Serikali igeni mfano wa NMB kuibadilisha TANESCO

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,641
46,298
Kwa sasa NMB ni benki inayofanya vizuri zaidi ikishindina na CRDB na kuziacha benki nyingine kwa mbali sana. Hii yote imewezekana kwa sababu ya uwekezaji uliotokana na kubinafsishwa kwa sehemu ya benki hiyo kwa kuuza hisa huku serikali nayo ikibaki na 31% ya hisa.

Serikali kama mnaipenda sana TANESCO mnaweza kuibakiza 40% iwe kwenu halafu mkauza hisa za 60% kwa makampuni na matajiri binafsi mbalimbali kwa maslahi ya wote na raia wa nchi hii kwa ujumla.

Ubinafsishaji wa NMB ulileta mageuzi makubwa ya benki hiyo huko nyie serikali mkiendelea kubaki na mkono wenu mrefu katika benki hiyo, mnaweza kufanya hivyo pia TANESCO mtuondolee hii tabu na mateso makubwa ambayo tunapata sasa katika umeme.
 
nmb ilibadilishwa na Mzee Mkapa (RIP) na siyo nmb tu success stories kubwa ni tbl tanzania breweries, sigara tcc au hata tra, sasa hivi unaiona akili yoyote kubwq ya kufanya chochote cha maana?

Mzee Mkapa wakati anakabidhi nchi aliaacha sound western chritian economic system na hela ndefu hazina, miezi 6 tu walilamba zote kwa anasa, sasa hivi wako bize kununua magoli …
 
Back
Top Bottom