Yaani nikifika iringa lazima nikajipendelee pale mahali.Sasa hivi amekarabati, ina sura nzuri na ya kisasa. Kazi kwako. Kuna wakati alikuwa na branch pale Ilula, sijui bado ipo au ndio vile tena.

Thank u ..I will visit you HeartMimi pia ni makazi yangu sasa nina miaka 2...aaaah,I just love this town. Wakati nahamia huku kutoka dar nilipatwa na mawazo sana,sikujua kama ntaweza kuuzoea hii mji. Iringa kuzuri...karibuni sana ambao hamjawahi kufika ..
ipo ndege moja ya auricHata Dibo mwenyewe kapapenda nae pamempenda! Dar vurugu sana! Vipi uwanja wetu wa Nduli kuna traffic ya kutosha ya kujia ndege!
Daaahhh umenikumbusha huu mji..Habari za jioni mabibi kwa mabwana,
Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa Iringa.
Kwa ufupi,
Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili. Mkoa wa Iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa Manispaa, Iringa Vijijini, Kilolo na Mufindi.
Katika elimu, mkoa wa Iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni;
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.
Shughuli za maendeleo, shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara.
Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k. Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za Kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watanzania changamkieni)
Mpaka sasa mkoa wa Iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni;
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM
Hivi karibuni Iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi, hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa, ambapo kwa sasa Kanda ya Ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.
Pamoja na mengine mengi.
Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia hongera sana ndugu zangu wana Iringa, ongezeni juhudi.
Asanteni sana.
Iringa town,
View attachment 399626View attachment 399627
View attachment 399628View attachment 399629View attachment 399630
View attachment 399632
View attachment 399634
View attachment 399635
View attachment 399636
View attachment 399637View attachment 399638View attachment 399639View attachment 399640
Ni kwasababu tu kiongozi wa zamani (mkwawa) aliamua kujinyonga kuliko kukamatwa na mjerumani(aliona itakua dharau) ndo watu wamechukulia wabena wooote wanajinyonga tu...hujamaliza kuipamba vizuri vipi watu wake hehe pipo kwa ujumla,naomba kuuliza hivi ni kweli rate ya kujinyonga huko ni kubwa au ni story
Iringa kuna baridi ndio ila nadhani ilikuwa enzi zile. Baridi ipo kiasi chake kutegemeana na mtu kwani kuna wadau huvuna chai wakiwa na vesti tu maeneo ya Mafinga hali Mafinga huenda ndo ikawa sehemu ye baridi zaidi mkoani Iringa kwa sasa.Mh..IRINGA kuzuri aisee...ila naski baridi ndo KIBOKO yao
Ni kubwa sana ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini. Kwa mhehe asilia ukimuudhi ama akiumizwa na jambo haichukui sekunde kujitia kitanzi. Kwao ni kitu cha kawaida sana.hujamaliza kuipamba vizuri vipi watu wake hehe pipo kwa ujumla,naomba kuuliza hivi ni kweli rate ya kujinyonga huko ni kubwa au ni story
Very nice comment , and I wonder the government never mentioned Iringa in its priorities, and we are importing paper materials from south Africa, Lol.Iringa is the best of all towns in the country in terms of all sorts of productions whether agricultural, industrial or whatever but the goverment could have never seen this at all.
Kwenye miti tu ya mbao na karatasi unaweza toa maelf ya products kuanzia mbao, karatasi, viberiti, toothpicks, lami, umeme, nguzo za umeme; viwanda vingi vyaweza jengwa na kutoa ajira katika mashamba hayo hayo ya miti.