Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Sio kweli mkuu, ni vile tu limekaa vinywani mwa watu but once u ask anyone to justify, hakuna anaeweza, lakini pia hilo limekaa kiutani zaidi na Mimi binafsi sioni tatizo katika hilo..
Sawa na kabila fulani kuitwa wezi vinywani mwa watu bila justification.
 
Nachoipendea iringa n mji uliopangika vizuri sana karibu kila mtaa una barabara ya kupitika magari na nyumb hazijajengwa kwa kubabana hata kuendeleza miundo mbinu mbalimbali inakua rahisi...Wale wenzangu wa mshindo mpo
Ebhana umetaja mshindo umenikumbusha home. Kuanzia kwa Mzee mambo, mama kayoka, Mzee asedi, Mzee Ngwada, kwa Mzee Ngezi, kalolo, maganga aaanh ntataja safu nzima ya mshindo at least nimeonesha tuko pamoja
 
Habari za jioni mabibi kwa mabwana,

Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa Iringa.

Kwa ufupi,

Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili. Mkoa wa Iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa Manispaa, Iringa Vijijini, Kilolo na Mufindi.

Katika elimu, mkoa wa Iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni;
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.

Shughuli za maendeleo, shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara.

Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k. Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za Kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watanzania changamkieni)

Mpaka sasa mkoa wa Iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni;
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM

Hivi karibuni Iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi, hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa, ambapo kwa sasa Kanda ya Ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.

Pamoja na mengine mengi.

Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia hongera sana ndugu zangu wana Iringa, ongezeni juhudi.

Asanteni sana.

Iringa town,
View attachment 399626View attachment 399627

View attachment 399628View attachment 399629View attachment 399630

View attachment 399632

View attachment 399634

View attachment 399635

View attachment 399636

View attachment 399637View attachment 399638View attachment 399639View attachment 399640
Iringa mji mzuri sana na uliotulia.
Bahati mbaya haujachangamka kama jirani na ndugu zao wa Mbeya.
Watu wake wakarimu na wazuri sana, lazima nitaoa huko.
 
Iringa ni mji mzuri huwa natamani Mara kwa Mara kurudi hata bila sababu
Nyumbani Iringa aisee ni kamji flani kasiko na bugdha ni katamu sanaaaaa.
Mitaa ya Kihesa Kilolo, Mkimbizi, Mwang'ingo, Semtema, Kihesa sokoni, Lugalo, Wilolesi, Ngome, mafifi, Gangilonga, Frelimo, Mshindo, Donbosco, mpaka zizi la Ng'ombe siku hizi.
Ukishusha kule chini Ipogolo kuna sekondari ya Tagamenda imejitenga ipo pembeni hivi niliwahi soma pale baada ya kutoka Highland nimeona kapicha pia ka Mafinga seminary nilisoma A level ni shule yenye mazingira bora kabisa.
Pako pouwa sana Vayawe Vanyalukolo Nyongise
 
Twilumba hilo mnyalukolo.
 
Nimeshuhudia live mbwa analiwa,babu yangu na wazee wenzake hukutana shambani bonde la ruaha,wanakula na kushushia na ulanzi,na mimi nilitaka kula siku moja,nikaacha!
Basi sawa.
 
Wenyeji wa Iringa mtuambie,kwanini majina ya maeneo mengi huko yanaanza na herufi 'i' kama ilivyo Iringa yenyewe.Baadhi ya maeneo ni haya:
Ismani,Ifunda,Ihemi,Itengulinyi,Idodi,Isupilo,Ilula,Isere,Ibumila,Izazi,Ipogolo,Ilembula n.k.
Duu yaani ni mengi balaa.Kama unayajua mengine,ongeza.
 
Umesahau sifa nyingine kwenye majina, Iringa ndio mkoa au mji ambao majina ya kigeni kwenye mitaa ni karibu hakuna, ukiondoa Frelimo na Donbosco. Jina lingine geni ni Pomern, kwingine kote ni I kwa kwenda mbele, igeleke, ilambilole, ikingilanyi,ipalamwa,ifupira,irambo,itimbo, ihimbo, nk

Sifa nyingine ni ukarimu kwa wageni, kama wewe unataka kuwekeza Iringa, basi wewe tafuta mtaji wako njoo. Kitu kingine kizuri kwa Iringa ni usalama nyakati za usiku, hata kama utatoka Miami Club usiku sana, mambo ya nondo hakuna. Halafu wana Mgahawa wao wa 24/7 pale kati unaitwa Baba Nusa, hata saa tisa usiku, msosi upo.

Iringa, hadi raha. Wale waleta raha mjini toka Ipogolo wamejengewa fly over safi kabisa.
 
Umenikumbusha baba nusa, hadi mwili umenisisimka kwa furaha. Niliingia mara ya mwisho 2008 nikiwa bado nasoma vidato. Bila kusahau sehemu ya V.I.P kweli baba nusa na balaaaa
 
Umenikumbusha baba nusa, hadi mwili umenisisimka kwa furaha. Niliingia mara ya mwisho 2008 nikiwa bado nasoma vidato. Bila kusahau sehemu ya V.I.P kweli baba nusa na balaaaa
Sasa hivi amekarabati, ina sura nzuri na ya kisasa. Kazi kwako. Kuna wakati alikuwa na branch pale Ilula, sijui bado ipo au ndio vile tena.
 
Back
Top Bottom