Hii ngumu kumeza

Hii ngumu kumeza

Status
Not open for further replies.
Nanga...

Kama ni kweli naamini ule usemi... ...
hakuna mkubwa dunia hii
Muonyeshe kishkaji kama umehisi kitu uone atafanyaje...

Kumuacha si suluhu..

Mbane..
 
Na ndio maana mi huwa sifikirii suala la kuoa..Ona kama hapo, utatumia mda mrefu kusolv hilo mpaka lipite bado linakuja kutokea lingine. Aisee kuna mengi ya kufanya
 
Wewe nahisi umenielewa......inauma sana Braza!!! Inaniumaaa
Kukuelewa kuhusu kumuacha??

Jiangalie kwanza na wewe hwenda huwa unamkwaza ...na ujuwe na yeye ni binadamu na ni dhaifu..

Pia kuna mengi ya kujipanga ....usikurupuke tu.. .

Hem muonyeshe mapenzi mazito ..uchungu wako malizia kitandani..

Atajutia alichofanya!
 
Kila siku mnaaswa kutokagua simu za wenza wenu hamsikii, ukikagua uwe tayari umejipanga kisaikolojia kwa utakachokikuta
 
Natamani unipigie simu nikupe uzoefu.
Kwakuwa wengi humu hatutumii majina yetu halisi. Nakushauri ungetiririka tu uzoefu wako hapa ili wanandoa wengine wapate cha kujifunza kutoka kwako. Wanandoa wengi wanakutana na changamoto hii, sio kitu kipya. Utofauti ni namna wanavyohitimisha tatizo.
 
Kila siku mnaaswa kutokagua simu za wenza wenu hamsikii, ukikagua uwe tayari umejipanga kisaikolojia kwa utakachokikuta
Mimi sinaga hiyo Tabia......ilinilazimu coz nilianza kumtilia shaka.

Halafu kumbuka pia kuna magonjwa ya zinaa+ukimwi.

Kwaio kuna vitu vingine lazima ufatilie inapobidi kwa usalama wangu
 
Mkuu kaa nae mueleze maujinga yake then msikiliza atasema nini then uendelee na maisha...

Kuna mengi ya kufanya kwenye maisha zaidi ya kulia kwenye mapenzi na isitoshe una watoto tayari..

Akikaza kichwa,,,Fyekelea mbaliiii
Unajuaje kwamba watoto ni wakwake?
 
Mkuu, Maumivu yako ni matokeo ya kuishi katika imani ya kwamba umepangiwa 'mtu wako'

Kumbukeni, ndoa na uaminifu ni concepts tulizounda kwa ajili ya kutengeneza jumuiya salama.
Hizo concepts ni abstract. Hazina nguvu against 'mahitaji ya asili'.

Kubali ukweli huu, utakuweka huru.
 
Kwakuwa wengi humu hatutumii majina yetu halisi. Nakushauri ungetiririka tu uzoefu wako hapa ili wanandoa wengine wapate cha kujifunza kutoka kwako. Wanandoa wengi wanakutana na changamoto hii, sio kitu kipya. Utofauti ni namna wanavyohitimisha tatizo.
Kwanza kabisa napingana na hao wanaokataa kuchunguza simu au mawasiliano ya wenza wao, huyo ni mkeo /mumeo wa ndoa,hivyo kufuatilia chochote kile kwake ni 'wajibu'... 'sio wawili tena bali ni mwili mmoja',maana athari zozote zikitokea, ni shared.

Mimi ilikuwa ni msg, nadhani zilisahaulika kufutwa,nikachukulia poa tu kwa ule ujinga eti tusifuatilie simu zitatuvunjia ndoa. Baadye nikaamua kufuatilia karibu mawasiliano ya ile namba, nililenga kujua muda anaopigiwa na how long wanazungumza.

Nikaja kuthibitisha pasipo shaka kuwa waliwahi kuwa katika wahusiano pindi nikiwa masomoni ila wakaja tengana miezi 5 kabla ya mie kurejea masomoni. Uchunguzi huu ulichukua takribani miezi 3 tangu kustukia mawasiliano hayo.

Nilipothibitisha, nikamwomba MUNGU anipe subra, maana ni 'NGUMU KUMESA'. Cha kwanza nikawa tayari kumsamehe, ila nikaweka nadhili kwa muumba wake kuwa, nitamuhoji mara 3 kwa vipindi ni siku tofauti, akikana zote mara 3,ndio ungekuwa mwisho.

Nikaandaa Questionnaire zangu kwa ustadi wa hali ya juu sana na umakini mkubwa kuepuka kuhisi kuwa kuna kitu akistukie, ila swali la mwisho nakumbuka lilimbabaisha na 'akapoteana'.

Ile ya mwisho alikili na akaeleza yote tangu siku ya kwanza hadi walipoamua ku break up, na sababu.

Nilimwambia ampigie jamaa simu na amuite aje nyumbani kwangu, jamaa akazingua, nikampigia nikwambie ndani ya masaa 4 aje kwangu, lasivyo......!! Jamaa alikubali kuja.

Yeye alilia na kueleza kila kitu... Aliomba msamaha nikawasamehe wote. Japo mgoni wangu aliogopa sana baada ya kutoka kwangu alienda kuomba likizo na baadaye uhamisho, nasikia alirudi mkoani kwao maana roho ya hatia ilikuwa ikimwandama. Mke nae kabadilika ajabu, hakutarajia kilichotokea.

Nadhani ndugu yangu huenda ukapata cha kujifunza hapo, japo sikushauri ufuate ufuate njia niliyoifuata, maana kila mtu ni wa pekee. Kuacha nalo wazo zuri, tatizo utayemleta naye hauna uhakika naye. Huo ndio uzoefu nilioupitia.
 
Watoto labda wakapime DNA.
Kama bado hujaongea nae kuna mambo kadhaa ya kufanya mkuu, japo nahisi nimekujua
1. Lazima utafute namna wote wajue kuwa umefahamu (mke na mchepuko)
2. Don't give a room for conversation to both of them
3. Kama una pesa na una sehemu ya kwenda kupumzika angalau mwezi au siku 40, just do it na huko find friends and a girl/woman wa kukuliwaza. Shortly uwe na kampani
4. After that time urudi back to your family ready for another life of less love. Haihitaji kujadili hilo mkuu vinginevyo utasababisha madhara makubwa zaidi, na utajuta.

N.B i)Kumwacha mke mwenye watoto wawili itakutesa maisha yako yote, unachotakiwa kujua ni uko nae kwa sababu ya watoto wako.
ii) Hapa ndipo inapoonekana faida ya kuwa na mpenzi wa pembeni, awe wa kudumu au temporal. Japo wengi tunakuwa nao kwa ajili ya tamaa ila cha msingi ujue wanasaidia sana.
iii) Pole sana ila usimwamini mwanamke kiasi cha kutokuwa na mchepuko. Otherwise ni dm mimi rafiki yako...
 
Hivi unafikiri kuna ndoa ambayo haina cheating!!!!
Wewe pima mwenyewe kuona ni bora kipi, kuacha au kuendelea nae.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom