Hili la Cleopa ni kama TUSI kwa Jakaya

Assuming kila mtu anatumia chandarua cha msaada wa Kikwete.

Maambukizi hayatakwisha?
 
Hivi kaponda au kaongea ukweli.Mbona sikuelewi.Unataka asifiwe katika upuuzi wote huu.Hapana,anayemsifia Kikwete ana matatizo ya akili.
Jana ITV nimesikiliza mdahalo uliokuwa ukiilenga Tanzania katika miaka 50 ijayo mmoja wa wageni waaliikwa alikuwa waziri mkuu wa zamani ndg Cleopa Msuya. Katika moja ya hoja zake ilionekana ni kama anauponda waziwazi utawala wa JK, hii ni baadhi ya michango yake;

i. Tz ya miaka 50 ijayo inahitaji Strong leader atakayeweza kusimama na kusema hiki kifanyike na hiki kisifanyike na ambaye ataweza kusimama katika maamuzi magumu (rejea JK kushindwa kuwa na msimamo juu ya matatizo yanayowakabili wa-tz likiwamo umeme)

ii. Tz inakabiliwa na ugonjwa hatari wa malaria, suluhisho sio kwenda kuomba msaada wa vyandarua suluhisho ni kukabili vyanzo vinavyozalisha mbu na vimelea vyake (msaada kutoka serikali ya marekani)

iii. Siku hizi hatuna wataalam wa kutosha katika masuala mbalimbali nchini mfano wa kina Prof. Benno Ndulu na wengine wa miaka ile, leo hii badala ya serikali kupeleka vijana kwa wingi nje ya nchi na kupata wataalam kama vile china na hata kenya, viongozi wamebaki kubuni mbinu mbalimbali zitakazowapeleka nje ili wapate posho kutunisha mifuko yao na kununua magari, nchi haina wataalam wa kutosha kuweza kuleta mabadiliko tunapoingia miaka 50 ijayo.(safari za JK nje ya nchi)

kwa maoni yangu nadhani mzee msuya kaamua kuponda wazi wazi utawala wa JK
 
Assuming kila mtu anatumia chandarua cha msaada wa Kikwete.

Maambukizi hayatakwisha?


Msuya yupo right ,kwani Neti ni sehemu tu ya malaria intervetion ....inakusaidia tu pale unapolala dhidi ya mbu wanaouma usiku wa manane ,ambao tunaamini ndio female anopheles........lakini ni wazi ili kuwakinga wote wakiwamo watu ambao wanaumwa na mbu kwa kuwa wanakesha nje kwa sababu mbali mbali au neti zimetoboka.....hata wanaoumwa na mbu wanapotoka kwenye neti kwenda vyooni...kuna jambo la muhimu la kufanya ...nalo ndio tungefurahi wamarekani wakatusaidia ....kujenga miundombinu rafiki dhidi ya malaria[drainages].utafiti....na kubwa tufanye wenyewe kuweka mazingira safi...dhidi ya mazalio ya mbu...haihitaji misaada!
 
Ni sawa kumwambia kiongozi udhaifu wake, lakin tujifunze kuona matatizo kwa kuangakia vyanzo na si matokeo.. kikwete si chanzo cha tatizo TATIZO NI 1.CCM 2.WATANZANIA WENYEWE
<br />
<br />
Naukubali mtazamo wako True Vote hasa kwenye suala la vyanzo vya tatizo. Sijaona like button. Ila mimi ningeanza na watanzania wenyewe kama chanzo cha tatizo kwa sababu CCM ni zao la watanzania na ndio wanaoiruhusu kuendelea kuwepo madarakani. CCM kwa mtazamo wangu imekuwa ni kichaka cha viongozi wabovu, dhaifu na mafisadi.
 
Huo ni ukweli mtupu yaani clear bila chenga,nchi hii haisomeshi wataalamu tena nje ya nchi imebaki kwa wenye fedha,watoto wa vigogo,walimu wa chuo kikuu pekee.na mimi najiuliza itawezekanaje kupata wataalamu wetu wa kuchimba mafuta au migodi ya madini hapa nchini kama zamani?.Nyerere aliweza hilo miaka 50 tunashindwaje baada ya wale wa kwanza kustaafu na kufa.zamani mwanafunzi akipata 1st class high school anatumwa nje kupata ujuzi au akasome ualimu aje kufundisha vijana wetu kwani waliaminika kuwa wana akili na uwezo wa kubadili vijana wetu kielimu. sasa ni kinyume chake 1st class lazima asome TZ na akifaulu vizuri mfano GPA 4.5 - 5 anaendelea na masomo ya Masters na PHD alafu tunamuachia afundishe vijana wetu,hana uzoefu wowote wa kazi au ujuzi wowote zaidi ya kitabu kila kitu anategemea kitabu sasa huku si kuambukiza ujinga watoto wetu?hujafanya kazi uliyojifunza ukapata changamoto yoyote katika kazi vipi unaweza ukawa mwalimu unawarithisha nini watanzania?.angalia mifano ya zamani walimu wengi au wataalamu wengi waliopo sasa baada ya kumaliza shule walifanya kazi miaka 2 ndiyo wakaenda chuo tena baada ya kumaliza JKT hawa ndiy6o wanastaafu sasa,kinafuata kizazi cha hakuna JKT hakuna uzoefu wa kazi (trainee) ni mategemeo gani tunayoyatarajia?.kuna changamoto mpya duniani hivi sasa vijana wetu hawachanganyiki na wenzao duniani kubadilishana uzoefu na kutuletea changamoto mpya unategemea tunajenga Tanzania ya nama gani?.mfano hai ni pale walipomshauri JK kuvunja uwanja wa Uhuru na kuweka majukwaa ya Kichina watanzania walikuwa wanayahitaji hayo majukwaa ya kichina zaidi ya kumbukumbu ya uhuru? kwani ulishindikana kujengwa sehemu nyingine hata b/moyo ukaitwa uwanja wa miaka 50 ya uhuru?sasa wajukuu wetu na vitukuu wakiona zile picha za mwaka 61 wakatuuliza hivi huu uwanja uko wapi tutawajibu nini,haya ndiyo masaibu ya kuwapa madaraka no JKT no Trainee,hawajali kumbukumbu ya nchi wanaangalia pesa tu.KUAMBUKIZA UJINGA.
 
Huyu aliwahi kuwa pm na waziri wa pesa yeye alifanya nini cha mno?

Alifanya mengi yaliyohitajika wakati ule na watu(waliokuwa wamemuweka madarakani) waliridhika. Watu wanatarajia viongozi tulionao sasa wafanye yanayoendana na wakati huu na yanayohitajiwa na waliowaweka madarakani.

Kuna tatizo gani kwa viongozi wastaafu kuwakosoa walioko madarakani? Nao ni sehemu ya wananchi ambao wamewaweka viongozi madarakani, wana haki ya kuhoji/kushauri,Hata kama kulikuwa na mapungufu nyakati zao. Tuwe wasitarabu!
 
Back
Top Bottom