Hii 'zoa zoa' na 'nyakua nyakua' ya Wasafi FM kwa watangazaji mahiri wa redio nyingine inamaanisha nini?

Naliona hilo ila wasiwasi wangu tu ni kwamba vipi Siku moja Mtu anayewapa hii ' Jeuri ' yote CEO wao Msanii Nasib Abdul ' Diamond Platinumz ' ikitokea ' akafilisika ' itakuwaje? Tukumbuke kuwa hakuna Binadamu ambaye ameshahakikishiwa na Mwenyezi Mungu kuwa atakuwa ' Tajiri ' Milele na kwa hapa Tanzania tuna mifano mingi tu ya Watu ambao miaka ya nyuma ndiyo walikuwa na ' Jeuri ' na ' Nyodo ' hasa Kipesa ( Kiutajiri ) lakini leo hii wamekuwa ' Masikini ' hadi ukiwaona Mitaani wanatia Huruma na unaweza hata kutokwa na Machozi. Mmoja wapo kuna Kituo cha DalaDala eneo la Sinza kimeitwa kwa Jina lake.
Maisha ni haya haya mkuu,

Usiogope kutumia pesa eti unaogopa siku ukikosa watu watakuonaje.

Ni navyodhani jamaa anawekeza hivyo kwa kua ameona fursa. Kwanza jamaa atajipatia wasikilizaji wengi wa media zake.Hivyo atajipatia matangazo mengi, pesa inaingia hapo. Ni uwekezaji wa kawaida tu mkuu.
 
Nchi ina watu zaidi ya M. 50 lakini kila siku tunasikia watu hao hao tu! Sijui Kitenge, mara Kumwembe, Sasali, n.k! Waende hata redio za mikoani! Sahara media na IPP media walijitahidi sana kuvumbua vipaji vya watangazaji kipindi kile!
 
Wamekwisa na Kutokota kabisa Waswahili tunasema ' Kwishnei ' kabisa.

Sasa ndio mnasema watawatoa kwenye reli watu walifanya investment na kufanya research? Basi wamlete na Salim Kikeke kama Azam ilivyoweza kuwaleta akina Charles Hilary. Kisa mtu kapata hela kwa ajili ya nanihilu tayari mnaona anaweza kila kitu?
 
Pale EFM ukimtoa Gerald Hando na ile team yake, ukawatoa wale jamaa wanaoendesha kipindi cha Singeli basi kile kituo kinaweza kufungwa kabisa.. Binafsi naona hivyo vipindi ndio roho ya EFM..
 
Kuna tofauti ya kupatikana kwa hizo fursa za Ajira unazosema na wao ( hao Watangazaji ) watakaoajiriwa kuwa ' Competent ' na ' Creative ' kama walioondoka. Na usisahau ukiachilia mbali ' Taaluma ' husika ila kataa kubali kuna kitu kinaitwa Shani ( Nyota ) ya Kimvuto ambayo huwa inamfanya Mtu fulani akiwa mahala fulani na Watu fulani basi anazidi Kukubalika na hata hiyo ' Media ' aliyopo nayo ' inang'aa ' vile vile. Maulid Kitenge, Tido Mhando na Charles Hillary Nkwanga ukiachilia mbali tu ' umahiri ' wao wa Kiutangazaji lakini pia wana ' Mvuto ' wa Kipekee ( hiyo Shani / Nyota ) ambayo Mwenyezi Mungu ' huwatunuku ' Binadamu baadhi tu na kila walipokuwepo walikubalika sana na hata wakiondoka huko Wasikilizaji nao huanza Kupotea taratibu.

Nakuelewa na upo sahihi kabisa mkuu. Nnachomaanisha ni kwamba, hao watu wenye mvuto, vipawa, talanta na vipaji hawajaisha, ingekua ni hao hao tu waliopo tunaowafaham ingekuwa ni tatizo kubwa.

Nakubali kuondoka kwao kutasababisha pengo kwa muda. Kumbuka hata wao walianza kwa kupewa nafasi wakajaribu ndio tunawaona leo wana majina.

