Hii kauli ya Magufuli "Polisi ueni Majambazi", imenitisha sana

Leo katika shughuli ya ufunguzi wa kituo cha kisasa cha mawasiliano cha polisi katika kukabiliana na uhalifu, Mh. Rais Magufuli amewaagiza polisi kwa msisitizo kuwa mnapowakamata majambazi wenye Silaha muwe mnawakamata haraka huku akisisitiza nadhani mnanielewa.

Mimi binafsi nimefurahishwa sana na agizo hilo maana majambazi yamezidi kiasi kwamba inatishia usalama wa nchi.

Mkuu interejensia ya kuwabaini wana siasa wa upinzani haiwezi kuwabaini majambazi???
 
Kwa mapolisi waadilifu hii sentensi inaeleweka,kwa polisi
wanaoitwa polisi lakini mioyoni hawana tofauti na wanaokamatwa
hii ni tungo tata.
Lengo la Mh. rais ni zuri tena kutoka moyoni
ila watekeleza amri hapo ndo kizungumkuti kinapoanzia.
 
Hivi mwanzoni walikuwa na vibali? mbona sasa wanaambiwa wakamatwe? Tanzania raha kwelikweli
 
Kwa mapolisi waadilifu hii sentensi inaeleweka,kwa polisi
wanaoitwa polisi lakini mioyoni hawana tofauti na wanaokamatwa
hii ni tungo tata.
Lengo la Mh. rais ni zuri tena kutoka moyoni
ila watekeleza amri hapo ndo kizungumkuti kinapoanzia.
Mkuu majambazi sio wa kuwaonea huruma
 
Kuna mtu wa CHADEMA anaitwa Malisa ashaanza kuwadanganya watu huko anasema eti Raisi amesema watuhumiwa wa ujambazi wapandishwe cheo kabla ya kufikishwa mahakamani. imenilazimu kuja kuipitia tena hii clip
 
Mkuu majambazi sio wa kuwaonea huruma
Mkuu unaikumbuka issue ya zombe?
waliouawa waliitwa majambazi,tukalipongeza jeshi la polisi baadaye,ikasemekana walikuwa
wafanya biashara,fedha yao ndo iliyowaponza.
Ndo maana nikasema jambazi kama ni jambazi kweli apigwe tu.lakini kama ni jambazi
kwa kuangalia ana nini mkononi kimaslahi hapo Mungu atuhurumie.
 
Kwa mapolisi waadilifu hii sentensi inaeleweka,kwa polisi
wanaoitwa polisi lakini mioyoni hawana tofauti na wanaokamatwa
hii ni tungo tata.
Lengo la Mh. rais ni zuri tena kutoka moyoni
ila watekeleza amri hapo ndo kizungumkuti kinapoanzia.

Kulikuwa na kamchezo fulani kanafanywa na hapo kituo cha mawasiliano.

Ndio maana raisi JPM amesisitiza hilo, nadhani utaielewa Mkuu.
 
Jambazi akienda na silaha kufanya uhalifu... haijaibeba kwa ajili ya maonesho... anaenda kuitumia... inabidi na yeye akamatwe haraka haraka..
 
Mkuu unaikumbuka issue ya zombe?
waliouawa waliitwa majambazi,tukalipongeza jeshi la polisi baadaye,ikasemekana walikuwa
wafanya biashara,fedha yao ndo iliyowaponza.
Ndo maana nikasema jambazi kama ni jambazi kweli apigwe tu.lakini kama ni jambazi
kwa kuangalia ana nini mkononi kimaslahi hapo Mungu atuhurumie.
Hapo Zombe ndo alikuwa jambazi.Polisi wenyewe nadhani ndo majambazi
 
Hawa majambazi silaha wanazipata wapi au kuna sarakasi fulani zinachezwa..!?
 
Hapa ndo napomkubali huyu mzee, majambazi piga risasi baasi, hakuna kulemba. Mambo ya kusubiri sijui haki ndo maana tunakuwa hatutoki. Probability ya kuwa mtu mwenye silaha sio jambazi ni ndogo sana, pia probability ya kusingiziwa kesi nazo sio nyingi.
 
Back
Top Bottom