Hii kauli ya Magufuli "Polisi ueni Majambazi", imenitisha sana

Hii kauli lengo lake kuu ni polisi wauwe raia wakati wa uchaguzi na isemekane kuwa ni majambazi
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake haitamshtaki askari polisi ikiwa ataua jambazi mwenye silaha.


Mgombea huyo alitoa ahadi hiyo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Mtwara.


“Katika serikali yangu askari akimpiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona hawavamii kambi za jeshi, Jeshi la Kujenga Taifa au Ukonga FFU?, wanaona polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua,” alisema Magufuli.



Mgombea huyo wa urais wa CCM pia aliahidi kwamba ataboresha maslahi ya askari polisi ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na wakiwa na furaha.


Chanzo: IPPMEDIA


Mytake: Magufuli katika ubora wake..........Mahakimu na majaji ombeni likizo
Ni kweli mkuu mahakimu na majaji hawatakuwa na kazi hasa ikizingatiwa kuwa huyu bwana ana rekodi ya kudharau mahakama akiwa bado waziri tu akiwa rais si itakuwa hakuna mahakama !!
 
wanabodi
Hivi majuzi Magufuli akiwa kwenye mkutano wa hadhara alilitaka jeshi la polisi kuwapiga risasi majambazi yote...
Hata jana 04/09/ Babu Duni akiwa Bagamoyo alikosoa vikali kauli hiyo ya hatari kwa utulivu wa nchi..

my take:Magufuli jinsi alivyo sura yake ndivyo moyo wake ulivyo
 
Nipashe la mengi ,mengi anataka lowasa ashinde halafu wote wanatoka kaskazini conect dot we usiyejitambua.
Kwahiyo mengi ndo mhariri wa gazeti? jitoeni ufahamu lakini elewa hela za misaada zimezuiwa sababu ya ccm kuendekeza ufisadi...tufanye mabadiliko.
 
Nipashe la mengi ,mengi anataka lowasa ashinde halafu wote wanatoka kaskazini conect dot we usiyejitambua.
Duh!! Na hata huyo Dr Slaa naye kusema Magufuli alimhonga hawara wake nyumba ya serikali naye si anatokea Kaskazini!? Na nina amini kama Magufuli angekuwa Muislam ungesema Mengi ana mtetea Lowasa kwa kuwa ni Mkriso mwenziwe. Amakweli CCM mme changanyikiwa.
 
Nipashe la mengi ,mengi anataka lowasa ashinde halafu wote wanatoka kaskazini conect dot we usiyejitambua.

Hapo kwenye red, hizi ni kauli za kibaguzi, ubaguzi wa ukanda hauna nafasi inaonekana umefiriska kufikiri waachie wengine wachangie
 
Kauli ya mgombea uraisi wa ccm kusema hadharani tena kwenye hadhira ya watu kuwa polisi wawauwe majambazi, imeonyesha yeye ni mtu wa namna gani hata akichaguliwa kuwa rais wa nchi. Magufuli ameonyesha yeye atakuwa dikteta wa hali ya juu. Na hafai kuongoza nchi hii. Watanzania wenzangu ninawaasa tusije tukamchagua kiongozi kama huyu tutajuta! Mambo mengi amekwisha fanya akiwa kama waziri yalijaa jazba kubwa na udikteta ambao hayazingatii sheria za nchi zinasemaje na mwisho wa siku zimekuja kuleta hasara kubwa kwa nchi! Kuvunja kwa kituo cha mafuta mwanza na ukamataji wa meli ya kigeni ya samaki yanaonyesha ni mtu anafanya mambo kwa hamaki! Pia amekuwa ni mtu anaetoa kauli za madharau kwa sababu ya cheo chake. Kauli kama wasioweza kulipia nauli mpya wapige mbizi! Au kauli ya kusema wenye malori kama hawawezi kulipa hizo faini wakapaki malori yao jikoni, ni kauli ya mtu ambae hajali. Huyu mtu wa namna hii hafai kwa mustakabali wa nchi hii. Naomba watanzania tusimuingize madarakani mtu kama huyu atatuletea matatizo makubwa! Mwenye masikio na asikie.
 
Unashangaa hiyo wakati majambazi yanaua?

Raia wanaua kibaka anaeiba pichu itakuwa jambazi?

tafuta jingine, hilo umebugiiiiiiiii maaan,
 
Jambaz ni muuaj hapaswi kuachwa hai jambaz anaua na hata hukmu ya uislam jambaz anatakiwa kuuawa akuthibitika hao ni watu hatar hongera maguful
 
wanabodi
Hivi majuzi Magufuli akiwa kwenye mkutano wa hadhara alilitaka jeshi la polisi kuwapiga risasi majambazi yote...
Hata jana 04/09/ Babu Duni akiwa Bagamoyo alikosoa vikali kauli hiyo ya hatari kwa utulivu wa nchi..

my take:Magufuli jinsi alivyo sura yake ndivyo moyo wake ulivyo
Hili jambo na kufananisha mabadiriko tunayitaka na yaliyofanyika Libya na Misri zina muondolea credit kabisa Magufuri sijui NEC hawasikii mbona sijaona wamwonye. Je UKAWA mko wapi ? perekeni malalamiko rasmi NEC.
 
Jambaz ni muuaj hapaswi kuachwa hai jambaz anaua na hata hukmu ya uislam jambaz anatakiwa kuuawa akuthibitika hao ni watu hatar hongera maguful
Mkuu umezungumzia hukumu baada ya kupewa haki yake ya kikatiba ya kusikilizwa kwanza , ama sivyo CCM ifute mahakama na tunakoelekea bila shaka itakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom