Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hizo mambo huwa zipo sana...

Enzi zile hakuna tochi zilikuwa zinafanyika hadi mchana na ajali nazo hazikuwa haba...
 
Kukimbia kote huko Gari za Posta zile Mitsubishi Fuso ikiwa mbele yako kwa dereva muoga kamwe utoipita.

Madereva wa Posta wanatunza sana muda na wanamwaga moto wa kutosha pia wanatii sheria ingawa wapo katika gari za serikali.

Usiku utaishia kuona body nyekundu tuu.
 
Tatizo mkuu haujataja aina ya gari lako.

Umeishia kutaja za wenzako tu.

Embu taja na ya kwako tuithamanishe, pia tujadili ni kwanini ulikuwa unaachwaachwa na kutimuliwa vumbi kizembe wakati ulikuwa unaendesha kishindani?
Nimeitaja mkuu.
 
Hizo mambo huwa zipo sana...

Enzi zile hakuna tochi zilikuwa zinafanyika hadi mchana na ajali nazo hazikuwa haba...
Ikifanyika mchana, tutakufa wengi...
 
Hautakuwa serious kufananisha subaru impreza na BMW...

Mkuu, kama hujui ndo utashangaa ila gari zina tofautiana, bmw zipo aina nyingi sana ila zenye uwezo mkubwa ni chache ni baadhi, sema kwa kuwa zinatoka germany, ni kuwa hazina speed governer ndo maana unaweza dhan zina uwezo zaid
 
Unamaanisha odometer ina 180kph ila inaweza kwenda 280kph?

Hows that possible??

Ndo tatizo hilo tu, fatilia sheria ya nchi na nchi kuhusiana na magar, we ndo yule ukikuta odometer ya VW golf ina 360kmp unabaki kushangaa ukidhan inafika apo
Fatilia mkuu na sio kuangalia dashboard
 
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
Huwa nikitoka zangu mlimani nafika Mombo pale kisha naanza kuwasubiri wazee wa private ila sasa kwa ligi hizo wacha niagize japo usafiri maaana tutaishia kuambiwa subirini na wale wakata tiketi wa Mombo


One day nilibahatika private moja kutoka Mombo kwenda Arusha ( ilikuwa cruiser flani amazing

Siku nyingine nimetoka Mombo kwenda Dar ikaja private moja brevis matata sana


Kwa ujumla napenda ligi ila sio za usiku
 
Hahah daah nimecheka sana,kuna polisi na cruiser yao waliikimbiza Subaru wrx sti hahah aisee walienda kusimulia.
Jf inafurahisha,kuna kipindi tulifanya ligi ya Mwanza to Dodoma yalikuwa magari manne tote V8 sasa sisi tulikuwa vijana watatu na dingi mmoja amevuka 50yrs,mzee tulimpeleka mbaya,, ila utu uzima dawa yule dingi baada ya kuona ligi sio ya kitoto alituovertake wote akatembeza V8 tukawa hatumuoni,huko mbele akaingia machakani akaficha gari sisi tukapita mafuta mabaya tukimtafuta yeye huku nyuma akatoka machakani na kutembea mwendo wake anaoutaka yeye. Yaani tulishindwa hata kula Singida hatuamini kilichotokea,dingi alitukuta Dodoma akatucheka na kujiona wa hovyooo
 
watembea kwa miguu wa JF tufahamiane...
 
sjawah kujua kwamba we ni boy...nkiona hyo avatar huwa nadhan ni KE

Dooh, jambo usilolijua sawa na usiku wa giza, naomba uulize swali ili upate jibu.

Sentensi yako haijaeleweka hataa...
 
Sio wewe nimekuona kwenye uzi fulani hivi unasema Dar -Arusha unatumia 4:30 hrs na kwamba unatembea 130-150Kph usiku?
Usiku sio salama kwa ligi.

Si rahisi kuona zaidi ya 200M, ukiwa speed zaidi ya 100kph, ni ngumu kukwepa hatari ya ghafla.

Usishindane na watu wa magazeti, hao wanapita hiyo njia kila siku tena usiku. Wanaifahamu vizuri sana.

Na usiku kuna ajali nyingi sana za uzembe na kukosa umakini.

Kuwa makini, usishindane na usiemjua.
 
Tatizo watu mnaji mwambafai barabarani na vigari vyenu halafu mnasema ligi, mwisho wake mna jirestisha in pisi wenyewe, mnawaachia ndugu zenu majonzi huku wakisema MUNGU amewapenda zaidi, wakati kumbe nyie wenyewe mmejichukia zaidi.
 
Back
Top Bottom