Gushleviv
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 3,457
- 5,325
Ok angalau hiyo tena kwa umakini, zaidi ya hapo ni high risk120mkuu
Ok angalau hiyo tena kwa umakini, zaidi ya hapo ni high risk120mkuu
Huna adabu, unalinganisha BMW na vigari vyenu vya Japani?Gari yangu ya kwanza kabisa ya kichovu toyota caldina, hapo natoka Moshi kuja dar na sina uzoefu sana na route za mbali, jamaa wa vits naye akaamua eti kunianzishia ligi, mimi niko 110 kph ananipita speed then mbele anaenda anapaki, nikipita tu huyu tena. Ama kweli ukiwa mchovu hata wachovu watataka ligi na wewe. Sasa hivi hata BMW akileta ligi na mimi ajipange kweli kweli, japo sita sahau kamwe dharau nilizoonyeshwa na vits kipindi nina gari la kichovu
Hizi wanazotumia viongoziLandcruiser ipi Mkuu?
Inayoweza kukimbizana na Mercedes-Benz, Aud au BMW?
Kuna maeneo machache sana ambayo unaweza kukimbia zaidi ya Speed 200km/hr kwa hapa Tanzania.Hiyo Speed 220 kwa Barabara zipi??
Wow!! Wanawake wanaopenda ligi barabarani huwa wazuri sana, na wenye umakini mkubwa. [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]Sijui kwanini mtu akikupita unapata mzuka na wewe umpite
Nishafanya ligi moja usiku na altezza
Barabara naijua my daily route muda, sa 6 usiku
Ilibidi nifike 160/170 ili nimuache mbali jamaa ...my gauge ni 180...kushindwa sitakiii alikoma mbona...
Nilisema sitokuja kimbia tena hivii
Sio siri mwendo mkali sio mzuri naishia 120 tu sikuhz
Miaka fulani nilipita toka Tukuyu kwenda Kyela.Kuna maeneo machache sana ambayo unaweza kukimbia zaidi ya Speed 200km/hr kwa hapa Tanzania.
Nitaje machache.
1. Kuna barabara inayoenda Mtwara, kuanzia eneo flani hivi linaitwa Nyamisati hadi ufike Nangurukuru, kuna kipiece hapo kimenyooka vizuri, unaweza kwenda kwa hiyo speed..
2. Barabara ya Kutoka Ushirombo kwenda Runzewe (Geita).
Kuna eneo hapo limenyooka vizuri, na unaweza kwenda hiyo speed, changamoto hapa ni mifugo.
3. Ukitoka Shelui to Senkenke unaweza kwenda hiyo speed pia (changamoto ni mifugo pia)
Hata Kutoka Shelui to Igunga kuna eneo unaweza kimbia vizuri...
4. Kutoka Bahi to saranda ndogo, pamenyooka pia.
5. Kutoka Tabora mjini to Urambo pia kuna sehemu unaweza kwenda hiyo speed...
Bmw ipi?Inapitwa kwa mbali sana kiongozi.
Mkuu ukiwa speed 200km/hr hakikisha mbele barabara ina karibia km 90 bila kona kali au matuta makubwa.Miaka fulani toka Tukuyu kwenda Kyela.
Kuna mkeka msafi sana sema kuna kona za kutosha.
Ila pale unamaliza kisahani fresh kabisa.
Acha ligi tutakulia mchele na maharagwe..Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.
Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.
Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.
Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.
Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.
Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.
Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.
Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..
Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.
Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...
Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,
Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.
Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
Ntanunua hii 3 series3 series, 5series x6
Kwa nn mkuuNakuonea wivu sana comrade.
Mkuu ukiwa speed 200km/hr hakikisha mbele barabara ina karibia km 90 bila kona kali au matuta makubwa.
Wadau wa route ya Mwanza kuna tuta liko km chache kabla hujafika Shy town, pale lazima upunguze speed, halivukiki hata kwa 40km/hr
Hujanielewa mkuu...Inategemea na gari mkuu
Subaru ata barabara fupi inafika
Kuna siku nimeitungua kuanzia pale korogwe(about 60kmph) mpaka karbia na kona ya kimara mwisho (160kmph) na ilikuwa inavuta tu inapanda kwa kasi
N.b
Nilikuwa na masela saa10 usiku
Inaonekana mkuu ukiona hizo 220km/h sijui 240km/h zinakupagawisha balaa,ukikutana na ki golf-gti polo kana 300km/h kuna uwezekano ukaogopa kwenda nako ligi kisa umeona dashboard yake kana speed 300.