Hii 'zoa zoa' na 'nyakua nyakua' ya Wasafi FM kwa watangazaji mahiri wa redio nyingine inamaanisha nini?

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Walianza na watangazaji ‘ mahiri ‘ sana wa michezo wakina Maulid Kitenge, Edward Kumwembe, Ahmed Abdallah, Yusuph Mkule, Mwanaidi Suleiman wakimjumuisha na yule mtangazaji waliyemkuta hapa wa michezo Ricardo Momo na jana tena wamemuongeza ‘ Mchambuzi ‘ wa michezo ambaye ndiyo alikuwa akiifanya Magic fm kuwa juu George Ambangile.

Na juzi tena katika kuonyesha kuwa hawana ‘ Masihara ‘ na kwamba wameingia katika ‘ Game ‘ hasa wamemnyakua mtangazaji ‘ mtundu mtundu ‘ Hillary Daud a.k.a Zembwela ambaye atakuwa katika kipindi cha asubuhi na nasikia tena kuwa wiki hii hii kuna watangazaji wengine ‘ mahiri ‘ wa kike na wa kiume wa vipindi vya burudani nao wanaenda kuwachukua.

Habari za chini chini ambazo ' nimepenyezewa ' ingawa bado sijazithibitisha zinasema kwamba baada ya Kumalizana na hao Watangazaji ' mahiri ' wa Michezo sasa wanahamia katika Watangazaji ' mahiri ' wa Vipindi vingine hasa vya burudani, vya kijamii na vile vya ' Kimahaba ' vya Usiku ambapo Redio ambazo kuanzia sasa zikae sawa kwani Watangazaji wake watake wasitake wanaenda ' Kuzolewa ' kama siyo ' Kunyakuliwa ' na Jeuri ya Wasafi Media Company ni hizi zifuatazo:

Ile iliyopo njia panda ya kwenda Coca Cola inatazamana na Taasisi ambayo Wafanyakazi wake wakisikia tu ' Majanga ' yoyote yametokea wao ndiyo huwa wa Kwanza kutokea eneo la tukio.

Ile iliyopo jirani na Mto Mmoja ambao huwa ukijaa hata Ofisi zao Maji hujaa na barabara ya kutoka Ubungo hadi Buguruni Sheli huwa haipitiki kabisa na Malori mengi hupita hapo hapo hadi Treni ya Mwakyembe pia.

Ile iliyopo jirani na Chuo Kimoja Wilayani Kinondoni ambacho Wanafunzi wake hasa wa Kike wakianza Masomo huwa na Nidhamu na Maadili ila baada ya miezi Sita ( 6 ) huanza kuwa ' Makahaba ' na kujiuza eneo la Mita chache na Geti Kuu la Chuo chao hicho

Ile iliyopo njia panda na barabara ya kwenda yalipo Makazi ya Mkuu wa Majeshi wa sasa CDF General Afande Mabeyo na hakuna DalaDala la Kawe ambalo huwa halipiti jirani nao na inatazamana na Eneo maarufu la Burudani na Starehe yenye Jina linalofanana na tarakimu moja iliyopo katika Sinema ya Mcheza Sinema Mkongwe James Bond.

Ile iliyopo eneo la Viwanda Mikocheni ambayo mwaka huu huu karibia 99.9% ya Wafanyakazi wake walitokwa na Machozi japo katika Familia yake sasa hivi ' Moto ' unawaka huko.

Ile iliyopo mkabala na Jengo Moja ( Hoteli ) eneo la Bamaga yenye jina la herufi ' K ' na ipo kwa nyuma yake tu hapo

Shikamooni Wasafi fm na Wasafi tv!
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,813
2,000
Walianza na watangazaji 'mahiri' sana wa michezo - akina Maulid Kitenge, Edward Kumwembe, Ahmed Abdallah, Yusuph Mkule, Mwanaidi Suleiman, wakimjumuisha na yule mtangazaji waliyemkuta hapa wa michezo, Ricardo Momo. Jana tena wamemuongeza mchambuzi wa michezo ambaye ndiyo alikuwa akiifanya Magic FM kuwa juu, George Ambangile.

Na juzi tena katika kuonyesha kuwa hawana 'masihara' na kwamba wameingia katika 'game', wamemnyakua mtangazaji 'mtundu mtundu' Hillary Daud a.k.a Zembwela, ambaye atakuwa katika kipindi cha asubuhi, na ninasikia tena kuwa wiki hi hii kuna watangazaji wengine mahiri wa kike na wa kiume wa vipindi vya burudani nao wanaenda kuwachukua.
Nimesikia Hassan Ngoma na Sasali nao wako katika mazungumzo ya mwisho mwisho na Dangote ili watue hapo Wasafi!
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
51,937
2,000
Walianza na watangazaji 'mahiri' sana wa michezo - akina Maulid Kitenge, Edward Kumwembe, Ahmed Abdallah, Yusuph Mkule, Mwanaidi Suleiman, wakimjumuisha na yule mtangazaji waliyemkuta hapa wa michezo, Ricardo Momo. Jana tena wamemuongeza mchambuzi wa michezo ambaye ndiyo alikuwa akiifanya Magic FM kuwa juu, George Ambangile.

Na juzi tena katika kuonyesha kuwa hawana 'masihara' na kwamba wameingia katika 'game', wamemnyakua mtangazaji 'mtundu mtundu' Hillary Daud a.k.a Zembwela, ambaye atakuwa katika kipindi cha asubuhi, na ninasikia tena kuwa wiki hi hii kuna watangazaji wengine mahiri wa kike na wa kiume wa vipindi vya burudani nao wanaenda kuwachukua.
hata EFM walivyoanza walipita njia hii ya nyakua-nyakua na baada ya muda mpira ukarudi kwa kipa.

cha msingi ajira ya utangazaji inapaswa kuwa na ushindani namna hii ili watangazaji wanufaike kwa malipo mazuri.
 

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
GENTAMYCINE

Nadhani ni namna ya kujibrand zaidi.
Na soon wanaweza kuwa ndiyo the best entertainment media hapa nyumbani.

Naliona hilo ila wasiwasi wangu tu ni kwamba vipi Siku moja Mtu anayewapa hii ' Jeuri ' yote CEO wao Msanii Nasib Abdul ' Diamond Platinumz ' ikitokea ' akafilisika ' itakuwaje? Tukumbuke kuwa hakuna Binadamu ambaye ameshahakikishiwa na Mwenyezi Mungu kuwa atakuwa ' Tajiri ' Milele na kwa hapa Tanzania tuna mifano mingi tu ya Watu ambao miaka ya nyuma ndiyo walikuwa na ' Jeuri ' na ' Nyodo ' hasa Kipesa ( Kiutajiri ) lakini leo hii wamekuwa ' Masikini ' hadi ukiwaona Mitaani wanatia Huruma na unaweza hata kutokwa na Machozi. Mmoja wapo kuna Kituo cha DalaDala eneo la Sinza kimeitwa kwa Jina lake.
 

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Fursa za ajira kwa wanahabari wengine.
Hizo nafasi zote zilizoachwa wazi si zinahitaji watu?

Kuna tofauti ya kupatikana kwa hizo fursa za Ajira unazosema na wao ( hao Watangazaji ) watakaoajiriwa kuwa ' Competent ' na ' Creative ' kama walioondoka. Na usisahau ukiachilia mbali ' Taaluma ' husika ila kataa kubali kuna kitu kinaitwa Shani ( Nyota ) ya Kimvuto ambayo huwa inamfanya Mtu fulani akiwa mahala fulani na Watu fulani basi anazidi Kukubalika na hata hiyo ' Media ' aliyopo nayo ' inang'aa ' vile vile. Maulid Kitenge, Tido Mhando na Charles Hillary Nkwanga ukiachilia mbali tu ' umahiri ' wao wa Kiutangazaji lakini pia wana ' Mvuto ' wa Kipekee ( hiyo Shani / Nyota ) ambayo Mwenyezi Mungu ' huwatunuku ' Binadamu baadhi tu na kila walipokuwepo walikubalika sana na hata wakiondoka huko Wasikilizaji nao huanza Kupotea taratibu.
 

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Nimesikia Hassan Ngoma na Sasali nao wako katika mazungumzo ya mwisho mwisho na Dangote ili watue hapo Wasafi!

Kwa hao Wawili sidhani kwani ukiondoa tu kupenda Kwao ' Kujipendekeza ' kulikopitiliza kwa ' Mamlaka ' husika hawana kingine cha ziada na nitashangaa kama Wasafi Media Company watapoteza muda wao na Pesa yao ' Kusumbuka ' kutaka kuwachukua hawa Watangazaji wako ' Wanafiki Waandamizi ' katika Tasnia hii ya Habari na Utangazaji nchini.
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,855
2,000
Maisha kitu cha ajabu sana, Kijana kutoka Tandale ameweza kuwaajiri na kuwalipa vijana ambao wengine inawezekana wamezliwa na kukulia Masaki na Oysterbay na kusoma best schools in town..

Maisha ya Kijana Diamond ni somo kwa wale wapambanaji na watafutaji wa maisha, hakuna kukata tamaa na Mungu humpa yeyote yule.
 

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Bwana weee leo si nimemsikia zembwela ndani ya wasafi fm

Wanaanza kunivuta kidogo kidogo

Mimi nimeshavutika nao tokea Wiki hii inaanza Mkuu. Japo wanahitaji ' Kuboresha ' vipindi vyao vingine kwani naona ni kama vile ' wamewekeza ' mno katika Vipindi vya Michezo vya ' Sports Arena ' cha Asubuhi na kile cha ' Sports Court ' cha Jioni / Usiku ila kwa vingine ' Vinaboa ' sana Kuvisikiliza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom