatib alimalizia na kukata simu.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Bado kuna mambo mengi sana ya kujua hapa, Mzee J4 ana mpango gani, vipi kuhusu Walter? Mamaake alikufa vipi hadi Mama Mdharuba kuwa chanzo? Vipi anakufa Hisham au Regina??..Huna sababu ya kukosa Episode 24

busy sana kwa sasa lakini mwezi huu wa 6 ukiisha Episode zitakuja bila kikomo...

Mawasiliano:
mdharuba@gmail.com
+255718274130
 
Mnisamehe kwa kuichelewesha, ila mambo yamekua tait sana, nikimalizana nayo haya mambo basi kila ktu kitakua poa.
 
Back
Top Bottom