Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,663
Ningeomba presidential decree ipite mara moja kwenye hili tangazo la kibiashara linalotia hasira na kueneza chuki kwa banking industry nzima.
Mara ya kwanza kutolewa hii kauli, tuliijadili hapa jukwaani na ikaonekana kwamba alichofanya Mh. hakikuwa kitu chenye afya hata kidogo kwa misingi ya kwamba;
1) Bank zote nchini ni za kibinafsi, ikiwa na maana umiliki mkubwa ni wa watu binafsi. Japokuwa kwa bank zilizoenda public, serikali haikuzuiwa kununua share.
2) Bank zote zinahudumia watanzania na zinalipa kodi.
3) Hoja ya kwamba serikali ikipata dividend basi ni faida kwa watanzania ni hoja dhaifu mno mno mno.
Sijui mtizamo wa Rais ulikuwa ni upi lakini ki tafsiri ya haraka ni as if anaona ni raha Tanzania tuwe na NMB peke yake.
So, literally unaweza kusema ni kampeni dhidi kuziangusha benki nyingine. Kwa faida gani tutapata nchi ikiwa na NMB peke yake?
Sijajua pia sheria zanasemaje, kuchukua hotuba ya Rais na kuifanya tangazo. Tangazo lenye dhima ya kuua ushindani wa kibenki.
Halafu sio afya kabisa, sijajua pia italeta taswira gani kwa wafanyakazi wa serikali wanaoomba facilities kwenye benki nyingine.. Naona kama tunatengeneza mazingira magumu pia kwa wafanyakazi wa serikalini.
Sitegemei kulisikia tena hili tangazo redioni. Ni kama vile mtu anakushawishi umchukie Rais.
Fungieni hilo tangazo kwa afya ya ustawi wa banking industry.