Hili la January Makamba ni hatari zaidi

Pesa za kulipa haya makundi atazitoa wapi?dini sijui biashara mara vijana mmmh!!!Ni nani atakuwa kiongozi wa hilo baraza,mkristu au muislam?Washauri wake hawsmtendei haki au la hataki ushauri wa nje
 
nakusoma vema The Boss

 
Last edited by a moderator:
nilikuwa naona kama anaomba urais wa serikali ya wanafunzi, sijui kwa nini wazo hili halinitoki!
 

Naye si kilaza tu!!
maana anshindwa kuwa Tanzania ni scular state. serikali Hian Dini ila watu wake wana dini na uhuru wa dini. kashindwa dogo kupamabanua hilo. wamemdanga akaropke hilo!!
 
Tunalo tatizo tuliowengi tunafikiri Tanganyika ilipoumbwa iikabidhiwa hiyo C C M kiasi kwamba tukiachana nayo basi nchi itayeyuka kubwa hapo ni kuachana na hizi porojo za watia nia wa ccm wamechoka hawana namna mpya ya kufikiri tuwape nafasi wengine mbona nchi zingine zimeachana na mazoea na afadhali kwao zinaonekana kwani ccm ndio niniiii+++
 

ni ukweli tupu Mkuu! akifanikiwa atajuwa rahisi wa ajabu kabisa! Hivi hajui hatari tarajiwa no ule UFA unaopanuka kati ya walionacho na ziada na wasio nacho hata cha kupepea?? hapo haijalishi seen, kabila, rangi, wala lugha mpaka kieleweke..:msela:
 
The Boss

Dini ibaki kuwa ni jambo la mtu binafsi na viongozi wa dini waachwe huko huko kwenye mimbari za dini zao
Unajua mnachekesha sana kuwasoma wakati mwingine. Nirahisi sana kumuona January Makamba amekosea kusema hivyo wakati kila mkutano niliwahi kuhudhuria wa vyama au sherehe za Kitanzania lazima muanze na Asalaam Aleikum - Asifiwe bwana Yesu Kristo, sasa kama mliona kuna makosa ya matumizi ya dini kwa nini hamkuanza na salaam zenu wenyewe mkaweka maneno jingine badala yake?.

Kumbukeni jamani sisi sote tuna dini zetu ambazo ndio mwongozo wa maisha yetu na hakuna kitu kibaya kama serikali ikipoteza mila na desturi za wale inaowaongoza kwa visingizio vya 'Separation of Church and State" kwa sababu wenzetu walifanya hivyo kwa sababu maalum wakipinga sheria moja tu ya Blasphemy ilowanyima Uhuru wa kutoa maoni. Sisi hatuwezi kuepuka Custom law maana ni sehemu ya jamii yetu na hakuna kitu kizuri kama kuwakutanisha viongozi wa Dini inapohitajika.

Hivi tunavyozungumza hufanyika vikao na mara nyingi vimetoa suluhu ya mambo mengi yalokuwa yakichukuliwa kama chuki baina ya imani zetu jambo ambalo lingeweza kabisa kuleta madhara makubwa kama lingepuuzwa. Isipokuwa nakubaliana na wewe sana tu pale serikali inapowaruhusu viongozi wa dini kutoa mwelekezo kwa kisiasa kwa serikali, kinachotakiwa ni wao kupewa maelekezo na serikali wao ni kama Polisi wetu wana serve na ku protect kwa kufundisha mema na kuonya mabaya.. kazi yao sio kutunga sheria bali wanawajibika kufuata sheria.

Dini haiwezi kubakia kama imani ya mtu binafsi ikiwa sisi wenyewe tunatambulishana juu ya Waislaam/Wakristu kama kwamba ni wafuasi wa ama society fulani. And for that needs to be controlled maana Wayahudi wameweza kudai nchi ni yao kwa kutumia dini na ikahalalishwa dunai nzima na sasa tumeona ISIS wakianza kudai nchi... ni mwanzo wa marudio ya kuhalalisha dini kumiliki nchi - Tujihadhari.[/QUOTE]

Mkuu maelezo ya The Boss ni sahihi kabisa.

Mambo ya dini yanatakiwa yasipewe nafasi katika serikali kama alivyoeleza kwa kirefu mtoa uzi huu. Nashangaa kuona wengi tunashindwa kujifunza kwa yanayotokea kwingine. Mifano yako ya Israel na ISIS inatosha kutuonyesha madhara ya kutukuza dini katika siasa.

Tatizo kuu la dini ni watu kusukumwa na imani bila Logic, na hapa ni dini zote (Mifano ni watendayo wakristo kwa waisalam huko Afrika ya Kati, ISIS watendayo kwa wakristo huko mashariki ya kati na Budha watendayo kwa waislam huko Maynmar).
 

I fully concur with you. January is not presidential material. Even after 10 years I would still not opt for January as president. At the moment the fellow is still fairly young but he comes across as the all-knowing type. He appears to believe that his stint at state house, writing JK's speeches made him know everything to do with running of government! The other day at one of the debates at Nkurumah's Hall I saw him on tv asking Mzee Butiku rather mockingly, why the first phase government did not build as many secondary schools as done by the fourth phase administration. When he got into parliament, because he knows everything, his first agenda was the Downs power generating plant. His argument was that it was stupid for the country to go without power while there was the Downs plant lying idle! It was as if there was no cost to be incurred by generating power from that plant! He does not seem to know that from independence Tanzanians learnt to be a proud people despite their poverty. For the period that he led the Parliamentary Energy committee he made it look like an executive organ of government. As for the PCCB, methinks the problem is not the procedure involving the DPP. The problem is lack of political will to tackle corruption. Lack of political will makes our politicians use the office of DPP as a filter to check what goes to court and what does not. Once there is political will the office of DPP will cease to be seen as stumbling block. Remember the Richmond scandal? Was the DPP involved in anyway? Was it not the PCCB themselves who cleared the process as clean, presumably owing to pressure from the politicians?
 
Mifano ya Israel na ISIS ni mifano ambayo waumini wa dini hizo walipuuzwa na serikali hivyo kuanzisha makundi yanayopingana na serikali. Wewe nambie dunia hii ya leo kuna nchi gani isoweka mawasiliano na viongozi wa dini? Na mahala popote kulipotokea matatizo yoyote ya kidini ni kutokana na serikali kuchukua upande mmoja maana kumbuka serikali inaongozwa na watu wenye nimani zao na huwezi kumtenganisha kiongozi na dini yake hata mseme nini.

Akiingia Lowassa atayaona ya upande ule maana ndio anawasiliana nao, Akiingia January naye atawasilikiza wa upande wake maana ndio huwasiliana nao akienda kusali. Inawezekana pia watu wake wa karibu na washauri wakawa wa dini yake ndivyo binadamu tulivyoumbwa unachagua marafiki kutokana na kukaribu wenu na kuelewana na yote nimatokeo ya mawasiliano.

Unaweza kumundoa Simba Serengeti lakini huwezi kuondoa Unyama wake. Simba atabakia kuwa Simba. Nasi kama binadamu imani za dini zimo ndani ya hisia zetu maana unaposema serikali kumbuka serikali ni WATU wenye imani zao, makabila yao na hata jinsia. Siri kubwa ya kuondosha Ubaguzi iwe Udini, Ukabila na Jinsia nchini ni uwezo wa kuchanganyikana na tukawasiliana kwa lugha moja tunayoifahamu sote kama jamii moja.
 

Mkuu,
Kwanza nikupongeze kwa kusikiliza ile speech ya jana. Na bila kumung'unya maneno ndio speech bora kabisa kuliko zote za watangaza nia. Natumaini utakubaliana na hilo. Sasa kwenye hiyo hoja yako. Hebu soma alivyosema jana. Nanukuu

"Kipaumbele cha tano ni amani, umoja na usalama wa mali na maisha ya Watanzania. Amani na umoja wa nchi yetu ni tunu na urithi tulioachiwa na waasisi wa nchi yetu. Marais wote waliopita wamefanya kazi kubwa ya kuzilinda tunu hizi. Serikali yangu haitakubali urithi huu upotee. Tutafanya jitihada zote ili kujenga maridhiano mapya na upendo miongoni mwa makundi mbalimbali katika jamii yetu. Nitawahusisha viongozi wa dini zote katika hili. Nitaanzisha Jukwaa la Rais na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) litakalokutana kila miezi miwili kujadili na kupanga mikakati ya kuendeleza amani, umoja, upendo na maadili ya jamii. "


Sidhani kama maana yake ni kama ulivyoweka wewe hapo wewe. Kumbuka vizuri sana jinsi Mwalimu Nyerere alivyotumia Bakwata na TEC kuijenga amani yetu NA kuinua maadili ya kiujamaa kipindi kile. Vile vile, kanisa na msikiti kuna intellectual heavyweights ambao sio mbaya Ndugu Rais akiwapa jukwaa kusikiliza shida zao.

Speech yote bado inapatikana hapa

January Makamba - Presidential Campaign Launch on Livestream
 
Wakuu..naomba mwenye namba ya simu ya january makamba anisaidie..tafadhali..asante sana
 
Mkandara, kwa maoni yangu tatizo la udini hapa kwetu siyo kubwa kwa kiasi amabacho baadhi ya watu wanataka lionekane. Tulishajenga msingi mzuri wa kutenganisha dini na serikali na tukapiga hatua kubwa. Tumerudishwa nyuma na wanasiasa wababaishaji ambao wameingiza dini kwenye siasa kwa maslahi yao binafsi. Ufumbuzi mzuri wa tatizo lililosababishwa na wanasiasa ni kurudi kwenye misingi tuliyoanza nayo; siyo majaribio myepesi kama haya ya January. Kusalimia Aleikhum salaam au Bwana Yesu asifiwe kwenye majumuiko ya kijamii siyo udini hata kidogo na hakuna tatizo. Sijui kama January amefanya uchambuzi wowote kuhusu tatizo la udini na kubaini kwamba linasababishwa na masheikh na maaskofu? Mbali na wanasiasa muflisi, tatizo la udini pia linatoka nje; itikadi kali za kidini.
 
