Hawa soko lao walitarget mafisadi wakati pesa za wizi zikiwa nje nje. Wafanyabiashara nao wakitengeneza faida kubwa kwa sababu walikuwa wakikwepa kodi. Kwa mtindo huo hata huyo Mkurugenzi wa NHC wanayemsifu sioni kama anastahili hizo sifa kama ameshindwa kuanalyze trend ya real estate market Tanzania. Kwa miaka hii ya uongozi wa Mh. Magufuli siyo rahisi kupata wateja wakutosha kununua hizo nyumba. Hivyo value ya investment ina depreciate with time. Hivyo kushindwa kuuza hizo nyumba kwa wakati maana yake ni kwamba payback period inaongezeka na hivyo kuongeza interest rate. Kwa maana nyingine ni investment yenye hasara tu. Wataalamu wetu ni shida tu. Kutofanya research au kutegemea research zilizofanywa miaka 10-20 iliyopita ndo utumie data zake kufanya investment matokeo yake ndo hayo. Hizo bei siyo affordable kwa wananchi wa hali ya kawaida.