Hii tabia ya kudharau simu za Tecno itakwisha lini?

Hii tabia ya kudharau simu za Tecno itakwisha lini?

Watu wa Tecno tunadharauliwa sana

Anyway, nimetumia tecno miaka 5 sasa. Sababu, value for money. Kwa bei zake unachopata ni kikubwa sana ukilinganisha na hizi brand kubwa.

Na ikifa au ikiibiwa sina stress, nachukua nyingine faster. Subiri jamaa wa Iphone simu yake iibiwe au ife, anakaa miezi 6 na nokia tochi 😁 😁 😁
 
I phone ukinunulia tanzania nyingi ni feki labda uwe umenunua nje ya nchi dubai na ulaya. Au asia sio china
iPhone zote zina be resembled China , sa sjui unasemaje kuhusu kununua iPhone China , nachojua iPhone nying Kwa Africa ni second hand , sio brand new
 
Aiseee huu mjadala sijui kwann watu wanapanik.
kwani kuna tofauti gani ya miandiko yenu kwenye mjadala huu kusema labda kuna mtu akitumia sim flan ndo mwandiko wake unakaa vizuri au busara yake inapanda?
 
Kwani mkuu kudharauliwa na mtu ambae yuko nyuma ya keyboard yake wewe unapungukiwa nn.

Umewapanikisha watu kwa vitu vya kawaida au umetaka watu wafake life zao?

Wengi wanaojionesha wanatumia sim flani ndio hao hao ambao hawana hizo sim na badala yake wanatumia wanazoziponda mda huu.

Sent using Nokia ya tochi.
 
Juzi nimepiga pcha na simu ya tecno ya mdogo angu ni brand new kabisa ila pcha imetoka kama tupo jikon tunajifukiza halaf muda huo mchana kweupe tupo road
Nkasema mbona tecno hawabadiliki wanashda gan?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
tecno waliponiuzi ni kuwa waliniletea system update basi nika update ..mamaaa kuja kucheki kuna features wameharibu.

kabla sijaupdate ultra power saving mode ilikuwepo ila baadae ikaondoka. si ujuha huu??

Nimeona kitu ambacho wachangiaji hawajakisema ni kuwa tecno hazipendwi kwa sababu akitoa toleo fulani lazima ayumbe sehemu sijui makusudi ama nn

Mf. toleo fulani anaweza boresha specification fulan afu akayumba kwingine eq.battery capacity afu akayumba camera ,au ram .sehemu nyingne rom ikawa nyingi afu ram ndogo

kwa mf me kisimu fulani nilinunua cha tecno mwaka juzi kilikuwa na ram 512MB. afu rom gb 8 .😀😀😀😀 inaitwa tecno S1..

me tecno hapana bora nitumie hata brand za 2014 ambazo zipo nje ya tawi la tecno na michepuko yake kama itel ,inifinix etc..

by the way OPPO anatakatisha moyo wangu navotype hapa
 
China kwa sasa hashikiki katika teknolojia duniani. Hizo simu za wachina kwa sasa zinasumbua sana makampuni makubwa na zinauza sana duniani kote. Marekani ilitumia ujanja katika kompyuta ikakimbilia China kufungua manufacturing plants ili products za China ziweze kuzimwa na hapa walifanikiwa ndio maana komputa karibu zote ni Made in China ingawa makampuni ni ya USA. China gharama za uzalishaji na labour ni cheap sana.

Kwa sisi wafuatiliaji wa uchumi wa dunia tunajua jinsi mataifa makubwa/ mabeberu wanavyoangaishwa na China. Kwenye issue ya 5G kampuni ya ZTE ya China na HUAWEI ndio wanaoongoza duniani katika hiyo teknolojia na kufuatiwa na ERRICSON, SIEMEN na mwisho QAULCOMM (Mmarekani) so ukiangalia Mchina ameshika usukani na si haba simu za iPhone ndio wametoa products sasa zinazotumia 5G wakati HUAWEI na Tecno walitoa toka mwezi wa tisa mwaka jana (ambapo ndio ikazushwa kuwa 5G ilisababisha CORONA).

Kuna sekta nyingine ambayo mchina ameanza kuwekeza haswa ili kushindana na makampuni makubwa duniani ya vifaa vya michezo. China ina products ambazo kwa sasa zimezagaa sana mitaani haswa kwenye mitumba na baadhi ya maduka ya jezi na raba za michezo kama AZAM Sports Shop hapa Dar. Jaribu kufuatilia bidhaa kama ANTA, Li- Ning, PEAK nk kwa sasa zinatamba sana duniani na mwishoni mwa mwaka jana ANTA ya China iliinunua FILA na pia ANTA ilishinda kandarasi ya kuvalisha katika michezo ya OLYMPIC 2020

Msimdharau mchina muda si mrefu dunia yote itashikwa na mchina.
 
Tumia kitu kutokana na uwezo wako na mapenzi yako ukisikiliza watu hutofika popote...leo anaetumia simu nzuri alianza na Siemens A 40...
 
kwa mf me kisimu fulani nilinunua cha tecno mwaka juzi kilikuwa na ram 512MB. afu rom gb 8 .😀😀😀😀 inaitwa tecno S1
Niliibiwaga W5 yangu, mzee akaniboost na hicho kidudue jamani niliteseka 😂 kisimu hakijai hata mkononi, kilijaa fasta kikaanza kustack nikaachana nacho nikanunua kitochi..mpaka sahivi kipo kabatini sina hata pa kukipeleka, nilimpaga mdogo wangu akakikataa
 
Smart phone 3 bora Dunia
1)iPhone
2) sumsung
3)Sony experia
NA hapo Sony na sumsung wanashinda
wangombania namba mbili

Smart phone za hovyo 3 Dunia
1)Tecno
2)Huawei
3)iflix
Mimi sijawai kutumia simu ya smart ya kichina toka simu za kawaida kipindi hiko nilikuwa natumia Nokia sumsung blackberry hizo ndio simu zangu na Sasa natumia Sony kwa matumizi ya kawaida kwa sababu inabebeka na iPad tablet ni ya nyumbani
Tupe Source za data yako sio unakurupuka tu kusema kile unachojisikia....global stats tu za Market share zjnaeleza ubora wa kampuni za simu..
Kwa Africa Samsung ni namba moja ikifuatiwa na Huawei na Apple huku asilimia 6.66% ndio wanaotumia simu unazozisema!
Kwa stats za dunia nzima
1.Samsung
2.Apple
3.Huawei
4.Xiaomi
5. Oppo.
Source: Statscounter.com
20200527_092224.jpg
20200527_092203.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Smart phone 3 bora Dunia
1)iPhone
2) sumsung
3)Sony experia
NA hapo Sony na sumsung wanashinda
wangombania namba mbili

Smart phone za hovyo 3 Dunia
1)Tecno
2)Huawei
3)iflix
Mimi sijawai kutumia simu ya smart ya kichina toka simu za kawaida kipindi hiko nilikuwa natumia Nokia sumsung blackberry hizo ndio simu zangu na Sasa natumia Sony kwa matumizi ya kawaida kwa sababu inabebeka na iPad tablet ni ya nyumbani
Sasa tecno sim nawewe kwanza kama unatumia tecno wewe umepitwa na waka sasa ivi ni Sim za watu wa vijini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliibiwaga W5 yangu, mzee akaniboost na hicho kidudue jamani niliteseka 😂 kisimu hakijai hata mkononi, kilijaa fasta kikaanza kustack nikaachana nacho nikanunua kitochi..mpaka sahivi kipo kabatini sina hata pa kukipeleka, nilimpaga mdogo wangu akakikataa

changu mwezi dec. kiliangukia screen ,hata mood ya kukitengezeza haipo
 
Back
Top Bottom