Mkuu 'CHIEF PRIEST', nimeona nisikuache na jibu nililokupa hapo juu bila ya kukupa msaada katika tafakuri yako ya niliyoyasema hapo..Huu upuuzi aliuleta Nyerere na CCM wanazidi kuubariki.
Kama huoni mchango wa Nyerere katika huu muungano wa mchongo basi wewe ndiye una uwezo mdogo wa kuchambua mambo. Hukumbuki Nyerere alivyokuja juu wakati wa G55 wanataka kuanzishwa kwa serikali tatu jambo ambalo ndiyo muarobaini wa kero za muungano. Nyerere alijua kabisa kuwa Katiba yetu ina mapungufu mengi tu lakini hakufanya lolote kuisaidia nchi kuondokana na janga hili kwa vile aliipenda sana CCM yake kuliko Taifa. Nyerere alikuwa bado na ushawishi wakati huo ndiyo maana aliweza kumng'oa Malecela na Horace Kolimba kwenye nafasi zao kwa vile waligusa muungano wa mchongo.Utajikuta unashiriki katika lawama zisizokuwa na msingi..
Hiyo CCM unayoizungumzia hapa haikuwahi kuwepo wakati wa Nyerere.
Kwa hiyo kumlalamikia Nyerere kwenye mambo ambayo hayakupangwa wakati huo kuwa kama yalivyo leo ni kukosa umakini wa kuchambua mambo.
Naamini uwezo wa kuchambua na kujuwa uhalisia wa mambo unao, ukiamua kukaa chini na kulipa tafakuri sahihi jambo husika.
Nyerere hahusiki na chochote katika upuuzi unaofanyika leo.
Bado hujasema. Nyerere ndiye alituachia janga hili. Elewa pia kuwa lawama nilizotoa si kwa Nyerere peke yake bali kwa CCM pia kuendelea kupita kwenye makosa ya Nyerere,umekurupuka.Mkuu 'CHIEF PRIEST', nimeona nisikuache na jibu nililokupa hapo juu bila ya kukupa msaada katika tafakuri yako ya niliyoyasema hapo..
Msaada wenyewe ni huu wa swali kwako:
Hivi "Kero" za Wazanzibari ambazo zilikuwa na kelele nyingi sana wakati wa Nyerere, zilikwishakwishaje hadi leo hii husikii tena zile kelele za maudhi toka Zanzibar?
Kama bado utaendelea kulalamikia Nyerere kwa haya tunayoyashuhudia leo, inawezekana ukawa nazo sababu nyingine na siyo hili swala la muungano.
LOooo!Kama huoni mchango wa Nyerere katika huu muungano wa mchongo basi wewe ndiye una uwezo mdogo wa kuchambua mambo. Hukumbuki Nyerere alivyokuja juu wakati wa G55 wanataka kuanzishwa kwa serikali tatu jambo ambalo ndiyo muarobaini wa kero za muungano. Nyerere alijua kabisa kuwa Katiba yetu ina mapungufu mengi tu lakini hakufanya lolote kuisaidia nchi kuondokana na janga hili kwa vile aliipenda sana CCM yake kuliko Taifa. Nyerere alikuwa bado na ushawishi wakati huo ndiyo maana aliweza kumng'oa Malecela na Horace Kolimba kwenye nafasi zao kwa vile waligusa muungano wa mchongo.
Hii ni misconception ya nilichoandika. Nilimlaumu Nyerere kwa kutumia ushawishi wake kuzuia mabadiliko ya muundo wa Muungano jambo ambalo hadi sasa liko valid kwani hata Tume ya Warioba ambayo ilikutana na Watanzania wengi zaidi na wengi wao walipendekeza muundo wa serikali tatuikimaanisha kuwa ni hitaji la Wazanzibari na Watanganyika, ila kwa sasa wa kulaumiwa ni wahafidhina waliopo CCM.LOooo!
Hii leo umetoa kubwa yako mkuu 'PRIEST', sijawahi kukusoma hivi.
Hapana wewe unatazama juu juuu 'superficial'; mambo yanayotakiwa kutazamwa kiundani zaidi; hilo ndilo tatizo la wengi.'
Sasa hadi unamsakazia Mwalimu Nyerere kwamba aliipenda CCM zaidi ya taifa lake? Kweli haya unayaandika kwa uamini na dhamira ya moyo wako, au kuna jambo jingine?
Hukuwahi kumsikia Nyerere mwenyewe akiishutumu CCM yenyewe alipoanza kuona inakwenda kivingine?
Naomba tu usinichukulie hapa kuwa namkingia Nyerere madhaifu yake; ninachotafuta ni wewe kuelewa maana ya muundo ulivyofanywa kwa wakati huo; na kwamba hakuna mahali popote panapoelezea kuwa maboresho hayatakuwepo.
Nyerere akatae marekebisho ya katiba kwa sababu ya kuilinda CCM? Hapana
Hiyo habari ya G55 ninaielewa vizuri sana; na hilo haliwezi kuwa sababu ya kudumu hata kama wakati wake umefika.
Bila kukuchosha, nataka tu uwekee maanani hili: Kwamba yanayofanyika sasa hivi kwa jina la CCM, hayo hayakuwa malengo yaliyokuwepo kwa wakati wa Nyerere.
Huwezi kumshawishi yeyote mwenye akili timmu kwamba Nyerere angepanga haya tunayoyaona leo ndiyo yawe matokeo ya muungano aliouasisi.
Sikuwahi kujuwa kuwa unao upeo finyu kiasi hiki unachoonyesha hapa leo.Bado hujasema. Nyerere ndiye alituachia janga hili. Elewa pia kuwa lawama nilizotoa si kwa Nyerere peke yake bali kwa CCM pia kuendelea kupita kwenye makosa ya Nyerere,umekurupuka.
Nyerere hajazuia mabadiliko 2026. Leo tupo hapa, na Nyerere hayupo.Hii ni misconception ya nilichoandika. Nilimlaumu Nyerere kwa kutumia ushawishi wake kuzuia mabadiliko ya muundo wa Muungano jambo ambalo hadi sasa liko valid kwani hata Tume ya Warioba ambayo ilikutana na Watanzania wengi zaidi na wengi wao walipendekeza muundo wa serikali tatuikimaanisha kuwa ni hitaji la Wazanzibari na Watanganyika, ila kwa sasa wa kulaumiwa ni wahafidhina waliopo CCM.
Tatizo lako unataka nifikiri kama unavyofikiri wewe, narudia tena kuwa Nyerere alizuia mabadiliko hayo wakati ule lakini sasa hivi yeye hayupo hivyo wa kulaumiwa ni hawa wahafidhina waliopo CCM, kukataa kumhusisha Nyerere na haya yanayoendelea ni kuikana Historia.Nyerere hajazuia mabadiliko 2026. Leo tupo hapa, na Nyerere hayupo.
Kwa nini waTanzania wa leo tusiwaamini kuwa wanaweza kufanya mabadiliko kufuatana na hali ya leo?
Nyerere hayupo huko CCM. Maamuzi yote yanafanywa na wahuni hao waliopo CCM leo hii; kwa nini lawama iendelee kwa Nyerere kwa maswala yanayotugusa leo!?
Kusema nina upeo finyu huo ni muono wako na mimi pia nakuona huna upeo kabisa huwezi ukalazimisha nifikiri kama unavyofikiri wewe hiyo ni akili ya enzi za giza za zidumu fikra za mwenyekiti.Sikuwahi kujuwa kuwa unao upeo finyu kiasi hiki unachoonyesha hapa leo.
Wewe ulitegemea alichofanya Nyerere ndicho kiwe cha kudumu milele hata kama hali ya nchi na kidunia imebadilika??
Tuendelee kudumu na vyoo vya mashimo, wakati hali ya sasa inaturuhusu kutumia vyo vya kisasa? Walimu mashuleni waendelee na chaki na ubao kufundishia wakati kompyuta za mpakato na vifaa vingine tayari vipo kurahisisha kazi zao?
Muundo wa muungano ulitengenezwa hivyo kwa mahitaji ya wakati huo. Hapakuwekwa na masharti yoyote kuwa muungano umekamilika na hautahitaji kuboreshwa.
Badala ya kuboresha hawa viongozi wa leo ambao ndio ungewatwisha lawama, wameruhusu kuuvuruga; halafu lawama unamtupia Nyerere?
Hapana, wewe huwezi kufikiri kama ninavyofikiri mimi, hilo haliwezekani kabisa.Tatizo lako unataka nifikiri kama unavyofikiri wewe, narudia tena kuwa Nyerere alizuia mabadiliko hayo wakati ule lakini sasa hivi yeye hayupo hivyo wa kulaumiwa ni hawa wahafidhina waliopo CCM, kukataa kumhusisha Nyerere na haya yanayoendelea ni kuikana Historia.
Hujalazimishwa na yeyote; labda ujihisi tu mwenyewe.Kusema nina upeo finyu huo ni muono wako na mimi pia nakuona huna upeo kabisa huwezi ukalazimisha nifikiri kama unavyofikiri wewe hiyo ni akili ya enzi za giza za zidumu fikra za mwenyekiti.
Itoshe tu kusema nimeamua kukupuuza.Hujalazimishwa na yeyote; labda ujihisi tu mwenyewe.
Hapana.Itoshe tu kusema nimeamua kukupuuza.