Think2
JF-Expert Member
- Jan 3, 2025
- 3,077
- 6,001
Unakuta Google Pixel 6 au Pixel 7 ya mtumba inauzwa TSh 400,000 hadi 650,000 Bongo.
Ukipiga picha hapo hapo dukani, inakupa muonekano safi kuliko hata Iphone ya milioni mbili.
Unainunua kwa furaha kutoka Kariakoo, Mlimani City, au kwa wauzaji wa Instagram. Lakini wiki mbili baadaye, unajikuta kwenye kilio cha kimya kimya.
Soko la Pixel za mtumba (Used/Refurbished) nchini Tanzania lina mambo mengi ya siri ambayo wauzaji wengi hawatakuambia kamwe.
Kama unapanga kununua Pixel ya mtumba Bongo, huu hapa ni mwongozo wa mambo 5 ya msingi lazima uyakague ukiwa hapo hapo dukani kabla hujamhamishia muuzaji fedha zako. 🧵👇
1. Elewa kwanza kuhusu vioo vya bandia.
Simu nyingi za Pixel za mtumba zimebadilishwa vioo na kuwekwa vioo vya bei rahisi vya TFT/LCD huko nje:
Kioo kikibadilishwa bila kutumia vifaa rasmi vya Google, mfumo wa alama ya kidole(Fingerprint) unagoma kufanya kazi kabisa.
Kama Fingerprint haifanyi kazi, chukulia kama kioo kilishabadilishwa!
2. Soft unlock kwenye laini.
Pixel zilizokuwa zimefungwa na mitandao ya Marekani (Kama Verizon au AT&T) hufunguliwa kwa njia za muda mfupi za programu (kuflash kawaida)
Zinafanya kazi vizuri dukani, lakini siku ukifanya Factory Reset au kuweka Update mpya, simu inajilock tena na kukataa laini zote za Tanzania.
Mwambie muuzaji akuruhusu ku-reset simu hapo hapo dukani kabla ya kulipa. Akikataa, ondoka.
3. Battery na motherboard.
Huu ndio mtihani wa kifo kwa betri na mfumo wa Pixel yoyote ya mtumba na hata simu nyingine yoyote.
Ingia kwenye kamera, weka settings za hizi za Video weka 4K af chagua 60fps, kisha rekodi video kwa dakika 3 hadi 4 ukiwa hapo dukani.
Mfumo huu unalazimisha processor, kioo, na kamera kutumia nguvu yote ya betri kwa wakati mmoja (sawa na kulipandisha fuso mlima kitonga).
Simu ikizima ghafla, au betri ikishuka kwa zaidi ya 5% ndani ya dakika 3, au kamera ikileta ujumbe wa Overheating na kujizima—hiyo simu ina betri iliyokufa au matatizo ya motherboard. Kwa kawaida itapata joto kwa nyuma ila joto liwe la kawaida sana, ila likizidi na betri ikashuka ghafla, toroka.
4. Mtandao
Google haina ushirikiano wa rasmi na mitandao ya simu nchini Tanzania:
Mtandao wa 5G kwenye Pixel mara nyingi haufanyi kazi moja kwa moja kwenye baadhi ya mitandao ya nyumbani bila kutumia App za ziada.
Hakikisha unaijaribu simu hiyo na laini yako ya internet ukiwa hapo dukani kabla ya kuondoka.
5. Upande wa Spare.
Kabla hujalipa hela, pita kwenye maduka ya spare uulize bei ya kioo halisi cha Pixel 6 au Pixel 7 au hiyo unayotaka kununua.
Kioo halisi cha Pixel kinauzwa hadi 350,000—karibu 60% ya thamani ya simu yenyewe!
Kama huna tabia ya kutunza simu kwa umakini, Pixel ya mtumba inaweza kuwa mzigo mkubwa kwako ikipata hitilafu.
Google Pixel inabaki kuwa simu yenye kamera bora zaidi kwenye soko la mtumba na mfumo safi zaidi wa Android. Lakini sio simu ya kununua kwa kukurupuka tu kwa sababu umeona picha zake ni nzuri dukani.
Hii inaleta swali la kujiuliza kabla ya kuchukua uamuzi wa kununua simu za mtumba:
Je, unaona ni bora kuhatarisha kununua Pixel ya mtumba yenye kamera ya hatari lakini spare zake ni ghali, au ni bora kuchukua infinix ambayo ukiamua una angulia maembe baadae unaweka kioo af salasini tu.
Mimi natumia samsung lakini 😂
You Bella wochi u a bak