Hii taarifa niitoe Takukuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii taarifa niitoe Takukuru?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Aug 19, 2010.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nipe mawazo
  Nimejenga nyumba yangu,sijavuta umeme.
  Nimekwenda TANESCO wakaniambia kuwa natakiwa nguzo tano na kila nguzo ni tsh 400,000 hivyo jumla ni tsh 2m na gharama ya mita ni tsh 460,000 hivyo ili umeme uwake kwangu natakiwa 2.5 m na kuwa kazi hii itakuwa tayari kwa muda wa miezi minne

  Hata hivyo nikiwa natafakari cha kufanya,mtumishi huyo wa ummma akasema lakini kama sitaki risiti na nataka umeme uwajke kwa siku tatu tu nimpatie tsh 800,000 za nguzo na 460,000 za mita na kuwa fedha hizo nampatia tukiwa kwangu.

  Sasa nifanye nini kwani hii ni rushwa,je nitoa taarifa TAKUKURU nikose umeme au nijitose nipate umeme ili nishuhudie heka heka za uchaguzi nikiwa nyumbani kwangu badala ya kuvizia kwenye bar
   
 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  rushwa ni rafiki mzuri.....toa rushwa ufanikiwe kwa Bongo
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Rushwa ndo imetawala Bongo ukisema uende TAKUKURU utakuwa umejipalia mkaa rafiki we toa mkwanja huo upate umeme mwenzio nimejenga Bunju A yalinikuta hayo ila mimi zilikuwa nguzo tatu nikatoa 1.2m akafanya kila kitu sasa nina umeme wa luku bila matatizo na mita inasomeka vizuri tu kwenye mitambo ya tanesco
   
 4. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,226
  Trophy Points: 280
  Rushwa ni adui wa haki.

  kwa maneno mengine, rushwa ni nzuri, rushwa ina haki kuwepo.
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Man mbona hiyo normal price aliyoitaja hapo juu ni cheap. 400,000 kwa nguzo? mi ninajua nguzo ni 1.2m. Sasa hiyo information ya laki nne pengine ni uongo. What i can advise nenda TANESCO mwenyewe ingia ofisini they will give you details. by the way kwa sasa wako kidogo vizuri kama ukishafanyiwa surved na ukalipia then lazima watakufungia umeme within 1 month na wasipofunga wanapaswa kukulipa. That is how it works ndio maana hawato kuruhusu kulipia kama hawako tayari. I think discorage rushwa. Infact hiyo issue si ya takukuru up until mchakato wa kutoa rushwa unaanza.
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Usishangae ukifika TAKUKURU ukaambia utoe kitu kidogo ili suala lako lishughulikiwe mapema na hicho kitu kitatolewa mkiwa nyumbani kwako bila kupata risiti! Like father like son! kumbuka TAKUKURU ni mtoto wa serikali ya CCM
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe aende moja kwa moja Tanesco apate details zote then from there he will know what to do. Nafikir mpaka sasa hivi TAKUKURU is too far away kuwashirikisha kwanza
   
 8. R

  Ramos JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Nimefurahishwa uliposema kuwa kwa sasa ukilipia unafungiwa mapema. Nina mpango wa kwenda kuwafungia wazee huko kileji, lakini nilikuwa nahofu kuwa naweza lipia alaf ikachukua miaka kupata umeme.
   
 9. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani takukuru wanatoa umeme?
   
 10. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Toa rushwa tu,haina jinsi thats how bongo is..fulll stop.
  takukuru sasa wako bize na ccm, na uchaguzi so swala lako halitapewa mkazo
  bongo ni sanaa tupu ndugu,
  mshahara hauendani na matumizi,sasa unadhani pesa ya mafuta,vocha za simu,na mtoto yupo saint academia kanumba ,wife pia ana gari lake, hizo pesa hazitoki ktk mshahara,zinatoka kwa watu kama wewe na mimi,ndo maana ya ule msemo wa kuchangia huduma :):mad2:
   
 11. T

  Tall JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.mpira wa bure na geti liko wazi kwa nini uruke ukuta?
  2.nenda kwa meneja wa kanda husika kamwone '' mweleze kuwa nahisi kuzunguushwa zunguushwa na sina imani kuwa nitaupata umeme.naomba msaada wako.
  3.hapo utapata umeme chapchap.
   
Loading...