Hii ndio sababu Adolf Hitler aliuwa Wayahudi

Hii ndio sababu Adolf Hitler aliuwa Wayahudi

Toa elimu mtoto unayempata kabla haujabariki ndoa ni mtoto halali au sio halali?

Halali kwa nani! Hebu tuambie huyo halali anapatikana kwa njia ipi na haramu anapatikana kwa njia!
 
Kwa mujibu wa Historia ni kwamba kabla ya Vita ya kwanza ya Dunia, kulikua kuna idadi kubwa ya Wayahudi waishio Ujeruman.

Hitler alikua ni miongoni mwa wapiganaji wa kijerumani,ujerumani walishindwa katika vita hiyo. Sasa wakati inatangazwa kua Ujerumani imeshindwa vita Hitler yeye alikua amelazwa hospitali kwa matibabu ya majeruhi, basi aliposikia Ujerumani imepoteza vita yeye Hitler hakuamini kabisa eti Ujerumani imeshindwa vita kwani aliamini kua jeshi la Ujerumani lilikua Imara na nguvu mno na lisingeweza kushindwa kwa namna yoyote isipokua kwa kusalitiwa na wayahudi ambao alikua wakiishi Ujerumani kwa idadi kubwa.

Kwa kifupi Hitler aliamini Ujerumani ilishindwa Vita hiyo ya kwanza ya dunia kwa hujuma zilizofanywa na Wayahudi na alijiapiza kulipa kisasi atakapopata nafasi.
Nakweli Hitler alipopata nafasi ya kua kiongozi wa Ujeruman aliua maelfu kwa maelfu ya Wayahudi.
Aliua mamilioni na siyo maelfu kama ulivyosema.
 
hitler alikufa mwaka gani?
Kitu kama April au May 1945 kwa kujipiga risasi baada ya kuelezwa kwamba Ikulu yake ilikuwa imezungukwa na majeshi ya Russia na washirika.
Baadaye Ikulu ililengwa na kushambuliwa kwa makombora yaliyopondaponda maiti ya mheshimiwa hadi kutotambulika kabisa.
Kuna uvumi mwingi kuwa alitoroka, lakini hakuna uthibitisho wowote juu ya tuhuma hiyo.
 
Hitler na Wajerumani waliwashutumu Wayahudi wa Ujerumani kuwa walishirikiana na Wayahudi wa Marekani kuishawishi Marekani kuingia katika vita kuu ya kwanza ya Dunia kuungana na muingereza ili kuipigs Ujerumani kitendo kilichopelekea Ujerumani kushindwa katika vita ile. Baada ya mjerumani kupigwa ilipoteza makoloni yake yote na kuwekewa masharti magumu sana ya kijeshi na washindi, mambo hayo yalikuwa yanawauma Wajerumani.

Kitu kingine kinachofahamika ni kwamba Hitler mwenyewe ana vinasaba vya Kiyahudi lakini yeye alijiona Mjerumani zaidi
 
Kitu kama April au May 1945 kwa kujipiga risasi baada ya kuelezwa kwamba Ikulu yake ilikuwa imezungukwa na majeshi ya Russia na washirika.
Baadaye Ikulu ililengwa na kushambuliwa kwa makombora yaliyopondaponda maiti ya mheshimiwa hadi kutotambulika kabisa.
Kuna uvumi mwingi kuwa alitoroka, lakini hakuna uthibitisho wowote juu ya tuhuma hiyo.
Hitler alitoroka na kwenda kufia Poland.
 
facts_and_history-20180204-0006.jpg
 
Hitler ni moja ya madikteta maarufu kuwahi kutokea duniani.
Alizaliwa April 20 1889 nchini Austria karibu na mpaka wa Germany na Australia.
Sababu kuu ya kuwaua wayahudi ni baba yake Adolf Hitler ambaye anaitwa Alois Hitler alizaliwa katika mzingira ya aibu.
Maria Ana Mama yake Alois Hitler alibakwa na MTU mmoja Leopold kutoka familia ya kiyahudi ambako bibi yake Adolf Hitler ambaye ni mama yake baba yake alikuwa mtumishi wa ndani.
Baba yake Hitler alikuwa mtoto haramu lakini baadae alihalalishwa na viongozi wa dini..
Adolf Hitler baada ya kukua alipewa hiyo historia tangu hapo hakuwapenda wayahudi.
Aliwapa jina wasaliti.
Asante.
NB#Hitler ni jina la baba mlezi wa baba yake dictator hitler km unajua zaidi tiririka.


Naombeni mwenye kujua undani wa mauaji ya wayahudi kipindi cha Hitler naomba story ya Nazi Concentration Camps zile kama Sobobor, Ustwich etc

Na zile death gas chambers.



1. Baada ya Ujeeumani kushindwa Vita ya kwanza ya Dunia.
Kupitia mkataba wa Versaille treaty Ujerumani iliomba kujisalimisha.

Wawakilishi wa wayahudi matajiri waliitaka Uingereza iwape ardhi ya Palestina (Palestine Land)/iliokua chini ya umiliki wa Mwingereza.

(Ndio ardhi hii inayogombaniwa leo na wapakestina )

Ambapo Wayahudi waliahidiwa kupewa kama wangeshiriki vita dhidi ya Ottoman empire.


Kwenye vita ya kwanza wajerumani walishindwa vita na Uingereza.

Hitler alikua na kila sababu kuamini kua hiki kikundi cha wayahudi Matajiri ndio ndio kimewezesha kutoa Pesa na kuifadhili Uingereza kwenye vita dhidi ya ujerumani yake. Hata kufanya wakashindwa vita. Lawama zikawaangukia wayahudi kua ndio chanzo cha ujerumani kushindwa vita ya kwanza ya dunia(WW1).

Ambapo waliamini ujerumani haikupaswa kushindwa vita ile ya kwanza .ukichukulia kua Russia ilishaacha kupigana.

Mwaka 1933 wakati Hitler anakua Raisi, wayahudi walikusanyika sehemu mbalimbali ulimwenguni wakiandamana kupinga bidhaa kutokea ujerumani. Wakati ujerumani ilikua katika mdororo wa uchumi.

Na Kulikua na Gazeti limeandika "Judea Declares War On Germany

Anti-Nazi boycott of 1933 - Wikipedia.

Ukizingatia kua katika Ujerumani makali ya maisha hayakuwaathiri wayahudi kwakua wengi walikua matajiri. Ukilinganisha na wajerumani walio wengi walioumizwa na huu mdororo wa uchumi.


2. Kuanzia mwaka 1925 mpaka 1935 vyombo vya ujasusi vya Ujerumani vilikuja na ripoti ni jinsi gani Stalin wa Russia aliua mamilioni kwa kushirikiana na wayahudi kwenye chama chake hata kushinda Kule Russia. Hii hali ikawapa hofu wajerumani wakaona inaweza kutokea na kwao kama hawajachukua hatua stahiki mapema za kuwaangamiza wayahudi. Ikapelekea anti semitic propaganda kuenea kwa kasi zaidi.

3. Mawazo ya Ubaguzi wa Rangi.
Inadaiwa pia Hitler alikua anaaamini katika Dhana ya Race (Ubaguzi wa rangi). Hii kitu alikua aliihubiri sana majukwaani kwenye mikutano yake. Aliamini watu weupe wenye muonekano wa nordic. Ndio binadamu wenye thamani zaidi kustahili kuishi ujerumani. Wayahudi hawakua kitu zaidi ya kundi la wadudu katika mtazamo wake. akapanga kuwaondoa. Alitaka taifa lisilo na vilema wala aina ya ulemavu yaani purity. Alitaka Wajerumani warefu, wembamba, wenye miguu yenye nguvu, wenye nywele za blondy.

4. Ili ku wini mioyo ya wajerumani. Hitler alituma hisia za kufufua uzalendo na utaifa kama sehemu ya siasa za ujerumani ambayo ilikua imevunjika moyo kwa kushindwa vita.

Akizingatia kua kipindi hicho wayahudi walikua na nguvu sana katika Siasa za Ujerumani. Hitler akachagua njia ya kipekee akijua kua wayahudi ni asilimia moja 1% tu ya wajerumani wote.

Pamoja na uchache wa wayahudi lakini walikua wameshikilia sehemu kubwa ya uchumi wa wajerumani kwenye maeneo makubwa kama;-
tafiti za kisayansi(Scientific Research),
wayahudi ndio walikua wanashinda noble prizes mara zote.

Walikua wameshikilia Mfumo wa Pesa(Finance), ma banki na biashara kubwa kubwa
na pia kwenyw Ubunifu na uandishi.
Madaktari
Lawyers
Bankers


Hitler hakufurahia kuona 70% ya wajerumani ni maskini wakati idadi ndogo ya wayahudi ni matajiri sana.

Hitler akaamua kutengeneza imani fulani kua wayahudi ndio chanzo kikuu cha matatizo ya wajerumani wote.
 
Hitler ni moja ya madikteta maarufu kuwahi kutokea duniani.
Alizaliwa April 20 1889 nchini Austria karibu na mpaka wa Germany na Australia.
Sababu kuu ya kuwaua wayahudi ni baba yake Adolf Hitler ambaye anaitwa Alois Hitler alizaliwa katika mzingira ya aibu.
Maria Ana Mama yake Alois Hitler alibakwa na MTU mmoja Leopold kutoka familia ya kiyahudi ambako bibi yake Adolf Hitler ambaye ni mama yake baba yake alikuwa mtumishi wa ndani.
Baba yake Hitler alikuwa mtoto haramu lakini baadae alihalalishwa na viongozi wa dini..
Adolf Hitler baada ya kukua alipewa hiyo historia tangu hapo hakuwapenda wayahudi.
Aliwapa jina wasaliti.
Asante.
NB#Hitler ni jina la baba mlezi wa baba yake dictator hitler km unajua zaidi tiririka.

Kuna vyanzo vinasema Hitler alikua myahudi yeye mwenyewe.
Kutokananna historia yake.

Ambayo Mama ake hakuwahi kumwambia.

Wanasema pia chuki ya Hitler dhidi ya wayahudi ilijengeka baada ya bibi yake kufariki. Daktari anayeitwa Eduard Bloch aliekua akimtibu kansa ya matiti, alikua ni myahudi.

Dodoso zinadai Hitler alilelewa kwenye Familia tajiri ya myahudi. Kupitia hiyo Familia alikua akipata manyanyaso makubwa.
 
Mtoa mada sidhani kama upo sahihi sana. Hitler hakutaka kuwaua wa Israeli. Baada ya kuwa Cancellor wa Germany Hitler kutokana na chuki zake dhidi ya wayahudi aliazimia kuwaondoa Ulaya lakini sio kwa kuwaua, bali alianza kuwahamishia kwenda kisiwani Madagascar. Baada ya Hitler kuvamia Russia idadi ya Wayahudi iliongezeka na kuwa kubwa mno kwa sababu aliwakusanya Wayahudi wote aliowateka Ulaya pamoja na wale waliokua Russia. Kutokana na idadi hio kubwa mno Hitler alimpa kazi ya kutafuta solution ya tatizo ilo kwa msaidizi wake aliekua anaitwa Reinhard Heidrich. Huyu jamaa baada ya yeye kuona uwezekano wa kuwahamisha Wayahudi wote kwenda Madagascar hautawezekana kutokana na idadi yao ndio akaleta proposal ya kuwaua wote. Alipendekeza kujengwe concerntration camps kubwa ambazo Wayahudi watakua wanauwawa kwa kiwango kikubwa ndani ya mda mfupi (hii waliita 'Industrial scale murder'). Zilijengwa kambi sita(6) kwa ajili ya kazi hii kwenye maeneo ya siri huko Poland, kambi hizo ni kama Treblinka, Belzec, Sobibor na nyingine 3 kama hizi. Mwanzoni walitumia gesi ya carbonmonoxide kuua watu lakini haikuwa inafanya kazi kwa ufanisi ndio baadae ikaletwa gesi nyingine inaitwa Zyklon. Askari wa Kijerumani waliokua wanafanya kazi kwenye hizi kambi walikua wanauoga kiasi flani wakati wa kufanya hii kazi. Serikali ya Hitler kuona hivyo wakaamua kuleta askari kutoka Ukraine. Hawa jamaa ndio waliokua wanaifanya hii kazi vizuri kwa sababu inasemekana walikua ni makatili sana, kwa siku moja walikua wanauwawa takribani wayahudi 80,000.
Escape from SOBIBO
 
Back
Top Bottom