Hii kauli ya Magufuli "Polisi ueni Majambazi", imenitisha sana

Magufuli anatumia nini kufikiri, harafu niliwasikia ataanzisha mahakama ya mafisadi ili wafungwe haraka....kauli hizi hata yule babu wa Serena hawezi kuzisema
 
Hivi wewe unaongea vitu gani?!Hivi unazijua sheria na miiko ya jeshi wewe?!au unaongea tu?
Mkuu kwanza nadeclare interest kuwa elumu yangu ni ya gumbaru , Sasa naomba unieleze ni polis wa nchi gani unaozungumzia? Je ni polis hawa wanaolalamikiwa kila siku kubambikia watu kesi , kula rushwa na kuua watu kama ilivyokuwa kule Morogoro nyororo na baadae kusema wameangukiwa na kitu chenye ncha kali n.k au ni wapi?!!
 
Hasara za kauli kama hizi ni pale polisi itakapokuwa inauwa watu hovyo kwa kudhani ni majambazi! Wakiulizwa watasema tulidhani ni majambazi! Mbona sharia ipo wazi kwamba polisi anaruhusiwa kuua kama huyo mtuhumiwa naond=ekana kuwa na uwezo wa kumdhuru polisi? Kuna sharia inasema polisi wakivamiwa na majambazi kituoni wasiwaue? Mbona wamehsua wengi tu katika mapmabano bila kusubiri kuambiwa na Magufuli? Magufuli alikuwa anamaanisha zaidi ya hapo kwamba polisi akikutana na jambazi whehetr la kweli au la kudhani ua? kweli? utwala wa sharia upo wapi?
 
Sasa kiongozi we ulitaka majambazi wachapwe viboko

Kuna faida zaidi kumkamata jambazi kuliko kuliua> Ukiliua unakuwa huwezi kuapata taarifa muhimu za kujua mtandao mzima wa majambzi. kwa hiyo kuua majambazi haina tija sana km lenngo ni kupambana nao. Mtu akishaamua kuwa jmbazi huwa haogopi tena kufa. kwa hiyo kumuua sio issue. Umahiri wa polisi utaonekan katika kuweza kuwakmata mjambazi yakiwa hai ili yasaidiwe kuonesha mbinu zao na kuwataja wengine. lakini sio kuua!
 
Sasa hao majambazi wanavyouwa raia ni sawa. Juzi tu apo jangwani majambazi yameuwa mtu kwenye daladala na kutoweka. Apo nyi mmelizika kama matukio km hayo hayajakukuta utachukulia laisi tu. Ila kiukweli inaumaaa. Ikiwezekana mtu akikutwaa na hatia auliwe tu.
 
Katika uchambuzi wa magazeti ya leo gazeti la NIPASHE limeandika kuwa Magufuli ametoa amri polisi waue majambazi !!!

Kauli hii nategemea wanaotetea haki za binadamu waitolee maelezo kama walivyoshupalia kauli ya babu Seya kuachiwa na Rais.

Kama rais mtarajiwa anatoa amri ya watu kuuawa bila kupelekwa mahakamani je akiwa Rais watu watasalimika?

Wanasheria na watetezi wa haki za binadamu naomba kauli yenu.

Chanzo: NIPASHE YA LEO.

Khe yaani wewe unawaonea huruma majambazi 😳😳😱😱😱
 
Hakuna jambazi. Ni mtu. Ukiua jambazi umeua mtu! Usijichukulie sheria mkononi!!!!
 
Katika uchambuzi wa magazeti ya leo gazeti la NIPASHE limeandika kuwa Magufuli ametoa amri polisi waue majambazi !!!

Kauli hii nategemea wanaotetea haki za binadamu waitolee maelezo kama walivyoshupalia kauli ya babu Seya kuachiwa na Rais.

Kama rais mtarajiwa anatoa amri ya watu kuuawa bila kupelekwa mahakamani je akiwa Rais watu watasalimika?

Wanasheria na watetezi wa haki za binadamu naomba kauli yenu.

Chanzo: NIPASHE YA LEO.

Mi pia alinitisha sana
 
Nimeota kuwa uchaguzi wa kumpata mgombea ndani ya CCM bado haujaisha na hivyo huenda kura zisipigwe tarehe 25 kwani nimeota utasogezwa mbele.. Nimeota kuna kitu kitampata mgombea na hivyo kuna chama kitapewa fursa ya kuchagua mgombea mwingine na hivyo kupeleka mgombea wamtakae.
Ndoto nyingine ni mbaya sana na zinatisha mbaya.

Aitheeeee!!!!!! lazima ulivimbiwa wakati unaota hii ndoto.
 
Hii kauli haina tofauti na ile ya Pinda,Piga tuuuuuu,CCM utawala wa sheria siyo jadi yao.Kama jambazi amemgeuzia mgong unamua ili nini?Je akijisalimisha naye atauawa?

Kwanza hii nchi majambazi yapo huru hayana shaka yanakula bata tu, ila raia mwema upepo ukimwendea vibaya ndio anasingiziwa jambazi.
 
Hivi ukigombana na mtu, kisha ukamuua, ukishitakiwa ukasema alikuwa ni jambazi, itakuwaje na imetamkwa kama ni jambazi auwawe...Tuwapime hawa wagombea kwa kauli zao
 
adinselemaaaa....!
1.waue tu mana hakuna namna nyingine...pombe

2.wapigwe tu,mi nasema muwapige tu...mr kulialia

3.hao wanafunzi wanaopata mimba wana viherehere..by dhaifu classic

4.tutakula nyasi ila lazma ndege ya rais inunuliwe...??

5.kama huna nauli ya panton piga mbizi...pombe

6.nyinyi munaonisikiliza hapa wote malofa na wapumbavu..by mpumbavu ben
 
Unamaanisha jambazi yeye ndio ana uhalali wa kuua polisi, ambao kwa mawazo yako unaona wao sio watu?
Jambazi ni mtu na Polisi ni mtu. Hakuna anayestahili kumuua mtu mwingine. KIla mtu ana haki ya kuishi. Kuna sheria ambazo lazima ziachwe zichukue mkondo wake wa kumpatia haki kila mtu!
 
Back
Top Bottom