Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

wewe ulimponda makamba na kumsifu OBAMA kwa kigezo cha Obama kusoma HAVARD.
NKAKUPA mfano wa mtanzania wa havard CHENGE nkakutaka umlinganishe na MAKAMBA kwa kuwa chenge anautendaji wa muda mrefu sana serikalini na amekuwa mpaka AG.mAKAMBA miaka tano tu ni sawa na obama single term ya useneta aliokaa tena miaka nne.

wewe unadharau ndugu kisa hata skielewi...unaona mtu wa HAVARD kila mara yuko sawa unasahau uongozi hasa wa kisiasa ni karama.UNAWEZA KUWA NA CHEO KIKUBWA SANA KIJESHI AU SERIKALINI kisichotokana na siasa mfano😀irector wa TANAPA,NSSF,TISS,CDF ila tukakupa cheo kidogo tu cha kisiasa kikakushinda.Siasa is all about influencing mass/umma na sio sheria au mkono wa chuma kama ilivyo ndani ya idara za TISS au TPDF

MBOMA alipochukua fomu ya ubunge tulimwomba aachane nayo kwa maana siasa si sawa na ukuu wa majeshi...inaitaji a lot of maridhiano.

Kwa kifupi viongozi wana zaliwa na kuwa viongozi
 
Naona unataka kuleta Ligi zisizo na msingi sasa. Unabisha kuhusu uwezo wa messi, na maradona, kwani hao wanaowapa tuzo kila siku hawawaoni hao wachezaji 10 waliobaki?

Uwezo wake binafsi ndio umemfanya awe sehemu ya hiyo timu, waliobaki wote wanabuild up around him. kama unabisha kuhusu hili basi ubishi ni asili yako.sitaendelea tena na wewe, maana mifano usiyoielewa unatoa macho, unayoielewa unabisha bila sababu.

Kuhusu kuwa na watanzania wachache wenye calibre yake, ndio ukweli huo, kwani Tanzania kuna maraisi wangapi walio hai?si wako wa-4 tu?kuna former AU secretaries wangapi?Mmoja. Kuna astronauts wangapi?I know of only 1. So yes, if you are that good, it does not matter how big the population of a country is, what matters is qualified you are and how many individuals live up to the status of being that qualified.
wewe mapenzi yanakupofusha mkuu,

Sasa kama ni ishu ya uwezo binafsi, si aanzishe timu inaitwa MESI acheze mwenyewe nafasi zote toka golini na afunge, si anauwezo bwana, au huyu astronout si arushe roketi yake mwenyewe mpaka huko angani? mkuu unasikia unachokisema lakini??

ndio maana hata katika tuzo waungwana hawaachi kuwashukuru wenzao, kwa maana bila ya watu hakuna mtu,

Narudia tena, ni hatari sana kukaa chumbani kwako na kujiaminisha kua hakuna kama wewe, kuna wengine wengi tu zaidi yako, pia naamini katika watanzania 50 milion, kunao mahiga na zaidi yake kama 20 million, ni mgawanyo wa majukumu tu mkuu, ndio maana huoni wote tukifanya kazi moja, ushaona wapi watu wote ni marais? sio kwamba hakuna wenye uwezo wa kua rais, kwahiyo huyo aliekua rais ndio anauwezo kuliko wengine, hapana, ni katika ile hali ya kibinadamu tu kwamba hatuwezi fanya jambo moja wote kwa wakati mmoja hivyo tunateua mmoja atusaidie kufanya kwa niaba yetu.

Naamini kuna watu ambao they could have done better than him. na wapo hapa Tanzania, tena kule ndoombo meru,
 
hapa kweli ni lost cause.

Mie najaribu kukuonesha inteligence ya Obama as the deciding factor wewe unakuja kuleta hadithi za putin na orodha ndeefu.

Sasa mtu uzoefu hana, akili hana, uwezo hana (Makamba huyu) kwanini tumlazimishe wakati kuna watu wana-chek almost all the boxes na wako tayari kuifanya kazi?

Endeleeni kuchagua vichwa maji, wenye uzoefu wa mashaka ila wenye midomo mirefu na mipango hewa isiyokwisha. Mkiletewa siasa wakati wa utekelezaji msitujazie server hapa JF

Kama hiyo orodha ndefu hukuielewa si uulize? Uliza hawa ni akina nani? Lakini itakuwa ni uchovu tu maana google ipo na ndo utagundua contribution yao iko mbali zaidi ya Obama. Mimi nimewaangalia. Hawa ndo wameigeuza Dunia hakika na ni ukweli hawakusoma Harvard!

Jamani huyo Obama ndo kipimo chenu?
 
Hahahaha yaani huyu jamaa eti kuzima mapinduzi etc ndy anaona anafaa kuongoza nchi kwa akili hzi kweli kazi ipo mkuu
Mkuu hii ni ajabu sana, kama ni hivyo basi Mwamunyange awe rais, au yule Mwakibolwa ambaye kawazima m23 kule drc maana hiyo ndiyo a very recent achievement katika medani ya ulinzi na usalama.
 
Sera ya Ujamaa na kujitegemea, naweza kuijenga bila elimu sahihi? Hii siyo ile ya Mh. Deo Sanga mbunge wa Njombe aliyesemaa kujenga barabara na mitaro yake hakuhitaji degree?

Kupambana na Ujinga, Umaskini, Maradhi, Rushwa na Ufisadi, kweli hakuhitaji elimu? Unaongelea level gani mkuu?

Naomba geuza shingo yake uangalie nyuma, kisha ulinganishe na hapo ulipo uone namna ccm ilivyotufanya kwa kudharau elimu na wataalamu wetu!.

Baada ya hapa funga macho dk 2, na ukifungua, utafakari kama bado una msimamo wako wa kusema haya mahitaji hayajitaji elimu!.

Ccm ni shetani ambaye kazi yake ni kuiba, kuchinja na kuharibu. Na ndiyo maana kwa kudharau elimu na kudhalilisha wataalam wetu, taifa limeangamia!.

Hiyo filosofia kwa sasa Watanzania hatuihitaji!. Tunahitaji kila mtu kwa taaluma, na uwezo wake asimame kwenye eneo lake la kujidai. Hatutadharau taaluma wala elimu na kufanya siasa za kijinga kama za ccm ya Jk.

Kindly forgive me for my openness.


Ujamaa na kujitegemea na wale maadui watatu.
 
Mahiga, Dr kitine, pinda, membe, makamba wote wanatoka kule mjengoni k nyama pale .....kuna movie inatengenezwa hapa sijui kubwa la maadui Nani na starring Nani
 
Kama hiyo orodha ndefu hukuielewa si uulize? Uliza hawa ni akina nani? Lakini itakuwa ni uchovu tu maana google ipo na ndo utagundua contribution yao iko mbali zaidi ya Obama. Mimi nimewaangalia. Hawa ndo wameigeuza Dunia hakika na ni ukweli hawakusoma Harvard!

Jamani huyo Obama ndo kipimo chenu?

Nami naona ni ule ugonjwa wa kila mtu kuamini kwamba alichonacho basi hakuna mwingine. Aliyeko US na Obama wake. Aliyeko UK naye ana bingwa wake, n.k. Hatufiki hivyo! Hii tabia!
 
Thus why huwa nasema ukitaka kujua level ya ujinga na utumwa wa watanzania soma jamii forum. Utashangaa the way watu wazima walivyo na matumaini na baadhi ya wanasiasa, they are fighting because ya wanasiasa!!! Kuna watu 24 hrs ni wanashinda jamiiforum kushambuliana badala ya kufanya kazi, kila siku kulalamika umasikini! I wish turudi enzi zile siasa ilivyokuwa hailipi, ili nchi hii itulie, nawaonea huruma sana watanzania wenzangu ambao kimsingi washakuwa ni watumwa wa kifikra wa wanasiasa, yaani ni shidah!! Mbona europe hakuna mambo haya, siasa haina nguvu kama ilivyo kwetu waafrika, au ndo kuiga american model!
 
wewe kweli huna hoja.

Yani mover and shaker UN ya post 2010, unamuita nyakati imepita?nadhani una-refer tu Edward Lowassa, ambaye cheo cha maana ndani na nje ya Tanzania ni kuwa PM miaka 8 iliyopita.

Mahiga is what we call an all around figure. Well versed in Economics, development, policy, Intelligence,security, diplomacy and leadership.
On top of that ni msafi kushinda almost wote hapo CCM. Sababu pekee hafai kuwa Mgombea wa CCM ni kuwa he is overqualified in comparison to people he is running with. Sasa ukiweke kimtu kama kijanuari na Mahiga sijui kitakimbilia wapi. Wakati Januari experience yake ya UN kaipatia kambi ya wamkimbizi kama mfanyakazi, Mahiga has his kama UNHCR director Geneva, wakati Makamba experience yake ya international Diplomacy kaipata kwa kuongozana na Misafara ya JK kama speechwriter au mbeba mikoba, Huyu bwana playground yake ni UN securty council, ambako wanapimana nguvu na mijitu korofi kama Russia, China, US , EU ,wasomali n.k.., wakati January security clearance yake imegomea kwa naibu waziri,mwenzie was security clearance yake was presidential level enzi za Mwalimu wakati we had proper security,too high that his name was not even mentioned back in the Mwalimu days. Enzi hizo unahisi flani nae mwanausalama, sio sasa hivi hadi kina Slaa wanajitamba nusu ya TISS wana-report kwake.

Wakati vijitu kama vikina january vina uzoefu wa miaka isiyozidi mitano kwenye leadership position huyu bwana ana uzoefu as long as January's age.

The only reason he does not fit is he is bigger fit than his opponents.


Mzee najua uko very passionate na huyu POSH BOY MAHIGA lakini acha uwongo kuhusu January kukosa security clearence kuwa naibu waziri.
 
Sifa hana,
Sababu hayajui vizuri matatizo ya Watanzania.

Watanzania tusiingizwe mkenge kuchagua watu ambao hatuwajui na wao hawatujui! Tutaishia kuwa dissapointed kama kesi ya mama wa milioni kumi za mboga!
Makongoro anatosha. Hao wengine ni longolongo tu.
 
Thus why huwa nasema ukitaka kujua level ya ujinga na utumwa wa watanzania soma jamii forum. Utashangaa the way watu wazima walivyo na matumaini na baadhi ya wanasiasa, they are fighting because ya wanasiasa!!! Kuna watu 24 hrs ni wanashinda jamiiforum kushambuliana badala ya kufanya kazi, kila siku kulalamika umasikini! I wish turudi enzi zile siasa ilivyokuwa hailipi, ili nchi hii itulie, nawaonea huruma sana watanzania wenzangu ambao kimsingi washakuwa ni watumwa wa kifikra wa wanasiasa, yaani ni shidah!! Mbona europe hakuna mambo haya, siasa haina nguvu kama ilivyo kwetu waafrika, au ndo kuiga american model!
tuambie baada ya kufanya kazi umenyanyua uchumi kiasi gani???
ulaya siasa haina nguvu kakudanganya nani???juzi kikwete alikataliwa kuingia denmark kwa sababu za uchaguzi

hata tufanye kazi vipi kama siasa ni mmbovu hamna maendeleo.siasa ni maendeleo, siasa hutoa tumaini na fursa
hapa mimi kila nkiwaona TRA nafunga duka kisa staki kulipa kodi, kodi kwa maendeleo ya nchi au nenepesha matumbo ya watawala????
 
Watanzania tusiingizwe mkenge kuchagua watu ambao hatuwajui na wao hawatujui! Tutaishia kuwa dissapointed kama kesi ya mama wa milioni kumi za mboga!
Makongoro anatosha. Hao wengine ni longolongo tu.
u r appreciated ndugu,MAKO tunamjua anatufaa
ni bora FISADI LOWASSA kuliko zimwi tusilolijua MAHIGA
 
kama walivyo 95% ya mabalozi na maofisa wa ngazi za juu wa serikali ya tanzania huyu hajui shida ni nini na watu wenye shida wanaishi vipi

huyu ndio wale wanaitwa the have lots na familia yake na mkewe wote ndio katika hiyo hiyo circus ya wanaoishi kwenye ivory towers. Marafiki zake kisirisiri wanamwita posh boy mahiga....

Huyu alikuwa anapigiwa kampeni na mmoja wa wagombea urais ili awe bosi wa usalama lakini hawakufanikiwa na mheshimiwa rais akamteua mtu mwingine (ambaye akina mahiga waliendelea kumpiga vijembe na articles zao kwa kutumia pseudo names kwenye media tanzania).

Mkewe ni mbunge janeth mbene, watoto wake wamesoma shule za international schools na hawajui kiswahili vizuri), mtoto wake mwingine wa kufikia ndio pr director wa nssf.

Huyu anajua zaidi mitaa ya upper east side of newyork kuliko kariakoo, ruvu, kigoma, tabora, mwambani na visiga

huyu anajua zaidi tena kwa kichwa north delegates lounge bar kuliko kwa macheni aubreak point (sidhani hataka anazijua)

cliques zake tanzania ndio hao hao ma diplomats wenzake waliozaliwa na silver spoon kuliko hao wenyeviti wa serikali za mitaa.

Ukimuuliza bei ya nyanya tanzania hajui lakini anaspend close to $700 kununua tai moja kwenye department store la kifahari la bergdorfgoodman (hili liko mtaa wa 5 avenue ambao umejaa maduka yenye kuuza vitu ghali zaidi duniani). Huyu mahiga suti zake ni bespoke za ermenegilo zegna, kiton k-50 anashindana na yule bepari mwingine (ami mpungwe). As a matter of fact huyo jk na kupiga pamba zake zote lakini bado hamfikii huyu jamaa ambaye juzi tumeshangaa kavaa shati la kijani ( naamini haya hilo shati la kijani la ccm alilovaa ni litakuwa limekuwa designed na hao hao jamaa zake wa 5th avenue)

mahiga anaweza kuwa ana uwezo wa kuongea na hao madiplomats na hao watu wa matawi ya juu wenzake lakini sidhani kama yeye na familia yake na marafiki zake na mnaompigia debe humu jamii forums mnaweza kutushawishi kuwa ni mtu ambaye yuko in touch na watazanaia waliopo on the ground

nina wasi wasi kama aliwahi kufika ofisi za ccm kariakoo na ukimuuliza klabu gani ilishinda upingwa wa ligi kuu mwaka jana sidhani kama anajua.

Ila ingekuwa yule binti yake mlokole ( modesta) anagombea tungemfikiria lakini kwanza aanze na level ya udiwani kumpima lakini si baba mtu ambaye najua fika kuwa mjumbe wa nyumba 10 hawezi kupita.

Kma ni mchezaji basi sioni tofauti yake na pascal cygan na eric djemba djemba. Tanzania na hasa ccm tunataka wachezaji wenye calibre ya thiery henry, ray parlour, patric vieira na roy keane na sio huyu mchezaji ambaye hata first 30 ya ujenzi rukwa hapewi namba.


Tazama video za watoto wake.








janeth.jpg


mkewe (janeth mbene)


nasema hivi

hawa watu bora wake tuu na pesa zao na connections zao lakini kwenye chama hatuwataki kwa sababu hawafanani na sisi kwa lolote lile.



hivi janeth mbene ni mkewe au mzazi mwenzake .....maana juzi katokea na mwanamke mwingine kama mkewe ....nadhani mleta hoja weka hoja vizuri
 
Last edited by a moderator:
Thus why huwa nasema ukitaka kujua level ya ujinga na utumwa wa watanzania soma jamii forum. Utashangaa the way watu wazima walivyo na matumaini na baadhi ya wanasiasa, they are fighting because ya wanasiasa!!! Kuna watu 24 hrs ni wanashinda jamiiforum kushambuliana badala ya kufanya kazi, kila siku kulalamika umasikini! I wish turudi enzi zile siasa ilivyokuwa hailipi, ili nchi hii itulie, nawaonea huruma sana watanzania wenzangu ambao kimsingi washakuwa ni watumwa wa kifikra wa wanasiasa, yaani ni shidah!! Mbona europe hakuna mambo haya, siasa haina nguvu kama ilivyo kwetu waafrika, au ndo kuiga american model!
Sawa mkuuza uchumi wa nchi wewe
 
Back
Top Bottom