Hii kesi hii sijui kama anaweza chomoka!?

Hii kesi hii sijui kama anaweza chomoka!?

Usilolijua ni tafsiri rasmi ya maneno hayo na tafsiri rasmi ya uahini.
Pili kuipinga serikali au kupinga au kuzuia uchaguzi siyo kosa kwenye mfumo wa vyama vingi

Nadhani umeshuhudia maelezo ya shahidi Mahamba aliyoandika mwenyewe akijaribu kugoma yasitumike mahakamani kama ushahidi, lakini baada ya TAL na majaji kumkomalia akawa hana namna akakubali. Je! Hapo umejifunza nini??????
Ni kweli Kupinga sio kosa.

Ila vurugu za kuchoma Mali za watu ni kosa la Ugaidi kwa sheria za TZ.

Ww leo hii ukienda kuchoma Sheli au soko. Unashtakiwa kwa ugaidi.

Sasa je Maneno yake ya April 2025 yalisababisha watu wahamasike na kuvuruga uchaguzi kwa kuchoma mali?.

Hili ndio mawakili wa serikali wanajaribu kuingiza hili kwenye hii kesi.
 
Tume ya Jaji Chande ilisema sababu za vurugu. Na moja ya sababu ni maneno ya wanasiasa na wanaharakati.

Kakamatwa miez 6 kabla ya Uchaguzi. Sasa Huyu ACP Mahimba ndio anataka kutoa ushahidi wa maandishi kuonyesha ni kias gan maneno ya Lissu yalihamasisha watu kufanya vurugu.

Kumbuka watu kadha wa kadha walikamatwa na wakaandika maelezo. Na baadae Raisi aliwasamehe.
Yale maelezo ni ushahidi.
Kama kwa namna yoyote waliaema wamehamasika na maneno ya Lissu ya April 2025. Kesi ni ngumu.

Hakuna ugumu wowote hapo kwa mujibu wa shtaka linahusu uhaini.
Maelezo yanahusu kuvuruga uchaguzi.

Hao waliokamatwa kisha kuachiwa walikamatwa kwa kesi ya uhaini au kuleta vurugu kwenye uchaguzi?

Kuzuia uchaguzi sio uhaini.
Kuzuuia kiongozi wa siasa asitangazwe sio uhaini.
 
Aliwahamadisha watu mapema mwezi Aprili nao wakatenda akiwa jela

Kwani kesi yake kwa sasa ni ipi?
Kesi yake ni kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi, na kuleta vurugu au uhaini?

Kusema utazuia uchaguzi bila kutaja namna utakavyozuia, ukawekwa jela zaidi ya miezi sita ikapita, kwenye uchaguzi kukatokea vurugu ukiwa jela, unahusikaje na kuzuia na kuleta vurugu kwenye uchaguzi unahusikaje?
Kuna viongozi wengi na watu wengi walikuwa wakisema watazuia uchaguzi kama hakutakuwa na reforms kwa nini wao wasikamatwe akamatwe Tundu Lisu?

Mahakama inauwezo upi wa kupima ushawishi wa watu hasa wanasiasa katika kauli zao?
 
Mkuu hujui kiongozi akitamka neno,haraka utekelezaji huanza pengine hata bila yeye kutambua!....
(Underground work huanza mara moja zinazo husu utekelezaji)

Hizo zilikuwa siasa tuu.

Yupo yule aliyesema polisi wasitafute wanaopotea kwani yeye(wao) ndio wanakuwa wanafanya kazi hizo.

Na watu wengi walipotea. Unafikiri kwa nini hakukamatwa?
 
Hakuna ugumu wowote hapo kwa mujibu wa shtaka linahusu uhaini.
Maelezo yanahusu kuvuruga uchaguzi.

Hao waliokamatwa kisha kuachiwa walikamatwa kwa kesi ya uhaini au kuleta vurugu kwenye uchaguzi?

Kuzuia uchaguzi sio uhaini.
Kuzuuia kiongozi wa siasa asitangazwe sio uhaini.

Kuna mstari mwembamba sana unatenganisha hapa. Na mara nying watu hawauoni au kuchanganya.

Uhaini maana yake ni Usaliti.
Usaliti wa Serikali ya nchi yako unayoishi.

Kuzuia uchaguzi sio Kosa la Uhaini.
Lakini unazuiaje huo uchaguzi?.

Kwamfano ukisema Jaman msiende kupiga kura, sio kosa la kiuhaini.
Ila ukifanyia watu fujo wasiende kupiga kura ni kosa.

Kwahiyo hapa inaangalia matendo sio maneno.

Mfano Niffer alikamatwa sio kwasababu aliwaambia tu watu wasiende kupiga kura.
Bali Alihamasisha watu kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawazuie watu wasiende kupiga kura.
Akawahamasisha watu wanunue mask ili mabomu ya machozi yasiwadhuru. Akahamasisha watu wabebe maji.

alaf siku ya uchaguzi. Kukatokea vurugu . Hata kama Niffer hakuwa eneo la tukio. Bado yeye ni mshtakiwa kwa sababu alikuwa na nia na amehamasisha watu kufanya kosa.

Kama angehamasisha (maneno) na vurugu zisingefanyika alikuwa hana kosa.
Ila vurugu (matendo) zilifanyika. Na ndio maana alikamatwa.

Na kosa lake likawekwa kama uhaini maana anasaliti serikali unayotakiwa Kuwekwa kwa mujibu wa kisheria.
 
Kwani kesi yake kwa sasa ni ipi?
Kesi yake ni kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi, na kuleta vurugu au uhaini?

Kusema utazuia uchaguzi bila kutaja namna utakavyozuia, ukawekwa jela zaidi ya miezi sita ikapita, kwenye uchaguzi kukatokea vurugu ukiwa jela, unahusikaje na kuzuia na kuleta vurugu kwenye uchaguzi unahusikaje?
Kuna viongozi wengi na watu wengi walikuwa wakisema watazuia uchaguzi kama hakutakuwa na reforms kwa nini wao wasikamatwe akamatwe Tundu Lisu?

Mahakama inauwezo upi wa kupima ushawishi wa watu hasa wanasiasa katika kauli zao?

Hati ya Mashtaka ya Lissu inasema hili ndio shata linalomkabili.

"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya".

Je unadhani Mawakili wakionganisha haya ya April na vurugu za Mo29 wanakosea?.
 
Kumbuka hayo maneno yanadaiwa kutolewa kupitia Chombo cha habari cha Jambo TV. Flash iliyobeba maneno hayo kama huna habari Mahakama ilikataa kuyapokea kama kielelezo. Kwa ufupi hayo maneno hayapo mahakamani.
Nipo hapa kwa ajili ya kujifunza, ni kwanini Mahakama ilikataa maneno hayo kutoka kwenye hiyo flash?

Pia ikiwa Lissu aliwekwa gerezani kabla ya uchaguzi miezi kadhaa kabla ya ule uchaguzi na hadi wakati wa uchaguzi alikuwa chini ya magereza, Je uhalali wake na uhusika wa yaliyotokea siku ya uchaguzi unatokea wapi?
 
Hii ngoma imefikia patamu, leo lissu alikuwa anatia huruma, mpaka alitamani amzibe mdomo shahidi wa mashtaka
Ccm kuna vilaza sana , kwamba hajui kwamba mahakamani kuna lugha za kutumia sio pa kuropoka , kuna lugha na mnyumbuliko unaotakiwa kutumika ukiwa mahakamani
 
Hati ya Mashtaka ya Lissu inasema hili ndio shata linalomkabili.

"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya".

Je unadhani Mawakili wakionganisha haya ya April na vurugu za Mo29 wanakosea?.
Nipo hapa kwa ajili ya kujifunza, ni kwanini Mahakama ilikataa maneno hayo kutoka kwenye hiyo flash?

Pia ikiwa Lissu aliwekwa gerezani kabla ya uchaguzi miezi kadhaa kabla ya ule uchaguzi na hadi wakati wa uchaguzi alikuwa chini ya magereza, Je uhalali wake na uhusika wa yaliyotokea siku ya uchaguzi unatokea wapi?
 
Nipo hapa kwa ajili ya kujifunza, ni kwanini Mahakama ilikataa maneno hayo kutoka kwenye hiyo flash?
Lissu ni mbobevu wa Sheria.
Kuna namna Ushahidi uliwasilishwa vibaya . Na vipengele vya sheria vikambeba Lissu.

Mfano Mahakama imekataa hadi ile video.
hii ya video ni kuwa Shahidi aliyeiwasilisha video pale mahakamani alikuwa Hana mamlaka kisheria.
Pia ikiwa Lissu aliwekwa gerezani kabla ya uchaguzi miezi kadhaa kabla ya ule uchaguzi na hadi wakati wa uchaguzi alikuwa chini ya magereza, Je uhalali wake na uhusika wa yaliyotokea siku ya uchaguzi unatokea wapi?

Soma hapo juu mfano wa Niffe post #86.

Kwa Lissu Kusingefanyika Fujo basi alikuwa hana hatia.

Pia Ushahidi wa Mo29 Mahakama imeukataa kuuongeza.
Lissu aliweka pingamizi la kisheria.

Na bila ushahidi wa Video na Huu wa maandishi wa mo29.
Lissu anashinda kesi.

Tatizo DPP hatakubali . Akiona anashindwa basi Ataifuta kabla ya hukumu na kuifungua upya. Inaanza moja na Ushahidi wote unasukwa vizur na kuanza kusikilizwa tena.

Kiufupi. Hili Jambo ni Kutunishiana misuli kisheria.
 
Ni kweli Kesi iliyofunguliwa April ni ya Uhaini na haihusiani na Mo29.

Ila haya ndio maneno ya Lissu.

"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"

Wanachofanya Hawa mawakili sasahivi ni kuhusisha haya maneno na zile vurugu.
Hata kama hati ya mashtaka haisemi kuhusu vurugu.
Sasa zile vurugu sio Uhaini..
Kukinukisha labda tupate tafsiri Mpya
Kuzuia Uchaguzi sio uhaini

Na jaji kasema mambo ya October 29 yasiletwe Mahakamani...

Na kama Kuna watu walifanya vurugu October 29 ...mbona walisamehewa ?

Ina maana hayo maneno ya Lissu kama wanataka yatumike Mahakamani...kesi itabadilika kutoka Uhaini Kwenda kuwa Uchochezi
 
Na jaji kasema mambo ya October 29 yasiletwe Mahakamani...
Yes. Hapa Lissu ameshinda.

Na kama Kuna watu walifanya vurugu October 29 ...mbona walisamehewa
Raisi aliwafutia mashtaka.
lakin Wangekuwa na shtaka la kujibu.

Kuchoma sheli , Ofisi za serikali na polisi kwa sheria za TZ ni Kesi ya Kigaidi.
Fujo zingeishia barabarani ni vurugu.
Fujo zimesababisha mali kuchomwa ni Ugaidi.

Umeona sasa mstar mwembemba unaotenganisha hapo?.
 
Sasa hizo fujo kafanya Lissu ?

Wapi Lissu alisema kachomeni moto vituo vya mafuta?
 
Kukinukisha labda tupate tafsiri Mpya
Kuzuia Uchaguzi sio uhaini
Kukinukisha au kuzuia uchaguzi sio kosa la kiuhaini.

Kukinukisha au kuzuia uchaguzi kwa kuchoma ofisi za serikal ni kesi ya kigaidi na uhaini.

