Kwa mujibu wa Historia ni kwamba kabla ya Vita ya kwanza ya Dunia, kulikua kuna idadi kubwa ya Wayahudi waishio Ujeruman.
Hitler alikua ni miongoni mwa wapiganaji wa kijerumani,ujerumani walishindwa katika vita hiyo. Sasa wakati inatangazwa kua Ujerumani imeshindwa vita Hitler yeye alikua amelazwa hospitali kwa matibabu ya majeruhi, basi aliposikia Ujerumani imepoteza vita yeye Hitler hakuamini kabisa eti Ujerumani imeshindwa vita kwani aliamini kua jeshi la Ujerumani lilikua Imara na nguvu mno na lisingeweza kushindwa kwa namna yoyote isipokua kwa kusalitiwa na wayahudi ambao alikua wakiishi Ujerumani kwa idadi kubwa.
Kwa kifupi Hitler aliamini Ujerumani ilishindwa Vita hiyo ya kwanza ya dunia kwa hujuma zilizofanywa na Wayahudi na alijiapiza kulipa kisasi atakapopata nafasi.
Nakweli Hitler alipopata nafasi ya kua kiongozi wa Ujeruman aliua maelfu kwa maelfu ya Wayahudi.