Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Naipenda Iringa, ndiyo mji mzuri na niupendao kuliko yote Tanzania, umesahau jiwe la Gangilonga nilishapanda mara nyingi tu hadi juu!

One love kwa masela wote pale Shooters downtown tulikuwa tunacheza billiards (polltables) na kushushia na bia bariiidi!

Long live Iringa, my home of Choice, Nitarudi Iringa Mungu akipenda!


1280px-Iringa.JPG

Huu mji uko vizuri sana. Hali ya hewa iko safi na hata watu wake kila mmoja ana mishe zake. Japo si mkaazi hapo lakini naamini ipo siku nitajenga kibanda changu hapo pawe makazi yangu rasmi. Kiufupi ni mji mzuri kwa kuishi. Shukrani mleta mada.
 
Huu mji uko vizuri sana. Hali ya hewa iko safi na hata watu wake kila mmoja ana mishe zake. Japo si mkaazi hapo lakini naamini ipo siku nitajenga kibanda changu hapo pawe makazi yangu rasmi. Kiufupi ni mji mzuri kwa kuishi. Shukrani mleta mada.
Kwakweli hali ya hewa ni safi sana mkuu, na sasa hivi hakuna maridi sana kama zamani nadhani ni kutokana na mabadiliko ya Tabia ya nchi, na pia mjini usafi wa mazingira hupewa kipaumbele sana na halmashauri pamoja na taasisi binafsi..
IMG_20170101_123420_799.JPG


IMG_20170101_123320_260.JPG
IMG_20170101_123238_867.JPG
tapatalk_1463305490066.jpeg
tapatalk_1463305548701.jpeg
IMG_20170101_123301_124.JPG
IMG_20160912_072310.jpg
FB_IMG_1481401942650.jpg
FB_IMG_1452506735184.jpg
 
Good job, kizalendo zaidi umeitangaza Iringa RC, Mkurugenzi, DC, kamati ya ulinzi na usalama na wadau wengine wakupe hongera hata ya kuchangia hapa umefanya juhudi kwani kutembea kona zote kupata picha hizi ni kujitoa tosha!
 
Habari za jioni mabibi kwa mabwana,

Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa Iringa.

Kwa ufupi,

Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili. Mkoa wa Iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa Manispaa, Iringa Vijijini, Kilolo na Mufindi.

Katika elimu, mkoa wa Iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni;
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.

Shughuli za maendeleo, shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara.

Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k. Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za Kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watanzania changamkieni)

Mpaka sasa mkoa wa Iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni;
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM

Hivi karibuni Iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi, hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa, ambapo kwa sasa Kanda ya Ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.

Pamoja na mengine mengi.

Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia hongera sana ndugu zangu wana Iringa, ongezeni juhudi.

Asanteni sana.

Iringa town,
View attachment 399626View attachment 399627

View attachment 399628View attachment 399629View attachment 399630

View attachment 399632

View attachment 399634

View attachment 399635

View attachment 399636

View attachment 399637View attachment 399638View attachment 399639View attachment 399640
Umenigusa mwe moyo
 
duh mkuu nimefurahishwa na mada yako ya kuipamba Iringa. Ni kweli ni mji mzuri sana na watu wake wakarimu sana niliwahi kukaa Iringa kwa mwaka mmoja napakumbuka sana
 
duh mkuu nimefurahishwa na mada yako ya kuipamba Iringa. Ni kweli ni mji mzuri sana na watu wake wakarimu sana niliwahi kukaa Iringa kwa mwaka mmoja napakumbuka sana
Asante, karibu sana tena mkuu..
 
kale kale kashughuri ka kula mbwa bado kanaendelea bado..!?
 
Back
Top Bottom