Mkuu hivi huyo mnyonge kwa Tanzania ya leo ni nani?
Jamani tukubali tuu matabaka hata Enzi za mwalimu yalikuwepo. Hivi wewe unategemea apartment pale Kawe iuzwe bei gani? Personally I cannot afford it lakini hii mentality na lugha za uongo eti watanzania maskini na bla bla nyinginezo naona zinatuongopea. Mashirika ya umma ATC, Mwatex nk..yalikufa kwa sababu hizi hizi. Shirika likitaka litoe huduma zinazoendana na soko..lazima gharama zitumike. Ngoja ATC ifufuliwe upya...watanzania tutataka tulipe nauli ya Ngorika kwa sababu ni shirika la umma. Litakufa within no time!
Kuna watu nchi hii wana hela yao safi. They can afford. By the way umasikini usitufanye kumuona kila mtu ni fisadi. There are those who work hard and get their cash bila kumuibia yeyote. Sasa wewe ni mtumishi wa umma au mwalimu au muuguzi unataka apartment ya million 300! Hapo lazima uibe.
Kikubwa tujifunze kuelewa kwamba kipato kinazidiana. kesho tusipite barabarani ukaona Masanja au Mshana anaendesha Mercedes Benz ukasema ni fisadi. No! Lazima watanzania tubadilike hii mentality ya entitlement na kuamini kwamba we can be equal. It is wrong. Kila mtu apambane. atafanikiwa in his/her own right.