Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,103
- 43,350
Labda wengine mmeshaliona hili:
My Take: Sasa kama ni kweli wanafikiria hili au wanaamini hili basi bila ya shaka wanatufikiria sisi sote akili zetu ziko kwenye chupa. Hivi kweli video zote hizi zimewekwa slow motion? Seriously? Inawezekana Lowassa hana matatizo makubwa ya kiafya kama inavyohisiwa na baadhi ya watu lakini kusema kuwa video zimefojiwa ili kumfanya aonekane dhaifu zaidi nadhani si kutendea haki watu wengine. Kuna njia moja ya uhakika pkuondoa wasiwasi huu.
TANGAZO MUHIMU
=========
Kuna Video Clips za Mzee zimefanyiwa Slow Motion Kidogo zinasambazwa ili kupotosha watu waone Mzee anaumwa. Zipo kama tatu hivi ambazo nimekutana nazo. Naamini wengi wengi mmekutana nazo pia, Moja ile ya jogging ya Albino kule Temeke, Moja anakaa kwenye kiti ofisini Na nyingine anatembea, inawezekana zipo zingine ama zitakuja zingine tena. Video hizo mkikutana nazo msishiriki kuzisambaza, pili mzitolee maelezo Haya niliyowapa kwamba zimefanyiwa slow motion kidogo ili kupotosha mana kuna watu wanaamini tena na wengine ni kati yetu pia. Watu wanatakiwa walifahamu hilo kuwa zimefanyiwa slow motion kwa kiwango fulani.
==============
By Jacob Malihoja
Mshauri wa Siasa
Team Lowassa Makao Makuu
"Mtu mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu wakati anajua una akili, ukikubaliana nae anakudharau"- Mwl. Nyerere