Hili tangazo la NMB la Magufuli lipigwe stop

Sina wivu wowote ila najaribu kuweka logic.. Yaani kiongozi wa nchi ambayo anapaswa kuwa neutral anawafanyia tangazo bank moja na kuziweka shakani zingine 50.. Hiyo wewe ndo akili?

Kodi inayokusanywa na hayo ma benki, watanzania walioajiriwa, miradi ya maendeleo iliyokuwa financed na hizo bank, ni kubwa mara ngapi.. Ondoa u CCM utaona makosa hapo
wala usihangaike nae huyu uwezo wake wakufikiri ni mdogo sana ila mada yako ni bora. sijaliona hilo tangazo ila Fair Competition Committee inabidi waingilie kati tangazo lipigwe marufuku
 
Kuna suala kubwa sana la ajira za watu hapa ambalo naona Wakubwa hawalijali kabisa. NMB imeajili wafanyakazi 3,400 tu kati ya wafanyakazi 17,000 wa mabenki nchini. mchezo tunaocheza na ajira za watu wengine 13,000 utaleta madhara makubwa sana kwa uchumi wetu. Makubwa sana.
 
Povu litawatoka sana kwakukosa kujua, sidhani kama hii ni biashara hulia.yatupasa tujue ayo ma bank mengine yameajili watanzania wangapi wanalipa kodi kiasi gani leo hii zifilisike tutatosha Rita?
 
benki nyingi sio msaada wa mtanzania masikini hata zikifa hamna shida...nmb ni benki rafiki kwa wanyonge na masikini
Uwezo na ufahamu wako kuhusu masuala ya uchumi unanitia Shaka sana. Unafahamu chochote kuhusu Corporate tax zinazolipwa na makampuni? unajua chochote kuhusu PAYE inayotokana na ajira?
 
Wananchi wengi tunaendesha maisha yetu kwa kupata mikopo kutoka benki, kama itabaki Benki moja tu, ni wazi maisha yetu yatatetereka kwakuwa riba itakuwa kubwa zaidi na tutashindwa kukopa, mwisho wa siku maisha yatakuwa magum na umasikini utazidi kutawala.
 
Kama ni benki bora acha iwe hivyo tu.. Hamna namna...
Yule mangi kakutuma??!
 
Uwezo na ufahamu wako kuhusu masuala ya uchumi unanitia Shaka sana. Unafahamu chochote kuhusu Corporate tax zinazolipwa na makampuni? unajua chochote kuhusu PAYE inayotokana na ajira?
wewe ndio husomeki.....kwa mfano umeiba gari uachwe kisa unalilipia kodi? mabenki yajikite kwenye kumnyanyua masikini wa kipato cha chini ambao ndio wengi sio kukopesha matajiri tu
 
Kazi ipo awamu ya sinema nyingi
Ningeomba presidential decree ipite mara moja kwenye hili tangazo la kibiashara linalotia hasira na kueneza chuki kwa banking industry nzima.

Mara ya kwanza kutolewa hii kauli, tuliijadili hapa jukwaani na ikaonekana kwamba alichofanya Mh. hakikuwa kitu chenye afya hata kidogo kwa misingi ya kwamba;

1) Bank zote nchini ni za kibinafsi, ikiwa na maana umiliki mkubwa ni wa watu binafsi. Japokuwa kwa bank zilizoenda public, serikali haikuzuiwa kununua share.

2) Bank zote zinahudumia watanzania na zinalipa kodi.

3) Hoja ya kwamba serikali ikipata dividend basi ni faida kwa watanzania ni hoja dhaifu mno mno mno.

Sijui mtizamo wa Rais ulikuwa ni upi lakini ki tafsiri ya haraka ni as if anaona ni raha Tanzania tuwe na NMB peke yake.

So, literally unaweza kusema ni kampeni dhidi kuziangusha benki nyingine. Kwa faida gani tutapata nchi ikiwa na NMB peke yake?

Sijajua pia sheria zanasemaje, kuchukua hotuba ya Rais na kuifanya tangazo. Tangazo lenye dhima ya kuua ushindani wa kibenki.

Halafu sio afya kabisa, sijajua pia italeta taswira gani kwa wafanyakazi wa serikali wanaoomba facilities kwenye benki nyingine.. Naona kama tunatengeneza mazingira magumu pia kwa wafanyakazi wa serikalini.

Sitegemei kulisikia tena hili tangazo redioni. Ni kama vile mtu anakushawishi umchukie Rais.

Fungieni hilo tangazo kwa afya ya ustawi wa banking industry.
tangazo hili kweli litoke tu!kwani halileti taswira nzuri kwa mabenki mengine ambayo ni mengi na yote yanasaidia kukuza uchumi wa nchi na yanachangia kwa kiasi kikubwa pato la serikali!naunga hoja tu tangazo liondolewe!
Ningeomba presidential decree ipite mara moja kwenye hili tangazo la kibiashara linalotia hasira na kueneza chuki kwa banking industry nzima.

Mara ya kwanza kutolewa hii kauli, tuliijadili hapa jukwaani na ikaonekana kwamba alichofanya Mh. hakikuwa kitu chenye afya hata kidogo kwa misingi ya kwamba;

1) Bank zote nchini ni za kibinafsi, ikiwa na maana umiliki mkubwa ni wa watu binafsi. Japokuwa kwa bank zilizoenda public, serikali haikuzuiwa kununua share.

2) Bank zote zinahudumia watanzania na zinalipa kodi.

3) Hoja ya kwamba serikali ikipata dividend basi ni faida kwa watanzania ni hoja dhaifu mno mno mno.

Sijui mtizamo wa Rais ulikuwa ni upi lakini ki tafsiri ya haraka ni as if anaona ni raha Tanzania tuwe na NMB peke yake.

So, literally unaweza kusema ni kampeni dhidi kuziangusha benki nyingine. Kwa faida gani tutapata nchi ikiwa na NMB peke yake?

Sijajua pia sheria zanasemaje, kuchukua hotuba ya Rais na kuifanya tangazo. Tangazo lenye dhima ya kuua ushindani wa kibenki.

Halafu sio afya kabisa, sijajua pia italeta taswira gani kwa wafanyakazi wa serikali wanaoomba facilities kwenye benki nyingine.. Naona kama tunatengeneza mazingira magumu pia kwa wafanyakazi wa serikalini.

Sitegemei kulisikia tena hili tangazo redioni. Ni kama vile mtu anakushawishi umchukie Rais.

Fungieni hilo tangazo kwa afya ya ustawi wa banking industry.
Hili tangazo linaondoa ushindani kwa mabenki!ukizingatia mabenki yote yanasaidia kuendesha uchumi na yanachangia pato la serikali kwa kiasi kikubwa!Mie nadhani linabidi litoke tu maana linachanganya wananchi na kudilute health competition kwenye soko
 
mim nadhani zinge tumika fikra yakinifu katika upembuzi wa swala Hili nyeti la kibenki kma tunavyojua benki industry ndio kila kitu katika Maisha ya watanzania Na wafanyabiashara kwa ujumla katika kukuza uchumi wa nchi kuangalia dividend pekeake Ni pointi zaifu sanaa kwani NMB pekeake haiwezi kukamilisha swala la mikopo kwa watanzania wote hasa wanaohitaji mikopo mikubwa Kama ya viwanda na barabara
 
Kiongozi especially Raisi anatakiwa awahamasishe wafanya biashara wakubwa na mabank yote nchini wafanye biashara kwa nguvuzote kwaajili ya kuinua uchumi wa nchi. Napia kwa wananchi akafanya hivyohivyo , Kama kauli mbiu yake inavyosema Hapa kazi tu, basi angeitumia kuwahamashisha wananchi kufanya kazi, biashara pamoja na mabank ilikuinua kipato, Hakuna nchi iliyoendelea ikawa na Bank moja au wananchi wake wakatumia Bank moja tu. Kwakweli washauri wanahitajika wafanye kazi yao mjengoni.
 
wewe ndio husomeki.....kwa mfano umeiba gari uachwe kisa unalilipia kodi? mabenki yajikite kwenye kumnyanyua masikini wa kipato cha chini ambao ndio wengi sio kukopesha matajiri tu
Mfano wako hauna Mahusiano na mada iliyopo mezani. Acha kulalama bila pointi, mabenki yanatoa mikopo ya kila aina kuanzia biashara kubwa mpaka wajasiliamari na kilimo. Njoo na data hapa za hao watu wa chini walionyimwa mikopo sababu ya utu wa chini wao.
 
Umevurugwa wewe. Wivu unakusumbua
Wewe ndo umevurugwa, asilimia kubwa ya watumishi na watu binafsi wanao weka pesa huko NMB wanaweka kwa kulazimiswa na masharti ya kazi na wala sio kwa matakwa yao binafsi.
 
Mfumo wa kuwa na mabenki mengi inasaidia kuwa na uhakika wa kupata Huduma za kibenki popote unapokwenda. Lakini sipati picha kukiwa na Benki moja!
 
Ulalamishi umezidi sana,mbona rais ameweka data. Hakuna benki inayipa serikali gawio kubwa kama nmb,kodi walipa kubwa,ajira ya watanzania wengi,benki inayohudumia watz wengi na inapatikana sehemu nyingi kama rtd.
Acha wafaidi bana,na hizi benki nyingine zikaze kwenye uwekezaji sio zinabaki mjini tu.
Kama bank from the start ilikuwa na support kutoka serikalini why not isiwe na faida na network kubwa? imagine taasisi zote za serikali zina account hapo pamoja na watumishi wote accounts zao za mishahara zipo hapo na mikopo yao pia, bank ina cheap deposits kutoka serikalini ndo mana mikopo yake niya masharti marahisi huwezi compare na other banks ambazo customers Wake ni Private unatumia Nguyen kubwa kupata wateja, deposits zake ni expensive and risky Kama fixed deposits so automatic bank itakuwa na masharti tight kwenye mikopo yake ambayo haitakuwa rafiki kwa watu wa chini, so acheni kuongea tuu bila kufanya utafiti kwanini other banks haziperform compare na hiyo bank yenu.
 
Sio vema kwa mkuu kuipigia debe nmb pekee wakati kuna benki zingine zenye tija kwa taifa...mapato, ajira nk
 
Back
Top Bottom