BABA LEA WATOTO
JF-Expert Member
- May 6, 2017
- 339
- 748
Habari ndugu na jamaa wa jukwaa hili!
Nianze kwa kukili kwamba Mimi ni mtumiaji wa muda mrefu wa JF na ID yangu kidogo inajulikana, hivyo nimeamua kubadili ID nyingine kutokana na jambo hili kuwa la kweli hivyo kutumia ID ya zamani pengine isingenipa amani sana kwani baadhi ya jamaa ama ndugu wa karibu wangepata kujua vitu ambavyo kimsingi nisingependa.
Pia natambua sana umuhimu wa mama katika jamii, na hata Mimi kabla ya hali ninayopitia nilikuwa napata homa hata tu nikisikia mama yangu yu mgonjwa ama anatatizo fulani, lakini hii haitoshi kunizuia kuelezea machungu anayonisababishia mama yangu tena mzazi, lengo langu hapa ni kupata msaada/ ahueni ya ninayoyapitia, inafika stage ninawaza hata kujitoa uhai lakini mungu yu mwema roho hiyo imekuwa ikishindwa.
Nilizaliwa katikati ya miaka ya themanini katika familia ambayo nilijikuta baba ni mtumishi wa serikali na mama ni mkulima, baba alitoka moja ya mikoa ya kanda ya ziwa kuja kufanya kazi mikoa ya nyanda za juu kusini, mimi nikiwa ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa mama yangu baada ya Dada yangu huku baba akiwa na watoto wawili aliokuwa amepata kutoka kwa mke wa kwanza waliotengana.
Kumbukumbu nilizonazo ni maisha ya dhika, shiida na tabu tangu utoto huku migogoro ya baba na mama isiyoisha iliyokuwa inapelekea mara kwa mara mama yangu kurudi kwao yeye mwenyewe huku akituacha na baba ama tukienda pamoja, migogoro ya wana ndoa hawa kiukweli na pengine kwa sababu ya utoto hakuna aliyekuwa akijua nini chanzo chake na mwisho wake lini, ilifika kipindi hata kushikiana mapanga, visu ama mashoka ya nyumbani mbele yetu ilikuwa ni kawaida huku tukiishia kulia kwani tusingeweza kuamulia ugomvi na zaidi hata majirani walichoka.
Mwaka 1994 – 1995, baba yetu alikwenda kujiendeleza kimasomo kwenye chuo fulani kwenye mkoa huo, mama yetu kwa sababu alizozijua yeye huku akiwa na watoto sita aliamua kutoka pale alipotuacha baba na kwenda wilaya nyingine kupanga huku akisema hataki kuishi tena na MZEE,kwa hiyo akajichukulia mamlaka ya kubeba kila kitu na kwenda kupanga huku akifanya biashara ndogondogo na sisi tuliokuwa tukisoma akitutafutia uhamisho wa muda, hapa maisha haya kuwa rahisi, kuishi NYUMBA ya kupanga na watoto sita hata vitanda hakuna ni mikeka kutandikwa chini tu na wengine vikojozi du!!!!kwa kweli maisha haya sinta yasaha mbaya zaidi mbaya zaidi mbaya zaidi alikuwa anatuacha hata wiki mbili bila chakula cha kutosha akiaga kuwa anakwenda kwenye biashara huku baba yuko masomoni na hajui kama tumehama.
Baada ya baba kurudi toka masomoni na baada ya vikao vingi na virefu tukarudi tena makazi ya awali, 1996 baba aliamua kustaafu kwa hiari kwa mujibu ya sheria kipindi kile ilikuw ni miaka 50, hapo tukahamia mji mwingine ambako alikuwa amenunua uwanja awali, huko aliendeleza uwanja kwa kujenga nyumba kwa pesa za kustaafu huku akishindwa kuimalizia baadhi ya maeneo, Mimi nikiwa darasa la tano na dada yangu darasa la saba na wadongozangu wengine nyuma yetu, kiufupi hakuna aliyekuwa ameanza hata sekondari japo wale kaka zetu wa upande mwingine nao wakiwa hawajabahatika kuendelea na masomo, mmoja alikuwa nyumbani kwa akina baba na mwingine alifukuzwa Iyunga Tech kwa utovu wa nidhamu baada ya hapo akawa mtu wa stand hadi naandika hatujui yuko wapi hadi leo.
Kwenye makazi mapya maisha yalibadilika ghafla baada ya furaha ya muda mfupi, nyumbani paliendelea kuwa uwanja wa vita mbaya zaidi ugenini, baadaye mama akatoka mwaka 1999 akatengana na baba binafsi nikiwa ndo ninaelekea kumaliza darasa la saba na Dada yangu akiwa kamaliza na yupo nyumbani kipindi hiki ndo kipindi ambacho pengine kilikuwa na mateso zaidi kwani maisha yalikuwa magumu nyumbani hakuna chakula huku baba naye akishinda kusikojulikana lakini baadaye ikabainika kuwa alipata mke mwingine.
Ghafla mimi na mdogo wangu wa kiume aliyenifuata tukaingia kwenye kuhudumia familia, wakati huo pia baba alinipeleka kuanza kidato cha kwanza mwaka 2000 kwenye moja ya shule za sekondari za T.E.W.W, ada yake ikiwa Tsh. 35,000 kwa mwaka, hata hivyo pesa hiyo ilimshinda kulipa kwa wakati na hadi naacha 2002 baada ya shule hizo kufutwa na Mungai kulikuwa na deni kubwa.
Maisha yalikuwa magumu kweli kweli unaweza shinda njaa siku nzima hivyo tukaanza kuishi kwa udokozi, mfn. Tulikuwa na ng' ombe mmoja ambaye analishwa akiwa ndani hivyo tukienda kukata majani mimi na mdogo wangu lazima tuibe ndizi, mihogo, mahindi mabichi nk. na kuficha kwenye mfuko wa nyasi za ng'ombe huku wadogo zetu wakitusubiri nyumbani ndo wale, na baba anarudi usiku hana habari nasi, wakati Fulani natoka shule nakwenda kukata majani ya ng'ombe na kuyauza mia mbili kwa gunia ili kupata pesa ya mahitaji na wakati mwingine naiba kipande cha sabuni kwa majirani ili tufue nguo za shule kukwepa aibu na adhabu toka kwa walimu.Maisha yaliendelea kuwa magumu hivyo huku tukiishi maisha ya kutangatanga na kudowea kwa majirani, da jamani njaa mbaya sana isikie tu kwa mtu.
Mwaka 2002 June, aliyekuwa waziri wa elimu wakati huo J. J. Mungai alitangaza kufuta shule zote za taasisi na zile zilizokuwa zinatumia majengo ya shule za sekondari za serikali ziliamriwa zichukue wanafunzi hao pia, Mimi shule yangu haikuwa kwenye mfumo huo hivyo Mimi na wenzangu tukashindwa kuendelea kwani binafasi pesa ya kwenda private school haikuwepo japo shule nilipenda sana. Huo ukawa mwanzo wa shiida nyingine kwangu.
Baada ya miaka miwili yaani 2004, katika kujitafutia nikafanikiwa kutengeneza urafiki na moja ya majirani zetu(kwa sasa namuita baba), huyu alikuwa ni mkimya sana na mpole japo watu wengi walimwogopa kwa ukimya wake, yeye na ndugu yake aliyepo Dar wana pesa nyingi tu, sasa kupitia dhiki nikajikuta najisogeza kwake ili nimsaidie kazi hasa za shamba ili nipate kula.Kumbuka hapa baba yetu nyumbani anarudi usiku na kudai chakula huku hajawahi nunua kwa muda mrefu tu, tena anakuja amelewa chakali, sintasahau siku nipo na rafiki zangu karibu na nyumbani muda ya saa mbili usiku baba kaletwa na wasamalia kwenye tololi kalewa chakali.
Nikiwa na huyo mzee jirani yetu huku tukiwa tunamsaidia shughuli za mbalimbali mwaka 2004, nikawa napata vijisenti hivyo kwa kuwa nilikuwa na malengo ya kusoma na moyo ukiwa unaniuma kuacha masomo na wenzangu wakiendelea, nikawa natunza vijisenti hivyo na kubahatika kununua nguruwe watatu kwa shilling 13,000@, na ilipofika desemba yule MZEE jirani alikuwa na kawaida ya kutupa pesa ya chrismass hasa tarehe 20, alitupa shilling 15,000 mimi na wenzangu ili tukanunue nguo lakini mimi nikatoka nikaenda Mbeya mjini. Hapo kulikuwa na babu mzaa mama yangu, nikatumia nauli shilling 2000, shilingi 13000 nikanunua bidhaa fulani nikaaanza kuzunguka nayo mitaani pale Mbeya Mjini na ilipofika January 2005 nikaanza kusafiri wilayani na mtaji ukakuwa zaidi hadi laki mbili.
Nikawa naenda Makambako hadi Mafinga hapo nakula na kulala guest, ilipofika February nikawa nimepata kama laki nne hiyo ni 2005, nikaamua kurudi nyumbani ili nianze tena shule kwa pesa hiyo na kwa sababu nilikuwa nimeacha nguruwe nyumbani sasa walikuwa wanne mmoja nilipewa nimtunze na mzee mmoja aliyemuuzia shamba yule mzee jirani yetu huko tulikokuwa tukienda kulima.
Kabla sijarudi nyumbani nilipitia Inyara nikakusanya pumba kwani ilikuwa bei nafuu nikanunua na mahindi ya chakula pale ili nirudi navyo nyumbani, lakini pia nilipitia Uyole huku kulikuwa na mdogo wangu wa tatu kunifuata alikuwa anaishi na mama mmoja rafiki wa mama na alikuwa amechaguliwa sekondari moja ya kata hivyo ikanilazimu nimlipie ada, nimnunulie sare za shule, vifaa na michango mingine.
Kufika nyumbani imebaki kama laki na ishirini ndo inatakiwa niende nayo shule, nikamchukua rafiki yangu ambaye alikuwa tayari yupo kidato cha sita, huyu alikuwa ni rafiki yangu pekee ambaye alijua wakati niliokuwa nikipitia toka shule ya msingi na hakuniacha, tulienda shule moja ya kanisa tukamkuta mkuu wa shule ( kutoka nyumbani kwenda na kurudi ni km. 18), mkuu wa shule akatupokea tukamweleza lengo letu ada ilikuwa ni 150,000/= kwa day lakini kulikuwa na michango mingine, tukalipia fomu na baadaye tukalipa shilling 80000 na nikaanza masomo ya kidato cha tatu kwa kuchukua mamba ya kidato cha pili niliyofanya kwenye ile shule ya awali.
.........itaendelea.....
Japo nasikitika kuna watu wanasema eti ni tamthilia da ni kweli hukupitia haya na mimi sikupenda nipitie haya ndo maana unaona ni hadithi za kutunga anyway najua ninachokitaka kutoka kwa waungwani.
Niliendelea na masomo yangu nikitoka nyumbani saa kumi au saa 11 kutegemeana na Mwalimu wa zamu huku nikisoma kwa kibatari. Karibu nyumba zote za jirani zilikuwa na umeme kasoro yetu tu, baada ya siku kadhaa na baada ya kutoka shule nilipata Ujumbe kuwa yule mzee jirani ananihitaji, nilienda nilimkuta yupo sebuleni anapumzika baada ya kutoka shamba, nilipomsalimia akaniulize mbona huonekani na yule mzee uliyechukua nguruwe wake kule shamba analalamika anataka pesa yake?
Nikamjibu sionekani kwa sababu nipo shule kwa sasa isitoshe yule mzee hatukukubaliana hivyo yeye alinipa nimtunze huyo nguruwe na baadaye tugawane faida pengine kwa sababu hajaniona kapata mashaka, mzee akashtuka.Akaniuliza unasoma? Nikajibu ndiyo…..akauliza tena baba kaamua kukurudisha shule? Nikajibu hapana mimi mwenyewe nimetafuta vijisenti kwa ile pesa ya Christmas uliyotupa nilikuwa nafanya biashara ndo nimerudi shule.
Huyu mzee alisikitika sana lakini alinilaumu kwa nini sikumueleza nia yangu ya kusoma muda mrefu kwani yeye asingeweza shindwa kunisaidia wakati tunashinda wote shambani. Akaendelea, kuanzia leo michango na ada zote nichukue kwake na pale nyumbani kwake nipaone kama nyumbani kwetu, hapa machozi yalikuwa yanadondoka kwa mbali kwa furaha iliyokuwa na huzuni kwa niliyoyapitia kwani mzee alikuwa na pesa kuwa tu kwenye himaya yake kulinipa uhakika ya kesho yangu, na ripoti zote za shule nikawa nampatia yeye alifurahi kuona pamoja na changamoto nilizopitia nilikuwa nikifanya vizuri darasani kushinda ndugu zake waliosoma bila shida yoyote.
Mwezi desemba 2005 baba yangu alifariki kwa kuuawa na watu ambao hadi leo hawajulikani hata nia yao haikujulikana, ni huyu mzee jirani alikuja kuniita kwenye nyumba yake mpya huko ndo alikuwa amenipa niwe naishi kabla hajahamia, akaniuliza mara ya mwisho umeonana na baba lini? Nikamjibu juzi, akasema hebu panda gari twende hospitali nasikia anaumwa amelazwa, da sikushtuka sana kufika kwenye geti la hospitali anakunja kuelekea mochwari halafu anaanza kunieleza... Mwanangu we ni mtoto wa kiume vumilia taarifa zilizokuja ni kuwa baba amefariki taarifa zaidi utapewa na polisi twende tuuone mwili kama ni mwenyewe kwanza.
Nilishindwa kujizuia kabisa nikalia sana hasa nikikumbuka ninayopitia. Baadaye tulizika. Wale nguruwe nikauza wawili ili kuendeshea shughuli za msiba na mama akarudi toka alikokuwa akiishi na baada ya muda akaamriwa na jamii abaki nyumbani atunze watoto.
Niliendelea na masomo kidato cha NNE mwaka 2006, na ilipofika mwezi aprili, weekend nilirudi nyumbani, mwaka huo nilihamia shule, nikiwa najiandaa kurudi shule, mdogo wangu wa kike alikuwa darasa la tano nikiwa nyumbani akanifuata akaniuliza kaka nikuandalie chakula si karibu utatoka? Nikamjibu sawa tu akaandaa tukala na akanisindikiza hadi umbali fulani nikamwambia arudi nyumbani.
Siku tatu baadaye nafuatwa shule naambiwa kuna mgeni nyumbani anataka lazima tuonane kumbe yule mdogo wangu aliyeniandalia chakula na kunisindikiza kafariki eti alipatwa na malaria ghafla na kapelekwa hadi hospitaliti ya rufaa lakini alifariki muda mfupi baada ya kufika hospitaliti hii ni tar. 26/4/2006.Na usiku baada ya maziko napata taarifa kuwa dada yangu, wa pili kunifuata kajifungua. Nikapigwa na butwaa kwani hata sikuwahi jua kuwa ni mjamzito.
Baada ya kumaliza masomo ya kidato cha NNE 2006, mwaka 2007 nikachaguliwa kujiunga na kidato cha tano shule moja ya serikali mkoani Mbeya nikaendelea na masomo kwa ufadhili wa yule mzee jirani na mwaka 2009 nikajiunga na chuo kikuu kimoja wapo jijini Mwanza.
Nikiwa chuo Mwanza hapa ndo tatizo lililonifanya nilete uzi huu nilipoanza kuliona, tatizo na mama yangu mzazi, kabla sijaenda chuo yule mzee jirani akanipa ngo'mbe mmoja (ndama) kama zawadi nikajenga banda nikamuacha nyumbani kwa usimamizi wa mama na baadaye Dada yangu mkubwa akawa ametolewa ngo'mbe mmoja kama sehemu ya mali hivyo wakawa wawili, lakini baada ya muda napigiwa simu kuwa ng'ombe hao wameuzwa. Nikamuuliza mama kwanini wauzwe tena bila hata kunitaarifu…..akanijibu ameona pale majirani hawapendi awe na ng'ombe hivyo kila mara wanaumwa ameona bora auze tu. Niliumia sana but nikaachilia yapite. Huku pesa kidogo ninazopata chuoni nawatumia nao nyumbani wanunue mahitaji halafu wanauza ng'ombe sikutaka malumbano.
Mwaka mwingine nikiwa namalizia likizo nakuta hati ya deni kutoka pride ikimjulisha mama kuwa deni lao limepitiliza muda wa kulipa na kwamba wanapanga kuuza vitu vya ndani, kumbe mama yangu anakopa sana pesa nikamuuliza akajibu ni kweli anadaiwa, nikamshauri si vyema kukopa tena anakopa ananunua chakula au matumizi ya kawaida, kesho yake nikamfuata Dada mmoja ambaye alikuwa ni rafiki yangu sana na alinipenda kwa sababu wazo la biashara anayofanya nilimpata mimi, nikamwomba anikopeshe kiasi cha pesa nilipe lile deni na nitamrushia kidogo kidogo nikifika chuo akanielewa nikafuta lile deni pride.
Nilipokuwa chuo pia pesa niliyokuwa napata pamoja na ya field ilinisaidia kununua thamani za nyumbani na kukarabati NYUMBA aliyokuwa kaiacha mzee lengo ikiwa angalau na sisi tuonekane watu.
Baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo mwaka 2012, mwaka 2013 niliajiriwa mwaka huu nikiwa naanza kazi tu mama yangu aliugua ghafla hapo mimi na ndugu zangu tulihangaika sana ili apate kupona kweli baada ya miezi sita alipona, mwaka uliofuata nikawa na program ya kukarabati nyumbani tena kwani nilikuwa na malengo ya kuoa nikafanya hivyo ili nitakapoingia kwenye majukumu ya familia yangu nisiwe na deni kubwa nyumbani nikafanya hivyo.
Mwezi wa December 2014 mke wangu akajifungua so nikawa nyumbani kwa krismas, mdogo wangu wa mwisho akawa amefaulu kuendelea na sekondari nikamlipia ada na michango mingine, muda mfupi baadaye mdogo wangu huyu kaacha shule na kutoroka nyumbani. Kumbe mama yangu anajua alipo na anajihusisha na kibarua gani mimi nahangaika kumtafuta kumbe mama anakwenda na wanaonana na anapewa visenti na huyu dogo baada ya muda nikaja gundua na anamtetea mno nikaamua kumuacha.
Mama yangu akishirikiana na Dada yangu walitaka kunizunguka kuuza plot moja aliyoiacha mzee kwa kuwa niko mbali, wasamalia wakanishtua pindi wapo na mteja nikawapigia simu akapokea dada yangu akanitukana akaniambia hawawezi kuniogopa mimi si Mungu huku mama akinijibu kuwa anataka kula mali aliyochuma na mumewe, kwa kweli niliumia sana sikuamini kama mama ninayemjali ananifanyia hivyo isitoshe kuna madeni nilikuta anayo desemba 2014 kwenye sacoss nikalipa.
Siku moja mama yangu kampigia simu mke wangu akilaumu kuwa mimi simsaidii na mke wangu anasupport hilo mke wangu aliponieleza nilienda nyumbani nikamueleza kwanini amwambie mke wangu mambo mazito na mimi ilihali nipo. Mama akachukia hakutaka mke wangu aniambie akanijibu mwambie mke wako kuna siku nitakuja mtwanga, niliumia sana nikamuuliza kuna lingine ama ni hill tu baadaye nikaondoka lakini baada ya kukaa na kutafakari nikaamua kusamehe. Mwezi disemba 2015 nikamtumia nauli aje nilipo kwa krismas.
Mwaka Jana mama yangu kaamua kuondoka nyumbani na kurudi kwao eti watoto hatumjali mbaya zaidi mwezi Desemba mwaka Jana akaniomba pesa ya sikukuu nikamjibu pesa yangu itatoka ikiwa tu atarudi nyumbani kwetu, akagoma na kuanza kunitukana nikakata simu.
Ameugua hapo katikati sijaacha kumuuguza, nimemtumia Bima lakini nyumba ya baba yangu kaiacha peke yake, mwezi January mwaka huu nikiwa nimembeba mwanangu nikampigia simu nikamuuliza uko wapi akasema yupo kwao nikamwambia nikitaka nimlete mtoto umsalimie ikiwa tu ungekuwa kwetu akanijibu mtoto nimpeleke kwa bibi mzaa mama yake na akikuwa siku akiuliza ni mwambie yeye alifariki. Nililia sana na utu uzima huu. Nimekaa muda mrefu bila kwenda nyumbani nimeamua mwezi wa sita nimeitisha kikao cha familia ili mimi na wadogo zangu tumuite aje atueleze na majibu yake yatatupa nini cha kufanya.
Nimeleta hapa ili mnisaidie mawazo kabla sijaenda mawazo yenu ni muhimu sana kwangu.
Mwisho naheshimu michango ya wadau wote lakini hadi sasa nimejifunza kitu na inaniuma kuona mtu Mimi naumia yeye anasema mi mwongo, mhuni @ mkwepa kodi, anyway kama nimepitia na kuvumilia hayo sioni litakalokuwa jipya.
Mungu awabariki na Jumamosi njema.