Kitu kingine, wrngi wakishafikia umri flani au kuzoea kazi, ubunifu unapungua inabaki ile mazoea. Lakini damu changa na wengine wanaotaka kutengeneza majina na kujenga wasifu wao kwenye fani wanakua na vitu vingi vizuri na hupenda kujaribu wanachoamini kitakuwa kitu kipya, ni hayo tu mkuu.
 
Naliona hilo ila wasiwasi wangu tu ni kwamba vipi Siku moja Mtu anayewapa hii ' Jeuri ' yote CEO wao Msanii Nasib Abdul ' Diamond Platinumz ' ikitokea ' akafilisika ' itakuwaje? Tukumbuke kuwa hakuna Binadamu ambaye ameshahakikishiwa na Mwenyezi Mungu kuwa atakuwa ' Tajiri ' Milele na kwa hapa Tanzania tuna mifano mingi tu ya Watu ambao miaka ya nyuma ndiyo walikuwa na ' Jeuri ' na ' Nyodo ' hasa Kipesa ( Kiutajiri ) lakini leo hii wamekuwa ' Masikini ' hadi ukiwaona Mitaani wanatia Huruma na unaweza hata kutokwa na Machozi. Mmoja wapo kuna Kituo cha DalaDala eneo la Sinza kimeitwa kwa Jina lake.
Hawa wote , ukiwaangalia si waajiriwa wa kawaida... Ajira imebadilika siku hizi, hata watangazaji.. Wao wamekuwa revenue centers kwa vituo vyao.. Hivyo wanachukuliwa kama assets... Kwenye timu za mpira , wanaita wachezaji playing assets.. Sasa imehamia kwa watangazaji, wachambuzi, kwani wao ndio husababisha kituo fulani kipate wasikilizaji wengi.. Sasa hilo la kufilisika au la kwa kituo husika .. Haliwahusu sana, kwa vile wao wanaendeleza kujibrand na wanahamia mahali pengine..

Ungetegemea mtu kama Tido Mhando au Charles Hilary angekuwa amestaafu na hayupo kwenye tasnia, lakini ndio kwanza wanang'ara... Sasa hawa vijana wa umri kama Kitenge, Edo na wengine, ndio kwanza wanaanza jaramba.. Na Mungu amewaangazia mapema..
 
Nimeona akina Zembwela na Kitenge wameanza kuzinanga ofisi walikotokea, eti wanasema mkia hauwezi kutikisa ng'ombe ila ng,ombe ndiye anatikisa mkia.
Hawa jamaa ilibidi wajiepushe sana na maneno ya taarabu kuzisema kwa mafumbo media walikotokea kwa sababu hawajui kesho yao itakuwaje.
Tena kama kitenge inabidi amshukuru sana dj Majizzo aliyemtoa radio one kwa sababu yeye ndoto yake ilikuwa ni kuzeekea radio one, media nyingine nazo zilikuwa zinadhani kumtoa radio one labda haiwezekani.
Nasikia hata siku majizo anatoa wazo la kumtoa radio one, wenzake walidhani kama anaota hivi.
Kwa kinachoendelea, hata radio uhuru wakivunja kibubu wanaweza kumng'oa yeyote yule na sisi wasikilizaji tutahahama tu.
 
Maisha kitu cha ajabu sana, Kijana kutoka Tandale ameweza kuwaajiri na kuwalipa vijana ambao wengine inawezekana wamezliwa na kukulia Masaki na Oysterbay na kusoma best schools in town..

Maisha ya Kijana Diamond ni somo kwa wale wapambanaji na watafutaji wa maisha, hakuna kukata tamaa na Mungu humpa yeyote yule.

Hoja yako hii ni ' dhaifu ' na ' mfu ' kwelikweli Mkuu. Ukisema Diamond ambaye amekulia ' Uswazinyo / Uswahili ' na kwamba hana pia Elimu Kubwa mbona hushangai ' Tajiiri Mwandamizi ' nchini Said Salim Bakhressa ambaye anajulikana hana Elimu lakini ameajiri Wasomi watupu tena hadi Wazungu wa kutoka huko huko Ulaya na Marekani ambako kila Siku Mimi na Wewe ' tunakuota ' Kwenda na hadi hata kutaka ' Kuzamia ' katika Meli?

