Hili la wanajeshi kutumia ilani ya chama imekaaje?

Hili la wanajeshi kutumia ilani ya chama imekaaje?

Juzi wakati Mheshimiwa Waziri wa ndani akihutubia maafisa wa juu wa vyombo vya ulinzi aliwauliza ni wangapi wana ilani ya chama na wanyooshe juu.

Wakabaki kutazamana tu kila mtu anamuangalia mwenzake.

Hivi jamani Afisa wa polisi, magereza, uhamiaji au zimamoto anatakiwa kutembea na Ilani ya chama?

Maana kwa mujibu wa katiba wao wanatumia sheria ya kulinda serikali na wananchi bila kufuata ilani yoyote.

Je, huyu waziri anajua majukumu ya jeshi au ndio utaratibu Mpya?

Alloooo!!!!!!!
Mpaka sasa wanajaribu kumwiga yule wa jirani kila askari ngazi za juu kushuka chini lazma awe upande wake
 
Hapo ndipo unakosea, mipango ya kuliimarisha jeshi yote ipo katika ilani ya miaka mitano ya ccm, Miradi yote mikubwa ya kimaendeleo ya vyombo vya ulinzi kwa miaka mitano ipo kwenye ilani ya ccm
Hivi unajua unachokisema mkuu, ebu kama huna uhakika kaa uache wanaojua au kasome tena vizuri.
 
Mwanajeshi anaongozwa na sheria za nchi sio ilani mkuu.
Mambo ya ilani ni kwa watoa huduma za kijamii na wala sio massuala ya kulinda nchi. Nihatari sana wanajeshi kuanza kutembea na Ilani la sivyo hakutakuwa na usawa.
Kwani kuna ilani inayoubiri ubaguzi!
 
Sio sahihi kabisa maana Majeshi hayana vyama, Waziri atakua amesahau
 
Ilani ya chama ndiyo imeeleza namna gani masuala ya ulinzi yatafanyika, humo ndimo kuna nyumba za askari, uboreshaji wa miundombinu ya vyombo vyetu vya ulinzi,vitendeakazi vya majeshi nk. Pia kumbuka serikali ni ya ccm na ndio inayopamga ,matumizi ya bajeti ambayo inapitishwa na bunge. Je kama wakuu wa vyombo vya ulinzi hawana ilani inayopangiwa bajeti, watatekelezaji majukumu yao?
Sasa hayo ndio yasabishe askari watembee na ilani ya CCM, kwani wao ndio watayatekeleza? Yaani ilani inawataka askari wajenge nyumba zao?
 
Kilichofanyika katika hiyo Wizara ni kuchelewa kuondolewa ' Pipa ' na kuwekwa ' Jaba ' kwa haraka. Naomba niishie hapa tafadhali.
Mkuu naamini umeamua kufuata ushauri wa hayati baba wa taifa kwenye kitabu chake cha TUJIKOSOE maana leo umeamua kuondoa boliti
 
Wanatekeleza Ilani ya CCM kisheria wala hakuna jipya hapo kila kitu kimeanishwa ndani ya Ilani ya CCM namna gani Serikali itafanya kazi za utekelezaji baada ya uchaguzi....kama ambavyo CHADEMA nayo kama ingeshinda Serikali ingetekeleza Ilani ya CHADEMA yakiwemo na hayo Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

UTAPATA TAABU SANAAAAAA
Unamaanisha huyo waziri yupo sahihi?
 
Mkuu naamini umeamua kufuata ushauri wa hayati baba wa taifa kwenye kitabu chake cha TUJIKOSOE maana leo umeamua kuondoa boliti

Na ukizingatia hata Mimi GENTAMYCINE pia ni ' Mzanaki ' halisi kwa Kabila.
 
Ilani ya chama ndiyo imeeleza namna gani masuala ya ulinzi yatafanyika, humo ndimo kuna nyumba za askari, uboreshaji wa miundombinu ya vyombo vyetu vya ulinzi,vitendeakazi vya majeshi nk. Pia kumbuka serikali ni ya ccm na ndio inayopamga ,matumizi ya bajeti ambayo inapitishwa na bunge. Je kama wakuu wa vyombo vya ulinzi hawana ilani inayopangiwa bajeti, watatekelezaji majukumu yao?
Hongera ndugu
 
Wanatekeleza Ilani ya CCM kisheria wala hakuna jipya hapo kila kitu kimeanishwa ndani ya Ilani ya CCM namna gani Serikali itafanya kazi za utekelezaji baada ya uchaguzi....kama ambavyo CHADEMA nayo kama ingeshinda Serikali ingetekeleza Ilani ya CHADEMA yakiwemo na hayo Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

UTAPATA TAABU SANAAAAAA
Hata mm Nahisi tabu sana, embu fafanua ilani ya chama kwa wanajeshi ikoje mpaka watembee nayo kama katiba!!
 
Back
Top Bottom