Hii ndio sababu kwanini Yesu alizungumzia sana Pesa/ Mali/ Uchumi kuliko maombi

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,775
15,844
Ukiacha Ufalme wa Mungu jambo la pili lililotawala hotuba, story mifano ya Yesu lilikuwa ni Pesa/Mali na uchumi. Hili alilizungumzia sana kuliko Maombi na Imani.

Zipo sababu nyingi, ila hii ni moja ya muhimu sana.

Umasikini ni utumwa. Mwenye mali atatumikiwa na wasionacho. Hii ni kanuni. Yesu alitaka wafuasi wake wawe na uhuru wa kifedha (financial freedom) ili katika hali zote wasiwe watumwa wa matajiri wa dunia hii kama tunavyoona watumishi wa siku za mwisho masikini wanavyopelekeshwa na waumini matajiri.

Ndio maana anasema yeye alifanyika kuwa masikini ili sisi tulio masikini tupate kuwa matajiri.

2 Wakorintho 8:9
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

Mwisho Yesu anajua mwenye uhuru wa kifedha ndio mwenye influence au ushawishi. Ndio maana hata yeye baada ya kufa sasa hivi anatawala kama mfalme wa wafalme mmiliki wa kila kitu. Kwa sasa anainfluence kubwa kuliko alipokuwa duniani ndio maana anasema kwa sasa wanaomfuata watafanya makubwa kuliko enzi zake.

Mwenye uhuru wa kifedha hata akiongea pumba watu hupiga makofi. Je sio zaidi ukiwa huru kifedha huku umejazwa madini ya roho mtakatifu?

Tafakari, chukua hatua.

Ni hayo tu.
Mtumishi Matunduizi
 
Hata Mungu hawapendi masikini sema anawavumilia tu
Na qmesema masikini hawataisha duniani. Maana anajua watu wengi wataendelea kukumbatia mindset za kuishiwa hadi mwisho. Hivyo ukiwa na chochote jua kuna masikini wengi wa kuwasaidia wamekuzunguka hadi mwisho wa dunia.
 
Kondoo wachape kazi waache blabla za kuambiwa pokea hewa huko makanisani.
Mungu alipomuumba adamu adamu moja ya zawadi aliyompa ilikuwa ni kazi. Ndio maana hakuumba dunia nzima eden. Edeni kalikuwa kabustani kadogo tu kenye uzio kisha akamwambia akalime na kukakuza. Maana yake ilikuwa ni jukumu la Adam na mkewe kuijaza dunia lakini pia kufanya expansion ya Eden ili kila qtakayezaliwa anufaike na wasirundikane kwenye hiyo rasilimali ndogo Mungu aliyowapa kama mbegu.
 
Hiyo ni asili tu mkuu .
 
HERI KUWA MASIKINI KATIKA KRISTO MAANA HAO NI MATAJIRI KATIKA ULIMWENGU ULE UJAO
Moja ya laana ya kutotii neno ni umasikini Torati 28.
Na Yesu alikuja kutukomboa kutoka kwenye laana zote za Torati ikiwemo ya kuishiwa.

Kuwa huru kifedha sio lazima uwe bilionea ila ni kutokuwa muhitaji na ombaomba. Paulo anaandika hakuwahi kuhitaji kwa mtu kitu bila kujali walimpa au la ili neno lake lisijekuwa la kujikomb na kujipendekeza akaucha unyoofu wa injili.
 
Halafu Yesu huyohuyo si ndio alisema:

"Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa mbinguni"

Halafu hapa kwenye huu uzi wako, Yesu huyo huyo Anatetea mali(fedha) za kidunia.

Tukiwaambia huyo Yesu wenu hajielewi na Biblia yenu imejaa Contradictions mnakuja na ufafanuzi uchwara...
 
Alisema ni vigumu hakusema haiwezekani. Difficult is not impossible.

Ndio Maana Yesu ndiye tajiru mwenye uwezo hata wa kumfirisi na kummaliza Shetani na vimali vyake anavyohonga wasiojitambua.

Watu wa Imani ni watu wa mambo magumu na Yasiyowezekana. Ndio maana Baba wa imani Ibrahimu alikuwa bilionea.

Ukielewa, waimarishe na wanaokuzunguka.
 
Wanauziwa maneno matupu wenzao wanachukua pesa za kweli kwa jina la sadaka na zaka! Hakuna kati ya hao wanaojiita watumishi wametajirika kwa maneno matupu ya "pokea".
Noma sana mkuu , hawajui hata kama hauamini Mungu au unaamini Mungu bila kuchpa kazi kwa juhudi na akili mambo hayatakwenda.
 
Alisema ni vigumu hakusema haiwezekani. Difficult is not impossible.

Ndio Maana Yesu ndiye tajiru mwenye uwezo hata wa kumfirisi na kummaliza Shetani na vimali vyake anavyohonga wasiojitambua.

Watu wa Imani ni watu wa mambo magumu na Yasiyowezekana. Ndio maana Baba wa imani Ibrahimu alikuwa bilionea.

Ukielewa, waimarishe na wanaokuzunguka.
Aliyempa Shetani uwezo wa kuwa na mali ni nani?

Shetani alipata wapi uwezo wa kuwa na mali?
 
Aliyempa Shetani uwezo wa kuwa na mali ni nani?

Shetani alipata wapi uwezo wa kuwa na mali?
Alipewa na Mwanadamu. Hakuna sehemu Mungu anampa kitu ibirisi. Ila Anaitwa mfalme wa dunia hii kwa sababu aliyekuwa mfalme Mwanadamu alimpa ufalme aliooewa na Mungu.

Hivi vitu huwezi kuvisikia kwenye madhabahu za kulisha watu fastfoods za miujiza, maajabu na maombezi ya kilaghai.
 
Back
Top Bottom