Na nani aliyekuambia kuwa Kusoma sana / Kuelimika mno ndiyo kuwa na Maisha mazuri na Kufanikiwa Kimaisha? Uwasilishaji wako umekaa Kichukichuki hivi hasa kwa Watu ambao labda wamejikuta ama wamezaliwa hayo maeneo yako tajwa ya Masaki na Oysterbay au wanaishi huko sasa na wala huhitaji Akili kubwa kuweza Kuling'amua / Kulijua hili.

Sasa kama umeanza kwa Kusema kuwa Diamond ametokea huko ' Uswazinyo ' pande za Tandale mbona hujiulizi kuwa hakuendelea Kukaa huko na badala yake amejenga maeno mengine ya Watu wenye ' Status ' zao nchini na hadi huko Masaki / Oysterbay pia ameshanunua ' Mijengo ' na anapangisha Watu?

Msomi Kuajiriwa na asiyesoma siyo tatizo na wala asiyesoma Kuajiriwa na Msomi siyo tatizo lakini ukweli utabaki pale pale kuwa hata kama huyu Tajiri asiye Msomi awe vipi lakini bado Kiuwelewa na Kimkakati hatoweza Kumfikia huyu Msomi Mwajirwa na Masikini. Mwisho kabisa tambua ya kwamba mgawa wa kila Ridhiki ni Mwenyezi Mungu pekee hivyo usije ukatokwa bure na Mishipa ya Shingo huku Mimacho ikikutoka kama Mijusi ya ' Balangulu ' kwasababu tu una Chuki zako na Waishio Masaki na Oysterbay. Kokote tu nchini Mtu ukiishi na kama ukijapanga vizuri unaweza kuyafurahia Maisha.
 
Tatizo la Tanzania ni ubunifu 0. Huyu kahamia huku kapeleka vipindi vyote vya EFM. EFM walikosea sana kutosajili miliki ya vipindi.

Wasafi iko party owned na owners wa CMG hivyo tusitegemee kuona wafanyakazi wa CMG wakinyakuliwa na Wasafi Media
 
Naliona hilo ila wasiwasi wangu tu ni kwamba vipi Siku moja Mtu anayewapa hii ' Jeuri ' yote CEO wao Msanii Nasib Abdul ' Diamond Platinumz ' ikitokea ' akafilisika ' itakuwaje? Tukumbuke kuwa hakuna Binadamu ambaye ameshahakikishiwa na Mwenyezi Mungu kuwa atakuwa ' Tajiri ' Milele na kwa hapa Tanzania tuna mifano mingi tu ya Watu ambao miaka ya nyuma ndiyo walikuwa na ' Jeuri ' na ' Nyodo ' hasa Kipesa ( Kiutajiri ) lakini leo hii wamekuwa ' Masikini ' hadi ukiwaona Mitaani wanatia Huruma na unaweza hata kutokwa na Machozi. Mmoja wapo kuna Kituo cha DalaDala eneo la Sinza kimeitwa kwa Jina lake.
Binadamu wanaishi kwa migongo ya wengine. Bila kujali kama kuna kufa. Kama unajali hilo watu wasingeoana, wasingezaa (maana unapozaa mtoto unajua kabisa utazeeka kabla yake na huenda ukafa kabla yake), wasingeajiriwa na makampuni mbalimbali. Kufa au kufirisika ni mtiririko wa maisha na kampuni ukianzishwa lazima waajiriwa wawepo.
 
Wazoefu na Wataalamu wa haya mambo tusaidiane kidogo katika maswali haya..

Hizi redio na TV stations zinapataje faida kiasi cha kuweza kuendesha biashara na kuendeleza uwekezaji?.
Wanapopewa matangazo. Na ili upewe matangazo lazima uwe na vipindi vinavyovutia wasikilizaji au watazamaji.
 
Wazoefu na Wataalamu wa haya mambo tusaidiane kidogo katika maswali haya..

Hizi redio na TV stations zinapataje faida kiasi cha kuweza kuendesha biashara na kuendeleza uwekezaji?.

Biashara zao wanafanya na wale Abiria ambao huwa wanakuja mara kwa mara na Ndege yenye Jina ambalo pia kwa sasa linatumika na Klabu moja ' maarufu ' nchini Uingereza ( ambao zamani walikuwa na Mchezaji wao tegemeo aitwae Chogo Chemba ) na kila hii Ndege ikitua tu Mkoa wa Wazaramo au ule wa Wachagga utaona Watu wapo ' busy ' mno huku muda mwingine CCTV Camera zikizimwa, sehemu za Mizigo Mitambo huzimwa, wengine hata wasio na ' Diplomatic Status ' utawaona wanapitia VIP Lounges huku wenye Mamlaka ya ' Uangalizi ' wa hivyo Viwanja muhimu kwa ' Mizigo ' inayopeperushwa kiurahisi na Upepo wakiwa wanajifanya kama vile hawaoni Kitu. Hao Abiria wakishuka tu katika hiyo Ndege kimbia katika Hoteli moja ' maarufu ' Masaki ( ambayo Wanamuziki wengi wa Kikongo akina JB Mpiana, Koffi Olomide na Ngiama Makanda Werrason hufikia ) mkabala na ' Slipway ' utawakuta kisha Wenyeji wao ( ambao wengi wao ndiyo hawa unaowaulizia wakishirikiana na wenye Mamlaka baadhi ) hufika hapo kisha ' wanamalizana ' na ndani ya muda utaona ' Utajiri ' wao ukizidi Kuongezeka. Kwa leo naomba niishie hapa tafadhali.
 
Tatizo la Tanzania ni ubunifu 0. Huyu kahamia huku kapeleka vipindi vyote vya EFM. EFM walikosea sana kutosajili miliki ya vipindi.

Wasafi iko party owned na owners wa CMG hivyo tusitegemee kuona wafanyakazi wa CMG wakinyakuliwa na Wasafi Media
Hapo CMG kuna watangazaji gani?!
 
Sasa ndio mnasema watawatoa kwenye reli watu walifanya investment na kufanya research? Basi wamlete na Salim Kikeke kama Azam ilivyoweza kuwaleta akina Charles Hilary. Kisa mtu kapata hela kwa ajili ya nanihilu tayari mnaona anaweza kila kitu?

Na hata huyo Salim Kikeke nae nasikia yupo katika ' Radar ' zao tena Yeye ndiyo akiwa anatakiwa kuwa ' Boss ' Mkuu hapo kama ilivyo kwa Mzee Tido Mhando kule Azam Media. Na inasemekana kuwa hatorudi peke yake bali kuna Vichwa vingine kama Viwili vya Kike atakuja navyo. Wasafi Media wameamua kufanya ' Kufuru ' sasa katika Medani za Kihabari, Mawasiliano na Utangazaji nchini Tanzania na hiyo ' Jeuri ' wanayo kabisa Mkuu japo najua unaonekana una hasira mno na Diamond huku ukionyesha kabisa kuwa Wewe ni ' Team Kiba ' pole yako.
 
Nimeona akina Zembwela na Kitenge wameanza kuzinanga ofisi walikotokea, eti wanasema mkia hauwezi kutikisa ng'ombe ila ng,ombe ndiye anatikisa mkia.
Hawa jamaa ilibidi wajiepushe sana na maneno ya taarabu kuzisema kwa mafumbo media walikotokea kwa sababu hawajui kesho yao itakuwaje.
Tena kama kitenge inabidi amshukuru sana dj Majizzo aliyemtoa radio one kwa sababu yeye ndoto yake ilikuwa ni kuzeekea radio one, media nyingine nazo zilikuwa zinadhani kumtoa radio one labda haiwezekani.
Nasikia hata siku majizo anatoa wazo la kumtoa radio one, wenzake walidhani kama anaota hivi.
Kwa kinachoendelea, hata radio uhuru wakivunja kibubu wanaweza kumng'oa yeyote yule na sisi wasikilizaji tutahahama tu.
Bro sidhani kama wamezinanga hizo media walikotoka kwani nimesikiliza hata mm pia,walitoa kama nukuu ya siku labda kwa tafsiri yako utakuwa sawa lkn usipotoshe kwa ambao hawajasikiliza.....Pia kumbuka wale wote wawili ni wanadaisalama kwa hiyo misemo ni kawaida kwa wenzetu wa pwani.
 
Back
Top Bottom