Hata ww leo. Ukichoma ofis ya serikal ya mtaa unastakiwa kama Gaidi.

Ndio sheria ya TZ inavyosema😊😊😊
 
NARUDIA TENA KUSEMA

Kumshilia Lisu hakutaweza kuleta mabadiliko ambayo wananchi wanayahitaji,Tangu awali watu na wapenda amani ya nchi hii walishauri ya kwamba,yafanyike mabadiliko katika ngazi zote za uchaguzi ikiwemo,Kutowaengua kihuni wagombea wa upinzani,Makamishina na wakurugenzi wapatikane kwa utaratibu mzuri ambao hauegemei upande wowote

Kwa mfano :-

Wapenda demokrasia na wapenda amani wakasema,Ndugu Ramadhani Mapuri ambaye ni mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye alikuwa balozi,amewahi kuwa mwananchama wa Chama Cha Mapinduzi,Hivyo anapaswa kukaa pembeni ili kutenda haki katika tume lakini kwakuwa hakuna viongozi wapenda amani toka moyoni ila wanapenda kutamka neno "Amani" midomoni mwao wakasema liwalo na liwe hawezi kung'ooka mtu!

Ok bado wapenda amani wakaendelea kusisitiza ya kwamba,Wakurugenzi ambao ni wateule wa Rais hawapaswi kabisa kusimamia uchaguzi kwasababu huko kwenye Halmashauri huwa wanagoma kuwaapisha mawakala wa vyama vya wapinzania na kuwaengua wapinzani kihuni!

Hayo ni miongoni mwa mambo machache ambayo watanzania wanayapigia kelele lakini kwakuwa hamtaki kusikia na kuyafanyia kazi,nyie mnaendelea kumshikilia Tundu Lisu kana kwamba ndiye anaye kwamisha mambo hayo!

Mwaka 2030 ni Kesho kutwa Tu!,Msipofanya mabadiliko wananchi wakamchagua kiongozi wanayemtaka,Nawahakikishia Mtaua tena watanzania wengi zaidi ya mlivyofanya Octoba 29

Vinginevyo siku ya Uchaguzi hakuna mtanzania ataenda Kupiga kura,Watanzania wote watajifungia ndani siku hiyo kwa kuhofia kilichotekea Octoba 29
 
Lissu kaanza lini kuipenda serikali mpaka aionee huruma kufungua sanduku la Pandora? Kesho babu yenu anakaangwa na aibu mtaona nyie, chonde chonde asimpangie cha kusema shahidi wa mashtaka hiyo kesho!!
Ww utakuwa ni mjinga kweli, kila mchezo una kanuni na wala haogopi. Huwezi kuongea chochote kama sio sehemu ya ushahidi. Kama unataka kuongea chochote nenda sokoni. Kama jamuhuri ingekuwa ina ushahidi wa maana asingewashinda huko kote. Unapoona shahidi wa jamuhuri anaongea chochote, ujue anachotakiwa kuongea hakipo.
 
Na ya yule muaji mkuu yataishia jela za ICC.
Niamini nikukuambia.
Aliyetoa order ya shoot to kill ni IGP.

Alipenyezewa taarifa za kiintelejensia kuwa kuna watu wana silaha za moto wako Mitaani. Na wengine wana Mikuki , Nondo na visu. Na kuwa wana mafunzo maalumu na wamefadhiliwa.

Ndio maana akaamua kuchukua hatua ile.

Juzi hapa Rais ameongea alivyokutana na tume ya pili.
Kuwa waangalie ni nani aliwafadhili wale wafanya vurugu.

Tetesi :
Sijasema kuwa walipewa intelejensia kwamba kuna wanajeshi pia wako mitaani.
Onganisha pia na Speech ya Capt Tesha.

Alaf ndio utajua kwanini Walitumia nguvu kubwa namna ile.
 
Back
Top Bottom