game over
JF-Expert Member
- Jan 1, 2016
- 10,387
- 23,298
Habari za jioni mabibi kwa mabwana,
Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa Iringa.
Kwa ufupi,
Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili. Mkoa wa Iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa Manispaa, Iringa Vijijini, Kilolo na Mufindi.
Katika elimu, mkoa wa Iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni;
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.
Shughuli za maendeleo, shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara.
Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k. Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za Kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watanzania changamkieni)
Mpaka sasa mkoa wa Iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni;
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM
Hivi karibuni Iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi, hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa, ambapo kwa sasa Kanda ya Ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.
Pamoja na mengine mengi.
Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia hongera sana ndugu zangu wana Iringa, ongezeni juhudi.
Asanteni sana.
Iringa town,