Hii ndoa inapumulia mashine, ushauri tafadhali

Hii ndoa inapumulia mashine, ushauri tafadhali

totopack

Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
52
Reaction score
10
Nina rafiki/ ndugu ambaye nilisimamia harusi yake(best man) miaka mitano iliyopita, kwa sasa wana watoto wawili.

Tatizo lilianza pale mume alipogundua mke ana madeni sana, anadaiwa na watu mbalimbali (wanaume kwa wanawake) jumla shilingi million 14 ambazo alikuwa anaweka dhamana kadi ya gari nk na analipa kwa riba. Iligundulika baada ya wadai kumpeleka polisi.

Katika kufuatilia mke akasema hajui pesa imefanya nini, jamaa akaamua kulipa deni ili kuondoa hiyo aibu ndipo afuatilie akiwa katikamchakato wa kulipa amegundua mke alimdanganya na kuna sehemu nyingine anadaiwa million 6 na bado anaendelea kukopa kwa kificho hivyo madeni yanaongezeka, jamaa kachanganyikiwa na mimi nimekosa cha kumshauri kwa kweli, humu kuna watu wanapitia changamoto mbalimbali za ndoa naomba tumshauri tafadhalini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza inaonesha huyo jamaa wakati anachumbia huyo bidada hakujipa mda mrefu wa kumchunguza. Yeye kawahi kufunga nae ndoa tu, sasa itabidi imgarim ukwepaji uchunguzi.... Na asimwache mke kwasababu ana watoto nae Ila achunguze tena hela anazifanyia nini, akipata jibu atapata tiba pia.....

Wanaume chunguzeni hawa wanawake wenye vihela chanzo chake ni nini kabla hujamwoa usikurupuke tu. Baadae utashangaa umemwoa kimada wa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwambie wema una kiwango chake na Subra pia inamipaka yake...
 
Kwa hiyo umeshindwa kutuambia mkuu kwamba mwanamme hana say kwa mkewe!
Sasa km anaongozwa hata tukishauri kazi bure maana hawwz arque na top level wake
 
Kwanza inaonesha huyo jamaa wakati anachumbia huyo bidada hakujipa mda mrefu wa kumchunguza. Yeye kawahi kufunga nae ndoa tu, sasa itabidi imgarim ukwepaji uchunguzi.... Na asimwache mke kwasababu ana watoto nae Ila achunguze tena hela anazifanyia nini, akipata jibu atapata tiba pia.....

Wanaume chunguzeni hawa wanawake wenye vihela chanzo chake ni nini kabla hujamwoa usikurupuke tu. Baadae utashangaa umemwoa kimada wa mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli alijitahidi,nawafahamu sana toka muda sema nje kabadirika sidhani kama alikuwa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom