Zembwela wa Wasafi FM aitaka Serikali iruhusu Uvutaji wa Bangi kwa Wanaohitaji huku akiisifia mno

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
"Nchi nyingi Siku hizi tena zilizoendelea kama ninayosafiri sana ya Netherlands na nyinginezo zinaruhusu Uvutaji wa Bangi kwa Raia wake wanapotaka sioni sababu ya Tanzania kuzuia wakati Bangi nayo ni Burudani na ina Starehe yake" amesema Mtangazaji wa Wasafi FM Zembwela (Hillary Daud) akiwa Nyumbani kwa Spika wa Bunge na Watangazaji Wenzake ambako kwa Asubuhi ya Leo wanafanyia Kipindi hapo.

Kwa GENTAMYCINE ninayemjua ndani nje Zembwela tokea akiwa Comedian na Rafiki yake Marehemu Max, alipokuwa East Africa Radio na East Africa Tv na Mitaani Sinza, Tandale, Mwenge na Magomeni na nini hasa anachokitumia ndiyo maana Macho yake 24/7 huwa ni Mekundu na Mdomo wake una Uweusi mwingi ngoja ninyamaze na niishie hapa tu.tafadhali.

TCRA Kazi Kwenu na Zembwela alivyo wa hovyo hovyo baada ya Awali katika Maelezo yake kutaka Watanzania tuvute Bangi muda si mrefu Kiunafiki kabisa ametengua hiyo Kauli na Kuzuga kwa kusema Tanzania hairuhusu Uvutaji wa Bangi.

Tafadhali achukuliwe hatua haraka pamoja na hiyo Redio ( Wasafi FM ) kwani kwa Kauli yake tu ya Awali kututaka Watanzania tuvute Bangi na Kuiomba Serikali iruhusu Uvutaji huo wa Bangi tena Hewani ( On Air ) imeleta Usumbufu na inaweza kupokelewa vibaya na tusiovuta Bangi hiyo akina GENTAMYCINE tukashawishika kuanza Kuivuta na Kulanduka nayo vilevile.
 
Namsikia hapa anaongea upopoma huo
Zembwela kaharibu sana Leo na Binafsi najua na Nina uhakika tena wa 100% kuwa Anavuta Bangi na hakuna Mwandishi wa Habari wa Tanzania asiyelijua hili / hilo.

Kama Mvutaji Tukuka wa hiyo Bangi alitakiwa auchune na asiishadadie ila kwa Kuisifia tena Hewani katika Chombo Kikubwa cha Habari cha Wasafi FM ameharibu na amejiharibia sana.
 
Ana hoja asikilizwe.,msiishie kumshambulia tu bila hoja yoyote
Pumbavu eleweni Hoja yangu Kuisemea Hewani kama hivyo tena Redioni ina athari Kubwa na hata Kisheria hairuhusiwi.

Hoja yako hii ingekuwa na Mashiko kama tu ingesemewa Bungeni ambako utungwaji wa Sheria unafanyika. Amekosea.
 
Back
Top Bottom