Hii ndio sababu Adolf Hitler aliuwa Wayahudi

Hii ndio sababu Adolf Hitler aliuwa Wayahudi

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,033
Hitler ni moja ya madikteta maarufu kuwahi kutokea duniani.
Alizaliwa April 20 1889 nchini Austria karibu na mpaka wa Germany na Australia.
Sababu kuu ya kuwaua wayahudi ni baba yake Adolf Hitler ambaye anaitwa Alois Hitler alizaliwa katika mzingira ya aibu.
Maria Ana Mama yake Alois Hitler alibakwa na MTU mmoja Leopold kutoka familia ya kiyahudi ambako bibi yake Adolf Hitler ambaye ni mama yake baba yake alikuwa mtumishi wa ndani.
Baba yake Hitler alikuwa mtoto haramu lakini baadae alihalalishwa na viongozi wa dini..
Adolf Hitler baada ya kukua alipewa hiyo historia tangu hapo hakuwapenda wayahudi.
Aliwapa jina wasaliti.
Asante.
NB#Hitler ni jina la baba mlezi wa baba yake dictator hitler km unajua zaidi tiririka.
 
Hapana sitaki upotoke na pia upotoshe watu, ni wapi huko ulikosoma au iman yako ipi inakuambia mtoto wa nje ya ndoa ni haramu?
Toa elimu mtoto unayempata kabla haujabariki ndoa ni mtoto halali au sio halali?
 
Nipe elimu...
Najua wewe ni muislam na unadhan kwamba uislam ndio unakuambia useme hivyo, je unajua maan ya aya hii katika quran?

Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).
 
Najua wewe ni muislam na unadhan kwamba uislam ndio unakuambia useme hivyo, je unajua maan ya aya hii katika quran?

Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).
Umesoma thread lakini?
 
Kwa mujibu wa Historia ni kwamba kabla ya Vita ya kwanza ya Dunia, kulikua kuna idadi kubwa ya Wayahudi waishio Ujeruman.

Hitler alikua ni miongoni mwa wapiganaji wa kijerumani,ujerumani walishindwa katika vita hiyo. Sasa wakati inatangazwa kua Ujerumani imeshindwa vita Hitler yeye alikua amelazwa hospitali kwa matibabu ya majeruhi, basi aliposikia Ujerumani imepoteza vita yeye Hitler hakuamini kabisa eti Ujerumani imeshindwa vita kwani aliamini kua jeshi la Ujerumani lilikua Imara na nguvu mno na lisingeweza kushindwa kwa namna yoyote isipokua kwa kusalitiwa na wayahudi ambao alikua wakiishi Ujerumani kwa idadi kubwa.

Kwa kifupi Hitler aliamini Ujerumani ilishindwa Vita hiyo ya kwanza ya dunia kwa hujuma zilizofanywa na Wayahudi na alijiapiza kulipa kisasi atakapopata nafasi.
Nakweli Hitler alipopata nafasi ya kua kiongozi wa Ujeruman aliua maelfu kwa maelfu ya Wayahudi.
 
Back
Top Bottom