Hii tabia ya kudharau simu za Tecno itakwisha lini?

Hii tabia ya kudharau simu za Tecno itakwisha lini?

Tabia ya kudharau simu za Tecno itawaponza milele baadhi yenu milele

Nashangaa hii tabia ikoje kwa sababu ni jambo la kushangaza Watanzania wa humu jf mnadharau simu za Tecno bila sababu zozote zile za msingi

Na watu wamekua wakibeza simu za tecno bila mantiki bila hoja ilhali taifa letu hata kile kichuma au kichwa cha kuchaji simu hatujaweza kuunda

Ni mambo ya ajabu sana katika makampuni yanayojitahidi kutengeneza na kuboresha bidhaa zao ni tecno miaka ya nyuma walikua na changamoto mbalimbali ila kwa sasa wapo vizuri

Angalia uimara wa simu,battery hata camera tunaweza kusema tecno sasa waweza mshindanisha hata na samsung

Kinachosikitisha ni kwamba zaidi ya asilimia 90% ya wana jamiiforum wanatumia tecno

Kama mnakumbuka kipindi ule ujumbe uliokua unatokea kwenye thread au comment za wana humu ule wa "SENT BY USING...

Jf kila mtu ana iphone na samsung ukipost tecno unapopolewa haya mnambie hivi kipind kile cha sent by using....mbona zaidi 90%users zilionekana tecno?hizo iphone au samsung zilipoteleaga wap?

ilionekana zaidi ya 90% ni tecno tu zilikua zinaonekana humu halafu hao hao watu watajifanya wana iphone na samsung tuacheni kufake maisha.

Tuache kubeza kampuni za watu na kuharibu brand za watu jamani mtakujaga kushtakiwa shauri yenu.
Mkuu Tecno zina shida kiasi maana zina stack hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si upambane na tecno yako kimya kimya dada. Simu ni 4 tu duniani Samsung, Huawei , iPhone and 1 plus zilizobaki kama tecno infinix etc ni vifaa vya mawasiliano
 
Hivi unawezaje kutoa pesa yako kabsa na kwenda dukani kununua Tecno labda hiyo pesa niwe nimeokota.
Simu hata kuombea namba kwa mtoto mkali unajifikilia mara mbili mbili.
Mwanaume na ndevu zako kutumia tecno huo ni umama.
 
Viva Tecno...

Nilianzia tecno nilionunuliwa na baba, baba hiyo siku aliniuliza nikuletee simu aina gani nikamwambia naomba dk 2 nakujibu.

Nikamuuliza rafiki angu brand ya kuchukua kati ya Tecno na Huawei, akasema chukua Tecno.
Samsung sikuiweka sababu nilikuwa naona ya mama jinsi ilivyo na camera mbaya mbaya tu

Mpaka sahivi natumia tecno ninazo nunua mwenyewe, sijawahi kuwaza kuhama sijui Tecno wameniroga [emoji30][emoji30]
Umerogwa si bure...
 
Tatizo ni ushabaki tu na fashion. Ila kila sim ni bora kuendana na matumizi yako. Unaweza kuta anaetumia tecno yupo well updated kwa kila information inayotokea dunian kushinda anaetumia iphone.
Kwaiyo ata wala usilalamike kwasababu ww unaetumia tecno unatofauti kubwa na anaetumia iphone, Samsung,sony nk.
 
Nikitongozwa na mwanaume anaetumia tecno siwezi kumkubali na akiniomba number simpi.
Nyie ndio mnaishiaga kwenda kuwasumbua wachungaji na manabii et mnatafta wachumba kumbe we mwenyewe ndo unajiroga.

Kwan kuna uhusiano gan wa hisia za mtu na sim anayomiliki?
Ebu acha bas kujizalilisha na kutuonyesha jinsi gan ulivyo cheap
 
Few years to come Xiami na Vivo wanampiga gap iphone. Maana saiv wanamuhemea kisogoni.
Nakubaliana na wewe. Haitachukua muda Chinese phone makers kui-outsmart Iphone.

Tena wachina wana very aggressive marketing strategy. Wanachukua high end features za simu kama Iphone au Samsung wanaziweka kwenye mid au hing end devices zao na kwa bei ndogo.
 
Mleta mada umefanya utafit gan kujua 90% ya wanaJF wanatumia? Teno,

Hizo simu usipate apointment ya kazi au busnesa ukawnda nayo as gentlemen utapoteza deal[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mtoa maada kuwa mkweli , unatumia tecno sababu ndio unaweza ku- afford.
Imagine mtu akuletee tecno hapa na samsung ya level hio hio utachagua nini?
Obvious utachukua samsung. Tecno hata mimi nimetumia lakini nilikua nimefulia . Nilipopata hela tu nikapiga chini sasa hivi nina samsung .nitanunua tecno tena nikiishiwa hela .
 
Tuna dharau vya wenzetu wakati hata radio call au yale masimu ya mezani hatuwezi kitengeneza?

Tumepumbazwa mno mtu mwenye iphone ya laki 6_7 kumcheka mwenye samsung ya laki tano na mwenye samsung ya laki tank kumcheka mwenye tecno ya laki tatu

Bila kujua pesa mlizonunulia zimejenga uchumi wa mabeberu huku wao wakiwapigisha vita ya maneno kwa kuwaongezea specifications za simu kwenye camera?utadhani mmekuwa wapiga picha)

Kupanua ukubwa wa 'prosesa' na RAM halafu hujawah ku notice any difference kwa maana bado utachomeka laini hizihizi za tigo na airtel ambazo speed yake unapimiwa kwenye kibaba

Wakeup Africa
hahahaha!

full kujimwambafai kisa kumiliki simu ya beberu, waafrika sijui tutaelimika lini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom