Hii kwako unaichukuliaje?

Hii kwako unaichukuliaje?

Umepambana kumlea na kumsomesha mtoto wako wa kike, mpaka akafikia hatua fulani ya elimu; iwe cheti, diploma, degree, masters, PhD, au u-profesa. Baada ya hapo, akaolewa na akawa na mji wake.

Changamoto: Leo hii unataka binti yako aje akusalimie nyumbani; itamlazimu mpaka aombe ruhusa kwa mumewe, na amruhusu, ndio aweze kufika, asiporuhusiwa hatokuja kukujulia hali.

Swali: Hii kwako unaichukuliaje, ukiangalia wewe ndio mzazi, uliyemlea na kumgharamikia elimu; lakini cha ajabu, leo mtu baki ndio anayempangia aje akuone ama asije kukuona?​
Zingatia maandiko ukiona unaumia au utaumia basi usimruhusu kuolewa, mbona rahisi tu hiyo na ukubali kulea wajukuu hapo kwako.
 
Tupe maana
Kama hujui maana ya send-off maana yake hata maana ya kitchen party hujui.

Kuolewa siyo lazima, usikubali kuolewa kama unataka uhuru wako kamili

Kwanza ndowa haitaki debate kila kitu unataka haki huwezi kukaa kwenye ndoa, nakushauri tafuta baharia sperm donor akupe mtoto tu mambo ya ndoa waachie wengine wewe huna upako huo.
 
Ikitokea binti yako amezuiwa na mumewe kuja kukuona, utamfanyaje?
 
Kwa mfano akienda bila kutoa taarifa, utamfanyaje?
Kama haiingilii ratiba yetu yoyote anaweza kwenda tu, naamini ataniletea salamu za wazazi. Mfano mnaishi Kimara na wakwe zako wako wanaishi hapo Ubungo na mkeo anafanya kazi City Center, anaweza kupitia atokapo kazini na kuniletea salamu zao, na ikawa poa tu.
 
Ina maana hutokuwa na cha kufanya, zaidi ya kupokea ujumbe wa huko alikotoka ?
 
Ikitokea binti yako amezuiwa na mumewe kuja kukuona, utamfanyaje?
Huo sasa ni ugomvi maana huyo mkwe ni mwanangu pia. Kumkataza mkewe asinisalimie ni sawa na kwamba yeye mwenyewe mkwe hataki kunisalimia. Hilo linapaswa kushughulikiwa kama mgogoro.
 
Kwa mfano akienda bila kutoa taarifa, utamfanyaje?
Umeshasikia watu wanapigwa kwenye ndoa na mzazi huwezi mfanya kitu mumewe..!?? Hivi kwenye jamii yetu hii, mzazi umekusanywa na wazee halafu mnajadili kesi ya mwanao anakimbilia kwako kila siku bila ruhusa, unadhani kuna mzee atakuelewa?

NIKUPE KISA HIKI CHA KWELI ILA MAJINA NITAYATUMIA TOFAUTI NA YA UKWELI
Kuna jamaa (Tumuite John) alikuwa anaishi kurasini kule maeneo ya WAPO radio. Wakati huo ametoka tu kumaliza tu shule, akapata kazi bandarini, kwenye kampuni mojawapo inayotoa huduma kwa Bandari. Baada ya muda fulani, akampata mdada ametoka tu kumaliza form six. Mdada huyo alikuwa anakaa maeneo hayo hayo kwa wazazi wake. Jamaa akaanza kunyandua demu huyo. Mwisho wa siku akajitambulisha kwao na akaowa ndoa ya kanisani (KKKT). Wakati wameanza kuishi pamoja, kutoelewa kwa mara kwa kukawa kunatokea. Mwanamke akipandwa na hasira ANAKIMBILIA KWA WAZAZI WAKE, HATA IWE USIKU WA MANANE. Bahati mbaya, anaweza akakaa huko hata wiki na mwisho jamaa anaamua kwenda kumfuata. Tabio hiyo John ikawa inamkera sana. Akaona inawezekana sababu ya ukaribu uliopo kwa maana ya umbali toka wanapoishi hadi kwa wazazi wa mwanamke. Na bahati mbaya, wazazi wake mtoto akikimbilia kwao wanampa maneno ya kumvimbisha kichwa. Kama vile chumba chako bado kipo, hapa kwenu hujauwa.. etc

John akaona isiwe tabu, akaamua kuhamia MABIBO. wakahama wote. Tabia ile baadaye ikapungua kidogo, hasa ile ya kutoroka usiku. Lakini mwanamke alikuwa anasubiria kukuche then anasepa. Mara ya mwisho, bwana John akaona huu ni ujinga, akaamua kupiga kimya. Hakumfuata. Mwezi ukakatika. Wazee wenzie na baba wa mwanamke wakaona hii si sawa. Wakamfuata mzee mwenzao na kumsema sana.

Mwisho wa siku baba akawa anamgeuka mwanae. Akiingia tu home, baba anamtimulia huko huko. Ndo hapo ndoa ikakaa sawa, kukawa hakuna tena kutorokea kwa wazazi

PIGA UA, UKISHAOZESHA UHURU WAKO KWA MWANAO UNAKUWA WA MIPAKA, KAMA ALIYOKUWA NAYO MUMEWE WAKATI HAJAMUOA.
 
Huo sasa ni ugomvi maana huyo mkwe ni mwanangu pia. Kumkataza mkewe asinisalimie ni sawa na kwamba yeye mwenyewe mkwe hataki kunisalimia. Hilo linapaswa kushughulikiwa kama mgogoro.
Sasa, hapo ndipo unarudi kwenye mada husika
 
mzazi kumlea kumsomesha mtoto ni wajibu sio ombi ila mtoto sio wajibu wake kukulea ww ulikua wapi kutafuta mali zako uje utoe macho uzeeni kweny mali ya mtoto wako
 
Ina maana hutokuwa na cha kufanya, zaidi ya kupokea ujumbe wa huko alikotoka ?
Ujumbe gani tena. Mtu akiniambia "nimepita kwa baba, hawajambo wanakusalimu", kuna nini cha ziada? Na tena siku hizi kuna simu, anaweza kunipigia hata akiwa nao "Baba T niko hapa kwa baba nimepitia mara moja kuwaona, hawajambo", nami nitaomba hiyo simu niwasabahi. Shida iko wapi?
 
kwa hiyo mkuu, Mahari ni sawa na kumuuza binti?
Tunajipaga imani tu kwamba si kumuuza..!! In reality ndo hivyo..!! Kama kununua chochote unafanya negotiations kama unazofanya wakati wa kukubaliana mahali, then what is the difference?
KIFUPI TUNACHOKIFANYA KWENYE KULIPANA MAHALI NI KUWA WE HAVE DECIDED TO CALL A SPOON A SPADE
 
mzazi kumlea kumsomesha mtoto ni wajibu sio ombi ila mtoto sio wajibu wake kukulea ww ulikua wapi kutafuta mali zako uje utoe macho uzeeni kweny mali ya mtoto wako
Hujafa hujaumbika. Unaweza kuwa na bilioni 10 benki lakini huna uwezo wa kwenda kwenye ATM kuchukua elfu 10 ya kununulia maziwa (unaumwa miguu, mgongo, kiuno, huoni vizuri au una dementia)
 
Tunajipaga imani tu kwamba si kumuuza..!! In reality ndo hivyo..!! Kama kununua chochote unafanya negotiations kama unazofanya wakati wa kukubaliana mahali, then what is the difference?
KIFUPI TUNACHOKIFANYA KWENYE KULIPANA MAHALI NI KUWA WE HAVE DECIDED TO CALL A SPOON A SPADE
Suluhisho hapa ni kutokupokea mahari ili binti awe huru anapokuwa kwenye ndoa
 
Ikitokea binti yako amezuiwa na mumewe kuja kukuona, utamfanyaje?
Hakuna mwanaume mwenye akili timamu atamzuia mtoto kwenda kusalimia kwao, lakini hizi ndoa za binti kwao ubungo halafu kaolewa kimara zina matatizo sana, mabinti wanajisahau kama wameolewa mara kwa mara wanataka wakapige story na mama zao kitu ambacho si sahihi na hakuna mwanaume yeyote anaweza kukubaliana na upumbavu huo.
 
Zingatia maandiko ukiona unaumia au utaumia basi usimruhusu kuolewa, mbona rahisi tu hiyo na ukubali kulea wajukuu hapo kwako.
Na asipomruhusu kuolewa, WANANZEGO TUTAYASEMA YETU.. bingwa anakula kuku na mayai yake. Na hasa kama kila akiletwa mchumba kutambulishwa mwamba anakaba hadi penati..!!

Namfahamu binti hajaolewa hadi leo kisa baba yake alikuwa swala tano na binti amewaleta nyumbani wachumba wa kikristo wanne kwa nyakati tofauti. Mwamba akawapiga chini wote. Cha ajabu baba akaachana na mama wa binti kwa mambo yao HALAFU AKAJA KUOA MKRISTO. Mdada hakumpenda baba yake hadi hadi baba anakufa. And unfortunately, binti ana watoto watatu yupo nao kwake kapanga vyumba vitatu
 
Hujafa hujaumbika. Unaweza kuwa na bilioni 10 benki lakini huna uwezo wa kwenda kwenye ATM kuchukua elfu 10 ya kununulia maziwa (unaumwa miguu, mgongo, kiuno, huoni vizuri au una dementia)
Mada inafikirisha sana
 
Suluhisho hapa ni kutokupokea mahari ili binti awe huru anapokuwa kwenye ndoa
Usiadhani mahari ndo inatoa mandate kwa mume kuwa mume. Ni ile hali ya wewe kusema nenda kaishi naye, full stop. Otherwise tungekuwa na fixed figure ya mahali. Ndiyo maana kuolewa, mahali inaanzia 0 hadi mamilioni ya fedha, lakini mume atapewa nafasi ile ile regardless of the amount ya mahali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom