Utakuwa una tatizo la msingi. Sijui kama picha hii inaonesha "kulazimishwa" au hata huo mtutu. Na mimi sijaongelea kuwa vitambulisho vinabezwa au la au kuhusu njia zinazotumika ni halali au la. Sijui hata umetoa wapi kwenye post yangu hayo unayoyasema. Nilichosema tu ni kuwa PICHA haioneshi analazimishwa kuchukua kitambulisho na ndio maana nikasema kitambulisho huyu mama alikuwa tayari keshalipia na anachofanya huyo jamaa ni kukiangalia tu!!!
Bro, labda kuna jambo fulani linakuudhi muda huu lakini kwa kifupi umechanganya topics. Ninaongelea PICHA tu!!!
Huu uzi unahusu njia zinazo tumika kuwapatia hao mnao waita wanyonge
Tumeshuhudia hadi polisi wanatumika kuwalazimisha kununua hivyo vitambulisho
Nitarudia tena. Umeleta uzi ukiwa na hoja ya "kulazimisha kununua kitambulisho" na ukaweka picha yenye maelezo kuwa mkuu wa wilaya "akimlazimisha" muuza mchicha kununua kitambulisho. Point yangu nikuwa picha uliyoiweka kama ushahidi unaonesha kitambulisho alichokishika mkuu wa wilaya ni mali ya huyo mama (amekivaa kwa mshipi wa rangi ya blue). Period. Siku nyingine ukitaka kusapoti hoja yako - uwe na video clip la sivo still photo huwa haitetei sana maneno (it is subject to interpretation). Period. Ngoja nisipoteze muda wangu na wewe.
Hii ni serikali ya maigizo hakuna kitu hapo.Hapo chini anaonekana mkuu wa wilaya akimlazimisha mama muuza mchicha kununua kitambulisho kwa sh 20000 wakati huo mchicha wenyewe hata magungu ishirini hayafiki.
Huku ndiyo kuwatetea wanyonge View attachment 1093921
Mkuu hivyo ndio kuwajali wanyonge na mwisho wa siku wanyonge haohao watapiga makofi na kushangilia wanaowakamua wakiwa majukwaaniHapo chini anaonekana mkuu wa wilaya akimlazimisha mama muuza mchicha kununua kitambulisho kwa sh 20000 wakati huo mchicha wenyewe hata magungu ishirini hayafiki.
Huku ndiyo kuwatetea wanyonge View attachment 1093921
Akimlazimisha?!!unajuaje kama anamlazimisha,Hapo chini anaonekana mkuu wa wilaya akimlazimisha mama muuza mchicha kununua kitambulisho kwa sh 20000 wakati huo mchicha wenyewe hata magungu ishirini hayafiki.
Huku ndiyo kuwatetea wanyonge View attachment 1093921
Hii inaitwa kodi ya kichwa iliyokuwepo miaka hiyo ya Nyerere hahahahahahLengo ni kuongeza wigo mapato japo hii ya vitambulisho ni tata sana! Suluhu ni indirect tax,viwandani,bandarini,mipakani.Tukikaa kimya inakuja kila raia above 18 yrs lazima awe na direct tax.
Hao wengine wanasikitika - Rais kuna watendaji watamharibia kura za 2020