Lakini mbona huwa tunaambiwa jamaa ni kichwa sana.

Sasa kama ni kichwa kwa nini mtihani wa fom foo akwapue:becky:?
hamna lolote ! sifa za uzushi tu , kichwa gani kimeshindwa hata kugundua mashine ya kubangua madafu , siasa za ccm ni ujanjaujanja tu .
 
Hii ni mada bora kwa uhai na ustawi wa Taifa la Tanzania na watu wake.

Kuwaweka viongozi wadin kwenye attention nikulipeleka Taifa kuzimu. Madai kadhaa yatazua migogoro hatimae machafuko na mwisho vita kamili.

1. Madai ya migawanyo ya madaraka kwa kuzingatia uwiano wa kidin badala ya taaluma za wahusika yatazuka huko.

2. Madai ya haki za kuchinja yataibukia hukohuko

3. Madai ya usawa wakumiliki resources kwa mitazamo ya din yataibuliwa mf. Mahospital, mashule, miradi nk

4. Madai ya migawanyo ya ruzuku bila kufuata utaratibu wala vigezo yataibuliwa ilmradi kila din ipate.

5. Madai ya kutofuga au kufuga baadhi ya wanyama yataibuliwa hatakama katiba inaruhusu.

6. Madai ya zamu yetu kupata urais siyo din yenu yatazuka nk

Kunamigogoro mingi itaibuka nakulitetemesha Taifa na kufarakanisha mtu na mtu, jiran na jiran, mkowa na mkowa nk.

Hili jambo nilakuliogopa kama ukimwi maana unapoingilia nipatamu sana kwa maambukizi mengi ukiachiambali ajali nk lakin UKIMWI UKIINGIA BALAA, KUTOKA NI MATANGA yaan vilio nakusaga meno.

Tusishabikie na kushangilia kifo tujiweke mbali na madhila balaa na hila za ibilisi. Viongozi wadin waache mbali kabisa na serikali isijingize kubeba gunia lililojaa na lijivuja tindikali aina ya cynide (udin) itatuangamizia Taifa letu.

Hongera The Boss hii ni mada bora na muhim sana kwetu na uhai Taifa kwa ujumla.
 
Sijui kama alijiuliza kwamba Bakwata haiwakilishi waislamu wote na wengine hawaikubali kama mwakilishi wao halali. Na pia hata hizo taasisi za kikristo haziwawakilishi wakristo wote, kuna madhehebu ya kikristo hayatangamani na taasisi hizo. Nakubaliana na maoni ya Boss, mtazamo wa Makamba ni too simplistic na itaongeza nyufa.
 
Umeshaambiwa hata mtihani wa fomu foo alikwapua pepa.
Rais gani hajui hata katiba yake inasemaje kuhusu dini.
Laiti Nyerere (R.I.P Mwalimu) angekuwepo akaona uozo unaoendelea.

Ha ha ha,January awe Rais?...sipati picha ya mambo yatakavyokuwa.Hajaomnesha ukomavu ktk maeneo aliyopewa.
 
Kwa kweli inanishangaza kuona viongozi wa serikali wakiapishwa na vitabu vitakatifu vya dini bilakuwa na kipimo cha imani ya mhusika kuhusu vitabu hivyo. Hii ni kulazimisha ndoa ya dini na siasa bila maridhiano. Ingefaa kuapa kwa kutumia katiba. Jambo jingine dini niuhusiano wa mtu na Mungu. Kwa nini dini iruhusiwe kuwa chanzo cha chuki na mifarakano hadi kufikiriwa kuundiwa chombo cha kushughulikia mahusiano ya Mungu na watu?
 
Mkuu kuna mengine tunayachukua kama yalivyo maana ukiingia kwa undani zaidi ya imani za dini utagundua kwamba Yesu hakuwa Mkatoliki wala Mrutheri na hata Muhammad hakuwa Sunni wala Shia bali mcha Mungu, haya madhehebu ya dini tumeanzisha wenyewe na hatari yake ni kubwa toka kuanzishwa kwake hivyo bora kuwepo mawasiliano mazuri baina ya vyombo hivi na serikali kama mshauri. Tunachopinga ni serikali kushirikiana na imani hizi ila huwezi kataza mtu na imani yake utakuwa unaondoa uhuru na haki yake.

Uingereza wameweza tu kukomesha Ugaidi wa IRA kwa kuanzisha mawasiliano bora baina ya vyombo vya dini na serikali. leo wameshindwa kuleta salama huko Mahsariki ya kati kwa sababu serikali zinajaribu kuwasiliana zenyewe dhidi ya dini pasipo kufahamu kwamba chimbuko la misukosuko yote hiyo yote ni mawasiliano mabaya yaliyopo baina ya madhehebu na nasaba zao.

Mahala popote pakisha anza ubaguzi wa aina yoyote iwe dini, Ukabila ama rangi basi ni vizuri sana serikali kuwa karibu na vyombo hivyo, kuwasilikiza na hata kuwashauri juu ya sheria na misngi ilojenga Utaifa wao sio dini zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…