Kuna mstari mwembamba sana unatenganisha hapa. Na mara nying watu hawauoni au kuchanganya.
Uhaini maana yake ni Usaliti.
Usaliti wa Serikali ya nchi yako unayoishi.
Kuzuia uchaguzi sio Kosa la Uhaini.
Lakini unazuiaje huo uchaguzi?.
Kwamfano ukisema Jaman msiende kupiga kura, sio kosa la kiuhaini.
Ila ukifanyia watu fujo wasiende kupiga kura ni kosa.
Kwahiyo hapa inaangalia matendo sio maneno.
Mfano Niffer alikamatwa sio kwasababu aliwaambia tu watu wasiende kupiga kura.
Bali Alihamasisha watu kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawazuie watu wasiende kupiga kura.
Akawahamasisha watu wanunue mask ili mabomu ya machozi yasiwadhuru. Akahamasisha watu wabebe maji.
alaf siku ya uchaguzi. Kukatokea vurugu . Hata kama Niffer hakuwa eneo la tukio. Bado yeye ni mshtakiwa kwa sababu alikuwa na nia na amehamasisha watu kufanya kosa.
Kama angehamasisha (maneno) na vurugu zisingefanyika alikuwa hana kosa.
Ila vurugu (matendo) zilifanyika. Na ndio maana alikamatwa.
Na kosa lake likawekwa kama uhaini maana anasaliti serikali unayotakiwa Kuwekwa kwa mujibu wa kisheria.
Usaliti?
Usaliti kwenye kitu gani?
Raia wa kawaida haweziitwa msaliti.
Usaliti unahusu makubaliano. Sio nje ya hapo. Dudukwe au wewe huna uwezo wa kuisaliti nchi yako kama ni raia wa kawaida.
Labda kama mlifanya makubaliano fulani.
Ndio maana kuna Viapo.
Au labda wewe tangu umezaliwa kuna sehemu uliapishwa na kukubaliana kuhusu nchi yako. Ndio unaweza kuwa msaliti.
Iko hivi, hii Dunia mambo ya nchi, utaifa yapo kisiasa, nje ya hapo hapana mipaka, ndio maana leo hii nchi inaweza kuwa Tanganyika kesho ikawa Na jina jingine kabisa na mipaka mingine kabisa.
Wanaosaliti nchi ni waliokula viapo.
Kingine kuna tofauti kubwa kati ya Usaliti na uhaini.
Mhaini ni mtu yeyote anayetaka, mwenye nia, au anayetaka kupindua serikali iliyopo madarakani. Huyo ni mhaini.
Msaliti ni mtu aliyegeuka, aliyeasi makubaliano. Huyo ni msaliti.
Tukirudi kwenye mjadala.
Suala la Niffer lilikuwa kisiasa.
Wewe kusema utagawa barakoa kwa watakao Andamana sio kosa. Ukizingatia maandamano yapo kisheria na yapo kikatiba.
Watu kufanya vurugu siku ya maandamano haihusiani na Niffer kugawa barakoa au kusema atagawa barakoa. Hakuna uhusiano..
Kwenye maandamano kunakuwaga na mabomu ya machozi ni kweli kwa sababu kunatokea vurugu. Kwa sababu sio watu wote wanaweza kuandamana bila vurugu. Hivyo kuwaambia watu waende na maji na barakoa sio kosa kisheria.
Mtu anaweza kubeba barakoa kwa sababu ya vumbi kutokana na Umati, afya kutokana Umati kuwa mkubwa na watu wanaafya tofauti, na kubeba maji kwa sababu ya kunywa.
Hivyo kisheria huwezi mkuta na hatia mtu aliyesema mbebe maji na barakoa kwenye maandamano au nitawapa maji na barakoa.
Labda uamue kumuonea tuu lakini sio kosa.
Kwenye maandamano hata halali uhalifu unaweza kutokea ndio maana polisi wanakuwepo.
Kwenye mechi tu za Simba na yanga uhalifu unatokeaga, watu wanaharibu uwanja wanang'oa viti n.k.