Hii kwako unaichukuliaje?

Hii kwako unaichukuliaje?

Sawa mkuu maswali yako yanafikirisha lakini kumbuka aalipokuwa nyumbani kama mwao ulimwekea full controll ukiwa kama mzazi na mlezi., Lakini ulipomuoza kwa Mwanaume manake ulimtoa katika controll zako na kuhamishia Mandate kwa mumewe, Hivyo huko lazima afuate taratibu chini ya mumewe.

Suala la kumsomesha halipaswi kuwa sababu kwa vile hata usingemsomesha lazima ingefika umri flani angeolewa na kwenda kwa mumewe. Vinginevyo useme hakupi misaada ya kiuchumi toka katika kipato chake cha mshahara ilihali wewe ndiye ulimsomesha, hakika hapo atakua anakukosea pakubwa ila sio suala la ruhusa ya kuja mzazi, Sidhani kama hata wewe ungependa mkeo awe anajiondokea tu kwenda kwa wazazik wake kwa vile tu walimsomesha!

Kiufupi kila nyumba ina mkuu wake na taratibu zake ambazo kila mmoja hutakiwa kuziheshimu!
 
Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa.

Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.

Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.

Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?​

Sio mtu Baki labda kama hujui maana ya "Mume"

Mke akishaolewa anakuwa kwenye ufalme mwingine, Oda zote anapokea Kwa Mume wake sio mtu mwingine.

Mume anauwezo wa kuzuia mke asiende kwao kusalimia Kama akitaka.
Lakini Kwa busara na kuendeleza mahusiano mazuri ya kindugu Kama familia zinazojitegemea ndio inashauriwa angalau Kwa mwaka mara moja mnaenda kusalimia nyumbani Kama mnaishi mbalimbali.

Kama ni mji huohuo basi inawezekana kadiri ya mpatapo nafasi.

Kumsomesha mtoto haimaanishi utaingia katika utawala na mamlaka yake.

Ni Sawa Uhuru Kenyatta alivyomsaidia Raila odinga alafu odinga akashinda, haimaanishi Kenyatta anayomamlaka ya kumuingilia odinga kisa alimsaidia.
 
Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa.

Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.

Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.

Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?​
Labda nikusaidie naona unazunguka zinguka tu, ulitakiwa uulize ni nini maana ya send off?
 
Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?
Si ulichukua mahari!!!?
Wakija kuazima ile mahari waliyokupa utawapa?
 
Nadhani sisi ndo tumefungwa na mila na desturi !! Pia ubabe ni mwingi ! Ila ile mama ndani kuomba ruhusa sio vibaya na hazuiliwi ile ni njia ya kutoa taarifa au kuaga anakoenda ili hata akipata shida sehemu unaelewa , vile vile kwa mume akiwa anaondoka lazima aseme au aage (ndo kuomba ruhusa huku) Mama atashindwa kuondoka ikiwa ratiba za nyumbani haziko sawa au majukumu ni mengi !!!

Kwa hivyo Baba au Mama akitaka kutoka lazima aseme anakoenda ndo kuomba ruhusa indirect kwa watu waliostaarabika.

Hapa hatuzungumzii kina aisha miuno feni ,sijui mamu mtamu ! Maana hawa watoto wa kiswahili ukileta ustaarabu hawakatiki kwenda kwao kila siku shughuli , mara kumtoa mwali 😃😃😃
 
KASHAOLEWA YUPO CHINI YA UANGALIZI MWINGINE NA MAMLAKA MENGINE (KAMA AMBAVYO ULIKUBALI KUMUOZESHA)

HAWEZI KUTOKA KIENYEJI ENYEJI TU MKUU, LAZIMA AOMBE RUHUSA KWA MUMEWE

Wewe hapo ulipo naamini wife wako hawezi akajitokea tu bila ruhusa na bila kutoa taarifa..akifanya hivyo tunaita ni dharau na kutomtii mume
Kwa mtazamo huo, Ina maana ile mahari uliyoipokea, ndio iliotumika kama kumuuza binti kwa mumewe?
 
Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa. Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.

Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.

Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?​
Kwanza rekebisha hilo neno la "mtu baki". Mkweo sio mtu baki, mwenyewe anakuita baba mkwe au mama mkwe, ni mzazi wake, babu/bibi wa wanae.
Pili, siamini kuwa watu walioko katika ndoa huwa wanaombana ruhusa kwenda kuwasalimia wazazi wao. Naamini kuwa kama wanaishi mbali nao, huwa wanapanga pamoja na kukubaliana ratiba na mambo mengine yanayohusu ziara hiyo. Kama wanaishi karibu wanataarifiana tu kuwa napitia hapa kwa baba mara moja, poa.
 
Nitaichukulia kawaida tu kwa sababu;
1. Hayo hayajaanzia kwangu. Hata wewe, kama ni baba mkeo anaomba ruhusa kwenda kuwasalimu wazazi wake, au kama ni mama nawe unaomba ruhusa kwa mumeo kwenda kuwasalimu wazazi wako.
2. Kutimiza majukumu yako kwa mtoto wako wa kike wakati akiwa bado hajaolewa, hakupori nafasi ya mumewe kwake. Huwezi kuwa baba au mama kwa mtoto wako at the same time uwe mume wake kinafasi
3. Embu waza ukuaji wa mtoto wako. Kila hatua kuna vitu unaacha kumfanyia, anavifanya mwenyewe au mumewe. Mwanzo mlimuogesha, kumnunulia hiki na kile au kumlea kwa ujumla. Mnapomuozesha, hii maana yake yaliyo mengi yatafanywa na mumewe, LIKIWEMO NA KUMRUHUSU KUJA KUWASALIMIA
 
Kwanza rekebisha hilo neno la "mtu baki". Mkweo sio mtu baki, mwenyewe anakuita baba mkwe au mama mkwe, ni mzazi wake, babu/bibi wa wanae.
Pili, siamini kuwa watu walioko katika ndoa huwa wanaombana ruhusa kwenda kuwasalimia wazazi wao. Naamini kuwa kama wanaishi mbali nao, huwa wanapanga pamoja na kukubaliana ratiba na mambo mengine yanayohusu ziara hiyo. Kama wanaishi karibu wanataarifiana tu kuwa napitia hapa kwa baba mara moja, poa.
NaNUKUU..... napitia hapa kwa baba mara moja... mwisho wa kunukuu...!! NDIYO RUHUSA YENYEWE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom