Angalau hakuwa mwizi kama hawa waliopo sasa madarakani.
Angalau hakuwa mwizi kama hawa waliopo sasa madarakani.
Huyu aliwahi kuwa pm na waziri wa pesa yeye alifanya nini cha mno?
Jana ITV nimesikiliza mdahalo uliokuwa ukiilenga Tanzania katika miaka 50 ijayo mmoja wa wageni waaliikwa alikuwa waziri mkuu wa zamani ndg Cleopa Msuya. Katika moja ya hoja zake ilionekana ni kama anauponda waziwazi utawala wa JK, hii ni baadhi ya michango yake;
i. Tz ya miaka 50 ijayo inahitaji Strong leader atakayeweza kusimama na kusema hiki kifanyike na hiki kisifanyike na ambaye ataweza kusimama katika maamuzi magumu (rejea JK kushindwa kuwa na msimamo juu ya matatizo yanayowakabili wa-tz likiwamo umeme)
ii. Tz inakabiliwa na ugonjwa hatari wa malaria, suluhisho sio kwenda kuomba msaada wa vyandarua suluhisho ni kukabili vyanzo vinavyozalisha mbu na vimelea vyake (msaada kutoka serikali ya marekani)
iii. Siku hizi hatuna wataalam wa kutosha katika masuala mbalimbali nchini mfano wa kina Prof. Benno Ndulu na wengine wa miaka ile, leo hii badala ya serikali kupeleka vijana kwa wingi nje ya nchi na kupata wataalam kama vile china na hata kenya, viongozi wamebaki kubuni mbinu mbalimbali zitakazowapeleka nje ili wapate posho kutunisha mifuko yao na kununua magari, nchi haina wataalam wa kutosha kuweza kuleta mabadiliko tunapoingia miaka 50 ijayo.(safari za JK nje ya nchi)
kwa maoni yangu nadhani mzee msuya kaamua kuponda wazi wazi utawala wa JK
<br />aliwahi kutuhumiwa kuhujumu uchumi miaka ya 80. na anatuhumiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika kifo Sokoine, kwakuwa Sokoine alikuwa mstari wa mbele kuwashughulikia wahujumu uchumi wakati ule
<br />Huwezi kulinganisha uwezo wa mawaziri wa Nyerere na JK. Wakati ule kazi ilifanyika basi tu mfumo wa uchumi wa dunia ulikuwa tofauti. Mashirika yote yaliyouzwa na akina Mkapa na JK yalianzishwa na wale jamaa.