Hii inapendeza sana kwa wapenzi

Hii inapendeza sana kwa wapenzi

Pengine hakuna wanaume wakamilifu lakini wanaume bora ambae anaweza kusimama mbele ya macho ya watu na kusema wewe ni bora kwake, wapo na Mungu anajua wallipo ni kumuomba akuonyeshe

Uko kukosekana kwa wanaume wakmilifu ndo kunakopelekea kukosekana wakina Michelle, ila Kama upo kiobama, utampata Michelle wako,

I believe utampata wapo wengi tuuuh
 
Nimekupenda sweet

Mungu akupi mbali nawewe , wala akupi tofauti nwewe, atakupa type yako kabisaaaaa, sa kma unjikuta sii Obama alafu unmtaka Michelle sijui inakuwaje apo.....
Michelle lazima apate shida.
 
Hakuna mapenzi duniani yanayoweza kushamiri bila uvumilivu. Mtu asipokuwa na moyo wa uvumilivu katika mapenzi basi kila mtu utamuona hafai. Kila siku utakuwa mtu wa kuanzisha mahusiano mapya kitu ambacho si kizuri.

Ni kweli, uvumilivu ni nguzo kubwa Sana kwenye mahusiano...
 
Haha dah aise,,hivi ukampenda mwanaume wako katika hali zote na yeye anajituma ataacha kukuhudumia kwa uwezo wake?? Tatizo wanawake wengi wa sikuhizi wanataka mambo makubwa kushinda uwezo wao mambo hua yanaenda taratibu, raha iliyoje mnakula matunda ya uvumilivu wenu na mlipotokea chini had mkawa na vingi sasa...lakin yote hayo kama hamna Mungu katikati yenu ni kaz bure ...kuna thread moja humu mwanamke anaomba ushauri amsaidie vipi mumewe aongeze kipato chake kutoka biashara anayofanya...ni wanawake wangapi wana moyo huo??
Kama ni mapenzi sijui kama kuna anayependa kweli kama mwanamke, ila life teaches people the hard way ndo mana...tusilaumiane ni maisha tu,uvumilivu doesn't guarantee happy endings always... U have to take calculated risks na umuombe Mungu akuhurumie na dhambi zako hivyo hivyo
 
Kwakwel mtabaki mnakazania point ya upotential lakin ukwel unabak pale pale kwamba love ili wa bind them pamoja ...achilia mbali elimu zao ...kwaio unataka kuniambia barack aliangalia elimu ya michelle ama michelle aliangalia elimu ya barack...hivi mmesikiliza vizuri alichoongea juzi katika hotuba yake ya kuwaaga wamerakani? Wakat anaongea na michelle?,,mlimsikiliza aliongea nini?
sawa mtajiandaa ujanani lakin kama hamna upendo wa dhati katikati yenu ni kaz bure tu.
Upendo basi angependa hata kondakta..the lady is smart wewee...Obama tangu yuko Harvard alishaingia kwny siasa low key...I agree upendo upo but she chose her type sio kirejareja tu.,
 
Nimekupenda sweet

Mungu akupi mbali nawewe , wala akupi tofauti nwewe, atakupa type yako kabisaaaaa, sa kma unjikuta sii Obama alafu unmtaka Michelle sijui inakuwaje apo.....
Ndo hapo mtu anabaki kulalama hampati Michelle, sasa mtu anampataje Michelle wakati yeye si Obama bali Joseph Konyi

Maana unakuta akina Michelle wote wako kwa Obama zao. Yeye atabaki tu na wa size yake.... Hahaha

Na kumbuka Michelle hawezi kuwa Michelle bila Obama, na Obama hawezi kuwa Obama bila Michelle.... If u know what am talking about...
 
Kunasiku wallet itatoboka. Na hapo ndipo utakaposimangwa na kuitwa mwanaume suruali. Maisha ya sasa dada zetu wengi wamekuwa mwiba. Hali inayopelekea na vijana wengi kuogopa kuoa na kuwa committed kwenye relationship
Hehehe wanawake wanavyotelekwa wanaume wanachukua nyumba ndogo mnadhani mabinti nao hawana la kujifunza hapo...kika mtu anahofia to let their guard down,ukijifanya unapenda sana unakua mistreated,always have a reserve for urself..usijiendekeze mnooo
Wangapi wamevumilia waume zao ktk shida na kuambulia nothiiiiing....?hehe omba tu Mungu
 
If he was somebody mbona alikuwa anaomba vibarua vya kazi alipokuwa chuo. Ukweli unauma. Ukisoma story jamaa walianza relationship wakiwa chuo. Na kabla ya kuanza kibarua jamaa kipatochake kilikuwa mkopo wa chuo kikuu
Dude even became chairman of Harvard Law Review, jmn he wasn't a nobody... Don get it twisted... He was somebody.. Miaka hio kusoma chuo tena Harvard afu blackii ilikua bongeee la dilii,
 
Dude even became chairman of Harvard Law Review, jmn he wasn't a nobody... Don get it twisted... He was somebody.. Miaka hio kusoma chuo tena Harvard afu blackii ilikua bongeee la dilii,
Sometimes kujiweka vizuri ni muhimu.
 
Kwakwel mtabaki mnakazania point ya upotential lakin ukwel unabak pale pale kwamba love ili wa bind them pamoja ...achilia mbali elimu zao ...kwaio unataka kuniambia barack aliangalia elimu ya michelle ama michelle aliangalia elimu ya barack...hivi mmesikiliza vizuri alichoongea juzi katika hotuba yake ya kuwaaga wamerakani? Wakat anaongea na michelle?,,mlimsikiliza aliongea nini?
sawa mtajiandaa ujanani lakin kama hamna upendo wa dhati katikati yenu ni kaz bure tu.
Hakuna upendo bila matendo. Naamini walitendeana vyema, walijaliana, waliheshimiana, walijitoa kwa moyo kila mtu kwa mwenzake. Penzi lao likakua mpaka leo tunawatolea mifano.

Sasa baadhi ya wanaume wanataka mwanamke ndo aonyeshe upendo wa mshumaa.
 
Upendo basi angependa hata kondakta..the lady is smart wewee...Obama tangu yuko Harvard alishaingia kwny siasa low key...I agree upendo upo but she chose her type sio kirejareja tu.,
Alifanya chaguo sahihi, wa kufanana naye.
 
Haya mambo mnayaexagerate sana, mbona wapo wengi tu, kwani akina mama Salma,Anna,Janeth walianza na waume zao wakiwa na kipato gani??

Hao hao unaodai wana hali za chini ndio kwa kiasi kikubwa sana wanaoa,kwani wanaoa wanawake wa nchi gani? Suala la mahusiano ni la wawili hivyo likifail basi ujue wote mmechangia kwenye kufail kwake.

Na wanaume wengi wa kitanzania waliofanikiwa basi wengi walianza chini sana na wake zao,ila wakishafanikiwa ndio mabalaa yanaibuka,but unakuta wake zao wapo nao tu, na wengine hudiriki kabisa hata kuacha wake zao maana wakati huo ndio wanakuwa hawafai bali dogodogo ndio wanafaa, hebu ifike hatua muwape credit zao muone na mazuri yao.

Tatizo letu watz ukikataliwa na mwanamke au ukiachwa basi unahukumu wanawake wooote,akikuacha basi shukuru,muache aende as maybe kubaki nawe ndio ingekuwa anguko lako,hakuwa wako huyo,wa kwako atabaki nawe katika hali zote.

Mpendwa natamani ningekuwa na pc hili nikujibu vizuri hii reply yako paragraph after paragraph lakini kwa bahati mbaya natumia simu, ila ntakujibu kama ifuatavyo naamini utanielewa tu.

Kwanza kabisa kama umelielewa vizuri bandiko langu hakuna exeggeration yoyote ile bali safari ya obama na Michelle ni ya kipekee sana kulingana mazingira yao, na hauwezi ukawalinganisha na hao uliotaja hapo.. Alafu huyo mama janeti magufuli hakustahili kabisa kumuorodhesha kwenye huo mfano wako, yaani huyu mama janeti aliyekataa kumpigia mumewe kampeni,... huyu mama janet ambae hakuna shughuli yoyote ya kijamii tunayomuona akifanya,...huyu mama janet ambae watanzania wengi hawajui kama yeye ndio first lady eti ndio unatupa kama mfano wa Michelle serious!? kwa context iliyopo hapa huyo jenet hayumo kabisa wanawake ambao ulitakiwa kuwa mention hapo regarding to the context labda mama Maria nyerere na mama Salma kikwete.

Unasema kwamba wanaume wenye kipato cha chini ndio wanaoa kwa kiasi kikubwa, sawa hili sikatai lakini je, wanaoa wanawake wa aina gani!!? Je wanaoa wanawake wanaolingana nao au kuwazidi vipato!? je wanaoa wanawake wanaowazidi kielimu!? na kama wapo ni wangapi kati ya hao wengi!?... The gospel truth ni kwamba wanaume wengi hao wenye vipato vya chini wanaoa ma low life wenzao na hili limechangiwa na pande zote mbili Yani wanaume na wanawake pia simaanishi kwamba mwanaume mwenye low status hawezi kumuoa mwanamke mwenye high status.

Ni kweli kuna wanaume wengi tu wa kitanzania walionzia chini sana na wake zao na walipofanikiwa wakageuka chatu kwa wake zao kwa kuwaachia maradhi ya moyo na wengine hata kuwauwa kabisa. Hakika ni ukweli usiopingika hakuna watu wanaojua kuvumilia wanawake na wanaongozwa kwa kunyanyaswa na mimi binafsi huwa namuheahimu sana mwanamke yoyote anayestahili kuheshimiwa haijalishi mahusiano yangu na yeye yako vipi.

Kuwahukumu wanawake wote kwa kosa la mwanamke mmoja huo ni upuuzi wa hali ya juu, lakini mimi binafsi naongelea hali halisi nnayoiona kwa hiyo usishangae kuona nikiinvolve majority. Wanawake wengi wa kipindi hiki hawana sifa za kuitwa wake, wengi wao ni wavivu kwanzia kufikiri na wana golddigging traits... The representative sampling suffices, angalia tu hata humu jamiiforum wanawake wanaokuja kutafuta partners style wanayoingia nayo..

eti mtu anakwambia asiwe mweusi sana awe maji ya kunde! serious hiv kweli una akili zako timamu hicho kinaweza kuwa ni kigezo cha kuangalia ukiwa unatafuta mume?

Haya sijui eti mara awe na degree pia na kazi nzuri..!! huu si ni upuuzi? je kama hana kazi nzuri kwa muda huo lakini kupitia wewe kwa network uliyonayo unaweza kumfanya akawa na kazi nzuri tu hapo tayari mkiwa kwenye mahusiano. Na sidhani kama hata huwa wanafikiria hili.

Kupitia hawa na hizi sababu zao chache unaweza kuona jinsi gani mabinti wengi wanavyokosa material ya kuitwa wife, na hawa ni reflection ya waliopo huko mitaani. Yaani wengi wanapenda mwanaume ambaye tayari yuko accomplished Najua hii sio kwa wanawake wote ila kwa hawa waliozaliwa miaka ya 80s kuja huku juu wengi wako hivyo. They are too selective and lazzy.

Wanaume tuna makosa yetu na tumechangia kwa kiasi kikubwa sana kuwaharibu hawa wanawake na sasa hatuna budi kuubebea huu msalaba.

Mwisho kabisa niseme kama Michelle wapo tanzania hii but finding one is like a needle in haystack.
 
Hakuna upendo bila matendo. Naamini walitendeana vyema, walijaliana, waliheshimiana, walijitoa kwa moyo kila mtu kwa mwenzake. Penzi lao likakua mpaka leo tunawatolea mifano.

Sasa baadhi ya wanaume wanataka mwanamke ndo aonyeshe upendo wa mshumaa.
Hakuna kitu hapo alifanya usanii tu, inaonekana huwajui vizuri wazungu
 
Dunia ya sasa ni wachache sana wanaojitoa kumpenda mtu genuinely. Wengi ni upendo wa maneno tu. Inasikitisha
Dahhh very true. Kuna mtu niliachana kwa kumwambia "tunaachana kwasababu nakupenda sana, siku moja naweza kufa kama nitaendelea kuishi na wewe"

Mapenzi ya siku hizi, everyone either he or she is on guards every time. Unakua ka vile upo kwenye mahusiano na some sort of nemesis. Kila siku mashindano, who talk more smarter,more responsible, more everything.....

All in all deep down within us, ipo roho yenye upendo ila tunaogopa kupenda. Love has become a vice not a virtue
 
Wanawake au wanaume wachache sana wanaweza kuchukua ndoto za wenzi wao na kuzifanya zao(as a team). Kuna tamthilia "House of Cards" Frank and Claire Underwood inatoa mwangaza fulani hivi wa maisha ya ndoa unapokua mtu maarufu au wadhifa mkubwa kwenye jamii.
 
Ni kweli. Kuna shida mahali. Wanaume wengi wanatembea peke yao kwenye ndoto zao.
 
Dahhh very true. Kuna mtu niliachana kwa kumwambia "tunaachana kwasababu nakupenda sana, siku moja naweza kufa kama nitaendelea kuishi na wewe"

Mapenzi ya siku hizi, everyone either he or she is on guards every time. Unakua ka vile upo kwenye mahusiano na some sort of nemesis. Kila siku mashindano, who talk more smarter,more responsible, more everything.....

All in all deep down within us, ipo roho yenye upendo ila tunaogopa kupenda. Love has become a vice not a virtue
Tehe! Mguu mmoja ndani mwingine nje.
 
T

True, amuwezi kufikia level za kina Obama Kama ni mmoja tuh anayepigania ilo penzi, lazima achoke ata awe na upendo wa aina gani,
Simama kama mwanaume wa kweli ili upate nawe kulia kama Obama,...
Yap! Upendo unatakiwa uwe two ways.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom